Kila mwaka Ulaya karibu tani milioni 90 za ya vyakula zinatupwa kwenye jalala. Ni matumizi mabaya yanayohusisha hata familia: kila mzalendo anatupa chakula kwenye takataka karibu kilo mbili kila siku ambazo bado zinangeweza kutumika kwa wiki. Ni takwimu za kutisha kabisa za kutokuweza kuvumilai ukifikiria kwamba katika maeneo mengi ya sayari hii watu wengi wanakufa kwa njaa. Kwa njia hiyo, Kamati ya Shirikisho la Baraza la Maaskofu Ulaya (Comece ) wametafuta ufumbuzi wa pamoja mapema wiki hii katika Bunge la Ulaya, wakitoa wito wa nchi wanachama wa Ulaya kupunguza matumizi mabaya ya chakula.
Katika Gazeti Osservatore Romano linaandika , Bunge la Ulaya huko Bruxelles ,
wamesema kupunguza matumizi mabaya ya vyakula kwa asilimia 30% kufikia mwaka 2025
, na asilimia 50 kufikia mwaka 2050 kulingianishwa na mwaka 2014.
Kati ya maombi mengine yaliyotolewa ni kutafuta ufumbuzi wa kutokuwa na vizingiti
vya kusaini na mbunge wa Croatia Biljana Borzan, ambaye ametoa kodi ya kutoa chakula
inayohusiha Kanisa la Ulaya na pia viongozi wa kila mwanachama wa Ulaya, ili waweze
kuwa wazi kwenye tiketi zinazoonesha muda wa matumizi ya chakula kinachotolewa na
mwisho wa matumizi yake.
Katika ujumbe uliotolewa katika mtandao wa Kanisa, Padre Olivier Poquillon wa Shirika
la Kidomenikani , ambaye ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Ulaya
anabainisha kuridhika na jinsi walivyotafuta ufumbuzi muhimu ambao ni mwongozo wa
Baba Mtakatifu Francisko, ambao mara nyingi amesisitiza bila kuchoka akipinga utamaduni
wa kubagua, ambao daima unawaacha waathirika kutokana na matumizi mabaya ya vyakula.
Ni mada ambayo Baba Mtakatifu alikumbusha katika hotuba yake kwenye Bunge la Ulaya
tarehe 25 Novemba 2014 , akisema, haiwezekani kuacha mamilioni ya watu wanakufa duniani
kwa ajili ya njaa wakati tani za vyakula vinaendelea kutupwa kila siku katika meza
zetu.
Kwa mantiki hii Katibu Mkuu wa (Comece) anabainisha kwamba kura za Bunge la Ulaya
zinapaswa kutafakari kwa kina na kamati ya Ulaya kama Ishara ya kutia moyo , ili
kuweza kuharakisha sheria ya dhati ya Baraza la Ulaya kujikita katika matendo kwa
ujasiri, kuwawezesha watu na hasa wadahu wake kwa namana ya pekee watumiaji ili kuondoa
ile kashfa ya matumizi mabaya ya kutupa vyakula.
Shirikisho la Baraza la Maaskofu Ulaya (Comece), linatatarajiwa mawazo ya malengo hayo kutotiliwa vizingiti maana yanakwenda sambamba na malengo ya melendeleo endelevu ya Umoja wa mataifa. Hiyo ina maana kwamba Tume ya Ulaya lazima kuimarisha kazi yake; kwa mtazamo huo, kazi muhimu zaidi ni kuwafanya wanaulaya wawe na ufahamu wa madhara ya kijamii ya kutupa chakula ambacho bado kinaweza kutumika . Hivyo Parokia na harakati za vyama vya Kikanisa ni lazima kuhakikisha kutoa machango wao wa kuhamasisha zaidi jamii.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |