2017-05-22 14:43:00

Kard.Filoni:Jimbo Jipya la Evinayong litunzwe kama kitoto kichanga!


Baada ya Misa ya Jumapili 21 Mei 2017 katika Jimbo Jipya la Evinayong nchini Equatorial Guinea Kardinali Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu alikutana na Mapadre na watawa wa jimbo jipya ili kuweza kuongea nao. Hawali ya yote ametoa salam na Baraka kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko aliyemteua kwenda kumwakilisha nchini humo kwasababu ya tukio la kutoa wakfu wa kiasikofu kwa maaskofu watuele watatu wa Kanisa Katoliki la Equatorial Guinea. Pia salam nyingi kwa Askofu mteule wa jimbo hilo Jipya la Evinayong Calixto Paulino Esono Abaga Obono,akimpongeza tena na kumtakia matashi mema  na kumwakikishia  kumsindikiza kwa sala ili utume wake mpya wa kiaskofu uweze kuwa na furaha  na matunda mema. Aidha hakumsahau pia Balozi wa kipapa katika nchi hiyo  na kumpongeza kwa shughuli nzuri waliyoitenda katika kutafuta ufumbuzi wa kuunda jimbo la Evinayong kwa lengo la  kufanya utume mzuri zaidi.

Akieleza jinsi ya mchakato wa jimpo jipya lilivyo kuwa linahitajika  Kardinali Filoni amesema, katika Mkutano wa  kawaida wa mwaka wa Baraza la Maaskofu uliofanyika tarehe 27 na 28 Juni 2011 Maaskofu wa Equatorial Guinea walikuwa wameonelea kuweka  kipaumbele katika kuunda maeneo mengine ya kitume mapya kwasababu ya huduma ya kichungaji na mipango ya Kanisa kwa ujumla. Walikuwa na lengo la kuweka kipaumbele zaidi cha uinjilishaji na wakati huo huo kuhakikisha mafunzo ya kina kwa waamini wakristo na  kama vile kuwaandaa waamini kuvumilia suala la maingilio ya madhehebu mapya. Hiyo ni kutokana na hali halisi ya Kanisa kwa ujumla ambalo lilikuwa na linaendela kukua ,ili kuweza kunza kwa upya utume wa kueneza Injili ambayo pia ilitakiwa kuwa na chombo cha  utawala muhimu kama jimbo , pia mipango mizuri ambayo inakaribia zaidi waamini na kuwasaidia kwa badhi ya ushauri, na pia katika maendeleo ya kiroho na kimaadilili kwa ajili ya makuhani.

Kwa njia hiyo katika malengo hayo yaliyokuwa yamekusudiwa tangu 2011 , Kardinali Filoni anabainosha kwamba  hayo siyo kwamba yanamsubiri askofu peke yake kufanya kazi ili kufika malengo hayo.Anachukua furaha ya  mkutano  huo kuwatia moyo katika baadhi ya ushauri ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto ambazo zilizopo: Ili kufika malengo hayo ni lazima kushirikiana wote pamoja na Askofu ili kuweza kuendeleza mbele jimbo . Jimbo limekuwapo ili wote wajisikie ndani yake kwamaba ni wazalendo na wanao wajibu wa utume wa kikuhani kwa njia ya muungano kamili na Askofu  ambaye amechaguliwa kuwa Baba wa kudumu  na mchungaji wa Kanisa .

Kardinali Filoni anawaeleza kuwa, wapende Jimbo na kuwa tayari kushirikana kwa uaminifu na ukarimu katika maisha ya utume kichungaji. Pamoja na kuwa wataalamu wa kikuhani na kichunagaji , lakini pis wanapaswa kuwa na uwezo wa kubuni na kupanga.Ni lazima kila mmoja ajisikie kuwajibika kwa dhati ili kuendeleza kwa moyo wote Jimbo jipya ambalo limepewa kiongozi mwema katika uchungaji. Aidha amesema kama wachungaji na watawa ambao ni wahusika wa Kanisa mahalia, wanaitwa kuwa chumvi na mwanga katika jamii kwa kufuata mfano wa Bwana mchungaji. Hawana budi kuishi kwa uaminifu na furaha ambayo ndiyo utambulishi wao kama mapadre na watawa. Wao ni lazima kutangaza Neno na maisha,laikini  hiyo itawezekana tu iwapo Kanisa litapewa kipaumbele kwenye utume wa kudumu na siyo katika uwepo wa jengo tu.

Ili kuweza kudumu daima katika maisha ya wakfu wa  kikuhani na utawa, Kardinali anatoa ushauri hasa ule wa  kuweze kupata fursa za mafunzo ya kudumu  ya kiroho, ambapo ameomba Askofu mpya aweze kushughulikia hilo suala ili wapate kuwa waaminfu katika utume wa  kikuhani na kwa watawa wote  kwa ujumla ambao amesema, hiyo ni safari ya uongofu daima ili kuweza kuishi kiukamilifu tunu msingi ya daraja la upadre. Amewatakia matashi mema ya kuendeleza mbele huduma ya unjilishaji ambayo wanajikita nayo wakiongozwa hawali ya yote na upendo wa Bwana  na kwa ajili ya Mama Kanisa. Wabaki katika umoja na sala  ili mama Maria mfano mzuri wa umisionari kwa Kanisa apate kuwafundisha kujitoa na kutunza kila siku fumbo la Bwana na mwanaye aliyefufuka ambaye anaendelea kufanya mambo mapya zaidi ya kujaza furaha na huruma pamoja na uhusiano mzuri wa watu, tamaduni na watu wote.

Mwisho amesema ujenzi wa jimbo jipya la Evinayong unategemea na wao,kujenga Kanisa kwa mujibu wa moyo wa Yesu, wainuke kwa pamoja kutembea na Kanisa lao,na Roho Mtakatifu awape faraja ya ndani katika shughuli yao ya kitume.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.