2017-05-21 15:45:00

Papa:Katika umoja na Baba Kanisa ni chemi chemi ya kisima cha upendo


Injili ya leo kutoka Mtakatifu Yohane sura ya 14 haya ta 15 hadi 21 (Yh 14,15-21) ni mwendelezo wa Injili ya Jumapili iliyopita ambayo inaturudisha nyuma katika tukio la Karamu ya Mwisho ya Yesu na mitume wake. Mwinjili Yohane  anakusanya mafundisho yake ya mwisho  kutoka mdomoni na moyoni mwake Bwana kabla ya mateso na kifo. Yesu anatoa ahadi kwa mitume wake , kwamba baada yake atawapatia msaidizi mwingine atakaye kaa nao milele, anaongeza kusema sitawaacha ninyi yatima maana nitakuja tena kwenu.

Ni maneno ya Utangulizi wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko Jumapili ya sita ya Kipindi cha Pasaka aliyotoa wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu tarehe 21 Mei 2017 kwenye viwanja vya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Baba Mtakatifu anasema; Maneno haya yanaonesha furaha ya ujio wake mpya wa Kristo. Yeye amefufuka na kutukuzwa , anaishi pamoja na Baba , wakati huo huo anakuja kwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Ujio wake unajionesha katika muungano wetu na yeye na Baba: kwa maana yeye anasema ; “siku ile mtakapofika  mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba nanyi mko ndani yangu, nami ndani yenu”.

Katika kutafakari maneno ya Yesu leo hii sisi tunatambua maana ya imani ya kuwa watu wa Mungu katika umoja na Baba na Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Katika fumbo la umoja , Kanisa linapata chemichemi ya kisima kisichokauka cha utume wake mwenyewe ambao ukamilika kwa njia ya upendo. Yesu anasema katika  Injil ya leo hii  “azipokeaye amri zangu na kuzishika , yeye ndiye anipendaye. Yeye anipendaye mimi nitampenda na kujidhihirisha kwake.” Baba Mtakatifu anaongeza kusema kwamba ni upendo unaotutambulisha katika kumtambua Yesu kwa neema ya Roho Mtakatifu. Upendo wa Mungu na jirani ndiyo mkubwa zaidi ya amri katika Injili. Leo hii Bwana anatualika kujibu kwa ukarimu wito wa kiinjili ambao ni upendo. Kumweka Mungu awe kiini cha maisha yetu na kujitoa katika kutoa huduma kwa  ndugu hasa wenye kuhitaji  msaada pia kuwatuliza.

Aidha anabaisha tabia ambazo siyo nzuri kwa upande wa Jumuiya za kikristo, na hivyo na hivyo wanapaswa kupenda na kutakiana mema kwa kuiga mfano wa Bwana na neema zake, kwani kinyume na hayo Baba Mtakatifu anataja kuwa, kuna kiburi, wivu na mgawanyiko ambao unaleta ishara mbaya katika sura ya Kanisa lililo zuri.  Kwa njia hiy anaongeza; Jumuiya ya Kikristo ni lazima kuishi kwa upendo wa Kristo, kwani bila kufanya hivyo ubaya unaweka mguu wake wakati huo huo sisi hujiachia na kutumbukia katika udanganyifu.

Watakao lipa ni watu wenye roho dhaifu. Ni wangapi walio kwenda mbali, ambao wanajisikia kutokukbalika, kusikilizwa na kupendwa. Hata kwa upande wa Mkristo kujua kupenda siyo jambo la kunua mara moja na daima, bali kila siku inabidi kuanza upya kupenda, ni lazima kufanya mazoezi kwasababu upendo wetu tunao utoa kwa ndugu zetu tukutanao  njiani kila siku uweze kukomaa na kutakaswa na uadhaifu wake au dhambi kama zile za ubinafssi, utasa na kutokuwa waaminifu. Kila siku ni lazima kujifunza sanaa ya upendo ,kila siku ni lazima kufuata kwa uvumilivu katika shule ya Kristo kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Mama Maria mtume na mkamilifu wa mwanaye  Bwana wetu atusidie daima kuwa wapole kwa Roho Mtakatifu, wakweli katika kujifunza kila siku kupenda kama alivyo penda Yesu.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.