Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Ni kufuru kutumia jina la Mungu kufanya mauaji! Dumisheni amani!

Papa Francisko anawataka Mabalozi wapya waliowasilisha hati zao za utambulisho mjini Vatican kujikita zaidi katika kukuza na kudumisha misingi ya haki, amani, maridhiano na kuachana na misimamo mikali ya kidini inayopelekea maafa makubwa kwa watu na mali zao!

18/05/2017 16:36

Ni furaha yangu kukutana nanyi wakati wa tukio la kuwasilisha hati za utambulisho wenu kama Mabalozi wapya wa Vatican kutoka kuwakilisha nchi zenu Kazakhstan, Mauritania, Nepal, Niger, Sudan, Trinidad na Tobago. Makaribisho muhimu ya Bi M’Haiham Balozi wa kwanza mpya Kutoka Mauritania katika Ubalozi wa Vatican nchini humo. Nitashukuru iwapo mtawafikishia kwa wakuu wa nchi zenu  hisia zangu za shukurani na heshima zikiambatana na maombi yangu kwa ajili ya watu mnao wawakilisha. Ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoitoa Tarehe 18 Mei 2017 alipokutana mabalozi wapya mjini Vatican kuwakilisha nchi zao Kazakhstan, Mauritania, Nepal, Niger, Sudan, Trinidad na Tobago. Baba Mtakatifu Francisko amesema, katika maeneo la kimataifa kuna utata mkubwa, mgumu na wenye mawingu meusi, kwa njia hiyo inahitajika uelewa mkubwa na utambuzi wa mwenendo wake il kutafuta mbinu na hatua muhimu zinazohitajika ili kuingilia kati katika kujikita katika kwa njia ya amani na kupunguza mvutano. 

Miongoni mwa mambo yanayozidisha matatizo hayo ni pamoja na uchumi na fedha ambavyo badala ya kuhudumia hali halisi ya mwanadamu,hiyo hupangwa na kutumika wenyewe binafsi, pia kuepuka udhibiti wa mashirika ya umma ambayo hubaki kwa manufaa ya wote, lakini wakati huohuo hukosekana usimamizi thabiti ambapo kuishia kushibisha matumbo ya walio wachache.  Baba Mtakatifu Francisko  anaongeza, pia kuna ongezeko kubwa la matumizi ya fedha kwa kuzingatia matumizi binafsi ambayo siyo kwa ajili ya kuleta usawa bali miongoni mwa wengine hutumia bila kutathimini kwa kina matokeo yake. Sababu nyingine inayosababisha migogoro ni itikadi kali katika matumizi mabaya ya dini ambayo uhalalisha kiu ya utawala. Hutumia jina takatifu la Mungu kwa njia zozote ili kuendeleza mpango wake binafsi.  Katika hatari hizi zinazosababisha ukosefu wa amani duniani, inabidi kujibu kwa kujenga uchumi na wahusika wa kifedha kwa ajili ya hatma ya binadamu na jamii ambayo wanaishi.

Ni mtu na siyo fedha au mwisho wake kuishia katika uchumi; Baba Mtakatifu anasema ni lazima kushughulikia matukio haya kwa njia ya uvumulivu kijasiri  ya mazungumzo na kidiplomasia, kuanzisha mikutano ya amani na siyo utendaji wa nguvu na kutumia haraka ya kuwaingilia watu  na kutowafikiria. Pia ni muhimu kubaini mtu yeyote ambaye anajaribu kubuni au kuunda uanachama na utambulisho wa dini  kwa lengo la chuki kwa watu wengine. Baba Mtakatifu anawaalika akisema; kwa yeyote anayetaka kutumia jina la Mungu , awe na juhudi za kuonesha kwamba heshima na jina lale ni kuokoa maisha na siyo kuua; kwa kuleta maridhiano na amani, na siyo mgawanyiko na vita; ni pamoja na huruma na upendo na siyo kutojali au ukatili. Iwapo tutasonga mbele katika katika mwelekeo huu, ambayo ndiyo sababu ya amani na haki, masharti ya maendeleo ya uwiano kwa wote yatakuwa ni hatua madhubuti siku za usoni.

Aidha kwa njia ya mabalozi hao ametuma salam kwa wachungaji na waamini wa jumuia za Kikatoliki zilizopo katoka nchi zao. Anawatia moyo kuendelea na ushuhuda wa imani na kutoa mchango wao kwa ukarimu kwa ajili ya wema wote. Na mwisho ametoa baraka zake kwao na familia zao , ikiwa pamoja na watu wa nchi zao , ili amani tele kutoka kwa Mungu iwafikie.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

18/05/2017 16:36