Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Kard.Filoni: Makuhani na watawa tambueni vema wito wenu na Kanisa

Makuhani na watawa Daima wawe thabiti na waaminifu kwa kuiga Mfano wa Mtakatifu Yohane Maria wa Vianney aliyekuwa akiwafundisha wanaparokia wake kwa njia ya ushuhuda wa maisha yake. - RV

19/05/2017 17:17

Mara baada ya Mkutano Kardinali Filoni katika Kanisa Kuu la Malabo nchini Equatorial Guinea tarehe 19 Mei 2017 ameadhimisha Ibada ya MisaTakatifu kwa Wakleri na watawa, ambapo mahubiri yake yametokana na masomo  kutoka katika kitabu cha matendo ya mitume na Injili ya Mtakatifu Yohane kuhusu upendo upeo. Katika mahubiri yake amesema, mkutano umemalizika muda mfupi, sasa tuko mbele ya Altare katika Kanisa Kuu na zuri la Mtakatifu Isabel wa Malabo. Maadhimisho ya Ekaristi takatifu ni mwafaka wa kuishi muungano wa kina na Kristo kati yetu kwa njia ya sala, kusikiliza Neno pamoja na kupokea mwili na damu yake Bwana.  Hiyo ni kwa sababu kuna mwili mmoja japokuwa sisi ni wengi lakini tunaunganika kwa pomoja katika kuumega mkate (1Ko 10,17). Neno muungano kwa mujibu wa Mtakatifu Paulo ni kuelezea uhusiano wa kina kati ya wakfu, kwa maana anabainsha umoja wa kina kati ya waamini na Kristo . Kwa kuwa tumeunganika katika ekaristi, lazima kuunganika kati yetu na kupokea maisha ya umoja wa mwili wa Kristo alioutoa kwa ajili ya binadamu wote.

Upendo na kujitoa yeye binafsi ni aina mbili za maeneno yanayojitokeza katika neno ambalo limesomwa, ni kwa maana ya kufundisha thamani muhimu ya kuishi na uhusiano wa ndani katika jumuiya ya Kanisa, makuhani na watawa. Hawali ya yote tunapaswa kuwa na utambuzi kwamba wito wa kikristo kama kuhani na watawa ni zawadi ya bure ya Mungu. Kwasababu yeye anasema” Ninyi hamkunichagua mimi; ni mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, na matunda yadumuyo” (Yh 15,16). Ni Yesu aliyetuchagua kwasababu siyo sisi tulio mchagua , na uchaguzi huo siyo kwamba tuna mastahili au kwa ajili ya hali ya kijamii au kiutamduni na kwa ngazi zozote.

Hii ni sehemu ya fumbo la Mungu mwenyewe ambaye ni mwingi wa huruma na aliye jaa upendo. Kwa mana hiyo wito huo unapaswa kutambuliwa vema na kuishi kiukweli, maana imani nakujikita katika matendo ya dhati. Kwa kujibu wito huo, ni lazima kujitoa kabisa bila kubakiza kwa Mungu na mwanae Yesu ambaye ni kama chombo safi cha  huduma na ishara ya wokovu wa dunia nzima. Hatuna budi kijiachia ili kutengenezwa na yeye kama mfinyanzi atengenezavyo chungu cha udongo. Sisi tuna haja na yeye, na Yesu mwenyewe anayo haja na sisi kwa ajili ya utume wake ili upate kuendelea leo hii kwa watu wake kama yeye alivyokuwa akifanya wakati ule kwa masikini na rahisi.

Yesu anawaita mitume marafiki na siyo watumishi (Yh 15, 14), Ninyi ni marafiki lakini mkifanya ninayo wahamuru; kwa maana ya kuwa na matendo ya upendo wa kujitoa binafsi kwake. Wakati huo huo alipokuwa akiwaalika katika upendo mkuu, alikuwa akiwakilisha mawazo makuu ya maisha yao mitume. Ni kwasababu aliwambia hatawaita watumishi kwani mtumishi hajuhi atendalo bwana wake. Ninawaita rafiki kwasababu yote niliyosikia kwa baba nimewafanya nanyi kuyatambua. Yesu hakuwa na siri kwa mitume wake; aliwasimulia kila kitu alichosikia kutoka kwa baba. Na hiyo ndiyo mawazo sahihi ya kuishi maisha ya jumuia, Kardinali Filoni anasisitiza : yaani kufikia katika uwazi kamili wa kutokuwa na siri yoyote kati yenu na kuaminiana kati yenu, maana ndiyo kkukuza uzoefu ambao mnauchota kutoka kwa Mungu katika maisha na kuweza kutajirishana ninyi kwa ninyi.

Licha ya hayo  anasema; Wakristo wa kwanza walifahuru kufikia mawazo hayo baada ya miaka mingi. Kwana waliishi kwa moyo mmoja na roho moja (Ndo 4,32; 1,14; 2,42.46). Anabainisha Kardinali, jueni ya kwamba katika Jumuiya zenu, anayetafuta kuishi furaha kivyake, anayeishi kibinafsi, anakwenda mbali na upendo. Kinyume chake  anayependa kuishi upendo wa dhati anapaswa kujikana furaha binafsi, na kujifungua kuwa wazi kwa wengine. Kama alivyosema Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wa Furaha ya Injili kwamba “ anayejikana binafsi na kuungana na wengine ni vizuri  kwasababu kujifunga binafsi maana yake ni kuishi kiuchungu na sumu isiyomalizika na ubinadamu uaathirika vibaya sana kwa kila chaguo lolote binafsi lifanyikalo.  Upendo ambao Yesu nataka wafanya mitume wake , unahitaji kujitoa binafsi moja kwa moja kwa ajili ya jirani, na kukataa aina zote za ubinafsi na ubaguzi. Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake (Yh 15, 13). Amri yake ni moja nayo  ni  “hii ndiyo amri yangu pendaneni kama nilivyo wapenda ninyi” (Yh 15,12).

Kardinali Filoni anabainisha kuwa, Yesu anazidi  Agano la Kale , ambalo lilifundisha mantiki ifuatayo “ mpende jirani yako kama wewe binafsi” na sasa amri mpya ni  yenye mantiki yake kwamba, mpendaneni kama nilivyo wapenda: hiyo ndiyo anatoa kama mtindo wa kupima upendo kati ya mitume. Yeye anajitokeza kama mwalimu anaye jionesha na siyo kwa njia ya maneno tu bali  katika matendo, yaani ni maisha ya kufuata  kwa ajili ya kupenda kama yeye; kujikana binafsi na kubeba msalaba. Hiyo ndiyo wajibu wa muungano kati ya makuhani mlioitwa kutenda kati yenu na maaskofu. Kwa kufanya hivyo ni lazima kufikiria jinsi gani Yesu alipendelea kuanzisha fumbo hili la ukuhani katika jumuiya na umoja wa kikuhani.

Yeye aliwapokea mitume wake wa kwanza kumi mbili  akawaita kwa kuunda umoja wa upendo. Jumuiya ya kwanza ya kikuhani aliitaka iwe ya umoja na kushirikiana, kwa kuwatuma waende kwenye utume, hata sabini na wawili, kama vile wale kumi na wawili kwenda wawili wawili (Lk 10, 1; Mk 6, 7). Na hiyo ilio waweze kusaidiana katika maisha yao ya utume na kuonesha umoja kama mtindo wa maisha  na asiwepo anayetenda peke yake bali kutegemeana na jumuiya ambayo ni Kanisa na jumuiya ya mitume. Amemaliza akiwata mapadre na watawa wote kuwa na utambulisho wa kikuhani  katika utume. Daima  wawe thabiti na waaminifu kwa kuiga Mfano wa Mtakatifu Yohane Maria wa Vianney aliyekuwa  akiwafundisha wanaparokia wake kwa njia ya ushuhuda wa maisha yake. Yeye alikuwa   maskini, alijikita kusaidia maskini kwasababu wasiwasiwasi wake ulikuwa ni  ukombozi wa roho za watu:  kwa njia hiyo wao wenyewe wawe mfano kwa waamini wao na katika jumuiya iliyoanzishwa na upendo wa Yesu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 

19/05/2017 17:17