Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu,
ambaye tangu tarehe 18 hadi 25 Mei 2017 atakuwa katika hija ya kitume nchini Equatorial
Guinea Jumamosi tarehe 20 Mei 2017 ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu na kuwaweka
wakfu Maaskofu watatu wapya walioteleuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Francisko.
Katika mahubiri yake amesema Baba Mtakatifu Francisko mtume wa Khalifa Petro mtume
wa Yesu amepata uwezo wa kuwaimarisha ndugu kwa ishara ya kibaba juu ya watu wa Equatorial
Guinea , kwa njia ya peke ya kufikiria jumuiya ya wanakatoliki wapendwa wa nchi hii.
Tarehe 1 Aprili 2017 walitoa uamuzi wa kuunda majimbo mapya ya Mongono na Evinayong,
na kuteua askofu mchungaji mwingine kwa ajili ya jimbo lililobaki wazi la Ebebiyin.Na
kumteua Askofu mpya mteule Juan Domingo-Beka Esono Ayang wa Jimbo Katoliki Mongomo.
Askofu jimbo jipya mteule Calixto Paulino Esono Ebaga Obono, Askofu wa kwanza wa
Jimbo jipya Katoliki la Evinayong. Askofu mteule Miguel Angel Nguema Bee, amewekwa
wakfu kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ebebiyin.
Kardinali Filoni anaendelea, hawa na watoto watatu wa nchi hii ambapo Bwana Yesu kwa njia ya liturujia ya daraja la kutoa wakfu wa kiaskofu wanapewa zawadi ya Roho Mtakatifu katika ujazo wa kikuhani. Wao wameitwa kwa ajili ya kutoa huduma ya Mungu na huduma ya jumuiya ya kikristo kama makuhani. Leo hii wanaalikwa kujikita katuka Kanisa kama Baba na wachungaji wa watu wa Mungu ambao wamekabidhiwa , watu walio kombolewa na kutakatifuzwa na Kristo kwa njia ya sadaka msalabani.Kama tunavyotambua nchi ya hii inashi kipindi muhimu cha kihistoria katika kuachanua kwa uinjilishaji. Kwa njia ya kuimarisha utume wa kimisionari ambao ulianzishwa wakati uliopita na wamisionari wa nyakati zile ambao walijitoa maisha yao kwa ajili kueneza Injili na maskini , uamuzi huu wa Baba Mtakatifu ni kutaka kundeleza mchakato mzima kwa ndani ya nchi ambao ni kwa ajili ya maendeleo ya Kanisa katika nchi hii.
Kipindi hicho cha kihistoria , kinawakilisha utambuzi wa safari ya ukomavu wa historia
ya sasa licha ya matatizo mengi ya wakati ulio pita. Kwa njia hiyo Kardinali Filoni
anapendelea kutoa pangezi kushiriki kati yao siku njema ya kipekee akimwakilisha Baba
Mtakatifu aliyemtuma kuwatia moyo waamni na watu wote wa chi.Kwa namna hiyo amesema
anatoa salam kwa Rais wa nchi hiyo na watu wake wote.
Lituturujia ya neno la Mungu lilongoz maadhimisho yao limetaka kukumbusha kwamba
tunacho kitenda leo hii siyo tofauti na maisha ya wakristo wa kwanza miaka 2000 iliyopita.
Kwa dhati baada ya kupaa kwa Bwana mitume walitambua kwamba katika Kanda ya Samaria
walikuwa wamepokea Neno la Mungu na wakaamua kumtuma Petro na Yohane, ili mwisho waweze
kutambua jinsi gani watu wa Samaria walikuwa na imani. Katika mji wa Samaria yaliishi
makundi ya ambayo hayakuwa ni ya kiyahudi, lakini ambao walina kuundwa kwa jumuiya
ya wafuasi wa Yesu na hivyo ilikuwa muhimu wa uwepo wa utume ili kuweza kugundua
na kuwahimarisha waamini wake imani.
Kwa maana hiyo katika nchi hii ya Guinea, Neno la Mungu lilipandwa na wamisionari
kwa miongo mingi iliyopita , ambao waliunda jumuiya za kwanza za kikriso na pia vikawepo
vituo vya kwanza vya kimisionari na maparokia ya kwanza , na mwisho kuundwa kwa majimbo,
ambayo yaliongeza kutoa matunda ya Kanisa la Gunea : Yote hayo yaliwezekana kwa neema
ya Neno la Mungu kutangazwa na kupokelewa na mababu zenu .
Halikadhalika amesema; utume huo unaendelea na kfanya kwamba Baba Mtakatifu anawapatia
maaskofu wapya watatatu wanao wekwa wakfu. Wao watakuwa na jukumu kama hilo la Petro
ana Yohane , wa kuimarisha na kukuza mbegu ya Neno la Mungu . Wao watakuwa kwenu kama
Baba na wachungaji. Hiyo ni kwasababu Balozi wa wa Kitume wa Vatican wakati wa mchakato
wa kutafuta maaskofu wapya alipowauliza waamini kutaka kujua ni askofu gani wanayemtaka
wengi waliandika kwamba wawe watu wa Mungu, wa sala, baba na kuwa wachungaji na
siyo tu kuwa viongozi.
Kardinali Filioni akiwageukia maakofu walioitwa katika daraja wa kiaskofu: hawali
ya yote wanapaswa kuwa watu wajasiri, thabiti katika kutoa ushuhuda wa imani , na
kwa njia hiyo wawe wahamasishaji wa huduma ya uinjilishaji na wahudumu wa watu wa
Mungu ambao wamekabidhiwa. Wao ndiyo wako mstari wa mbele katika kuwajibika kwanza
katika utume na kwa njia yao wanaungana na mapadre, watawa na walei wote kwa ukarimu
katika utashi wa kishirikiana nao. Anawashurukuru kwa ajili ya kukubali kwa ukarimu
utume huo mgumu wa shughuli ya Kanisa.
Kardinali Filoni anaongeza kuwaeleza kwamba, wao siyo viongozi wa kabila au wa serikalii
, bali ni wachungaji daima wa wote. Wito wa kuwa askofu daima ni ule unaokufanya
kuwa tayari kufanya mapenzi ya Bwana. Kwa njia hiyo kuna uraha na mateso.Lakini
kama vile katika familia yenye , baba, mama na watoto, hapakosekani kipindi cha furaha
na mateso, na hivyo hata wao mambo hayo hayatakosekana.
La muhimu ni kutambua katika upeo wa kikriso yote ni zawadi na neema kwa Mungu
. Sisi hatuwezi kamwe kusema tunasatahili mbele ya mengi tunayopokea kutoka kwa Bwana.
Hiyo ni dhahiri kwasaba bni yeye kwanza anayetuita na pia kujua mahali gani anatutuma
katika utume wa kuendela kutangaza Injili na kusaidia kuimarisha Kanisa.
Bwana amewachagua siyo kwa ajili ya mastahili yenu labda zaidi ni kwa ajili ya mapuungu
yenu, na kwa njia hiyo asiwepo hata mmoja wenu kujidai. Kumbukeni maneno ya mtume
Petrombele ya Yesu aliyekuwa anataka kumkabidhi zizi lake aliongoze , alitamka kwa
unyenyekevu kwamba nenda mbali na mimi Bana maana mimi ni madhambi , lakini wajua
ni jinsi ani ninakupenda , wajua udhaifu wangu.Hata hivyo Bwana aliweza kumwimarisha
na kumkabidhi Kanisa lake.
Mwisho amesema kwa wote wote wambaao yenye sura ya kanisa Kuu moja na majimbo manne nchini Guine kwamba wanapaswa kusaidia kujenga kwa kina umoja kwa ajili ya wema wa watu wote wa nchi. Uwepo wa majimbo mawili mapya , maaskofu wanateza kuwa karibu na watu na kwa njia hiyo Kardinali Filoni anamatuamani ya kwamaba wanateza kuwafikia .Kwababu haya majimbo yameundwa kwa ajili ya kutaka kuwasaidia ninyi. Lakini kumbukeni kwamba majengo tu hayatoshi iwapo utakosekana ushirikiano. Jambo muhimu ni kuimarisha uwepo wenu na kuwa sehemu ya Kanisa katika ulimwengu , kama vile katika majimbo yenu mahalia kushirikiana katika maisha ya jumuiya na kuyafanya yakue.
Kwa namna ya pekee majimbo mapya ya Mongomo na Evinayong, ni kama karatasi nyeupe
isiyokuwa na maandishi kwa ajili ya kuandika katika kitabu kikubwa cha Kanisa. Ni
nyinyi manaopaswa kuandika historia ya maisha ya kila mmoja , kwa kushirikishana na
kuifanya ikue kwa furaha na ukarimu.
Ndugu wapenda upendo ni nguvu na kujenga na kukuza, kwa njia hiyo penda Kanisa lenu
na kulisaidia zaidi badala ya kulichambua na kubainisha makosa. Ni kwa njia ya kupenda
na kushirikiana mnaweza kiimarisha na kufanya ukue utume wa kuinjililisha. Maendeleo
endelevu ya maadili ya Kanisa la Guine iko mikononi mwenu, Maskofu wenu ni wazalendo
kama ilivyo mapadre wenu, na watawa wenu. Uamuzi uko mikononi mwenu !
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |