2017-05-21 13:02:00

Papa: Amewataja Makardinali wapya kutoka sehemu tofauti za dunia!


Baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Baba Mtakatifu Francisko amesema kwa masikitiko makubwa ya taarifa zenye uchungu kutoka katika nchi ya Afrika ya kati ,na kwamba wako rohoni mwake hasa mara baada ya ziara yake ya  huko Novemba 2015. Mapigano hayo yamesababisha idadi kubwa ya waathirika na watu kukosa maahali pa kukaa ,aidha machafuko  haya yanasababisha kukwama mchakato wa amani. Baba Mtakatifu anasema yuko karibu kiroho na watu wote maaskofu na wale wenye mapenzi mema kujikita katika kusadia watu na kutafuta amani ya kuishi. Aidha anasali kwa ajili ya marehemu wote na majeruhi, na kutoa wito kwamba vita vya kutumia silaha visitishwe na ili kutafuta matashi mema ya mazungumzo ambayo yanaweza kulte  amani ya kudumu na maendeleo ya nchi.

Amesema tarehe 24 Mei 2017 wataunganika wote kiroho na waamini wakatoliki wa nchi ya China kwa ajili ya sikukuu ya Mama Maria msaada wa Wakristo, anayetolewa ibada katika Madhabahu  huko Sheshan wa Shanghai.  Na kwa wakristo wote wa Cina Baba Mtakatifu anasema; wainue macho yao kwake Maria mama Yetu ili aweze kutusadia kutambua mapenzi ya Mungu katika safari ya dhati ya Kanisa la China na kuwaimarisha kupoka kwa ukarimu mpango  wake wa upendo. Mama  Maria anatutia moyo wa kujitoa sisi wenyewe katika kujikita kwenye umoja kati ya waamini na ushirikiano wa jamii nzima. Anaongeza; msisahau kushuhudia kwa imani na sala na upendo na kuwa wazi katika kukutana na kuzungumza daima.

Aidha Baba Mtakatifu Francisko wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu amewataja majina ya Makardinali 5 wapya watakao ungana katika Baraza la Makardinali  tarehe 28  Juni  2017.  Baba Mtakatifu Francisko amesema, hawa kutoka pande zote za dunia ambapo ni kutaka kuonesha ukatoliki wa Kanisa ulivyo sambaa dunia nzima , ambapo pia wanawakilisha jina la umoja wa parokia ya Roma inayoshuhudia uanachama wa Makardinali kwa Jimbo la Roma ambaye anaongoza kwa upendo katika makanisa yote.

Makardinali wapya wanatoka katika nchi ya Malì, Hipania, Sweden, Laos na San Salvador. Ibada Takatifu ya Misa ya kusimkwa kwao itakuwa tarehe 29 Juni 2017 katika Sikukuu ya Watakatifu Petro na Paulo.
Majina yao ni  Monsinyo. Gregorio Rosa Chávez, askofu msaidizi wa San Salvador (Salvador) ;Askofu Mkuu Jean Zerbo,wa Jimbo Kuu wa Bamako (Mali); Askofu Mkuu  Anders Arborelius, wa Stockholm -  (Sweden); Askofu Mkuu  Juan José Omella, wa Jimbo Kuu la  Barcellona (Uhispania): Askofu Mkuu Louis-Marie Ling Mangkhanekhoun, msimamizi wa kitume huko  Paksé (Laos).

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.