2017-05-17 16:29:00

Mtakatifu Maria Magdalena ni mtume wa matumaini ya Kikristo!


Mara baada ya kusoma Injili ya Siku iliyochaguliwa kuongoz Katekesi ya katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko ya Jumatano 17 Mei 2017 ameanza na tafakari yake kuhusiana na tukio la Pasaka, kwasababu bado Kanisa linaendelea na kipindi cha Pasaka na kusema; katika wiki hii tafakari yetu bado inaendelea na fumbo la Pasaka. Leo hii ni kukutana na mmoja ambaye katika Injili wanasema Maria Magdalena ndiye aliyekutana na Yesu akiwa wa Kwanza. Ilikuwa imekwisha siku ya mapumziko ya Jumamosi. Ijumaa hapakuwepo na nafasi ya kumalizia utamaduni wa mazishi, kwa njia hiyo mapema asubuhi, wanawake walikwenda katika kaburi la Yesu kumpaka manukato. Aliyefika akiwa wa kwanza alikuwa ni Maria magdala, huyo ni mmoja wa mtu aliyekuwa amemsindikiza Yesu hadi Galilaya , na kujikita katika huduma ya Kanisa lililokuwa linaanza.

Katika kujikita kwenye safari hiyo , Baba Mtakatifu anaeleza ,kwamba, hiyo inaangaza imani ya wanawake wangi kwa dhati wenye ibada kubwa  kwa miaka mingi ya kwenda katika makaburi, kwa ajili ya kukumbuka wale ambao hawapo tena. Kwasababu  mahusiano ya dhati siyo kwamba yamekatika kutokana na kifo,bali kuna anayeendelea kupenda hata kama yule aliyekuwa anapendwa amekwisha tangulia kwenda mbinguni daima. (Yh20,1-2.11-18) inaeleza wazi na haraka ya kwamba Magdalena hakuwa mwanamke wa kuchangamka kirahisi, kwasababu baada ya kuona kaburi wazi , alirudi nyuma akiwa amekata tamaa na kwenda kwa haraka kwa mitume mahali walipokuwa wamejificha kuwaelezea jinsi Jiwe lilivyo vilingishwa kutoka kaburini:  mawazo yake ya kwanza yalikuwa kwamba kuna mmojawapo aliyekuwenda kuiba mwili wa Yesu. Kwa namna hiyo tangazo la kwanza la Maria Magdalena halikuwa la ufufuko , bali la wizi wa mtu asiyejulikana wakati watu wamelala usiku huko Yerusalem.

Baadaye Injili zinaeleza safari yake ya Pili ya Magdalena ya kwenda katika kaburi la Yesu: kwa mara hii lakini kwa mwendo taratibu , na mzito, Baba Mtakatifu anasema alikuwa na kichwa kigumu kwani alikwenda na kurudi, kwa maana hakukata tamaa kwasababu  hakuamini. Hivyo  Maria anateseka mara mbili: kwanza kwa ajili ya kifo cha Yesu na pili kwa ajili ya kutopata maelezo ya kupotea kwa mwili wake.
Wakati anakaribia Kaburi akiwa amejaa machozi, Mungu anamshangaza kwa njia isiyotegenewa. Mwinjili Yohane anabainisha jinsi gani macho yake yalikuwa mazito na kufumba: hakuwa na utambuzi wa malaika wawili walikuwa hapo wakiuliza na hata mwanaume aliyekuwa nyuma ya mabega yake, maana alimfikiria ni mtunza bustani hiyo. Kwa bahati anatambua tukio hili la kubadilisha historia yabinadamu mara tu anapomwita kwa jina Maria!

Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kwamba ni jinsi gani ilivyo nzuri kuona matokeo ya mfufuka, kwani kwa mujibu wa Injili zote wanasema, matokeo haya  yalijitokeza kwa namna hiyo binafsi!. Kwa maana hiyo kuna mtu anaye tufahamu, anayetazama mateso yetu na kukata tamaa kwetu, anayeamka akiwa wa kwanza kwa ajili yetu na kutuita kwa jina. Hiyo ndiyo sheria tunayokutana nayo iliyowekwa kama muhuri katoka katika kurasa za Injili. Wapo watu wengi karibu na Yesu wanaomzunguka, wapo watu wengu wanao mtafuta Mungu, lakini jambo la kushangaza ni kwamba kabla ya wao kumtafuta , hawali ya yote ni Mungu mwenyewe  anayehangaikia maisha yetu, anataka kutatua matatizo. Kwa kufanya hivyo yeye anaita kwa majina kwasababu anatambua sura zetu binafsi za kila mmoja wetu. Baba Mtakatifu Francisko anaongeza; kila binadamu ni historia ya upendo ambao Mungu anaandika katika ardhi hii.

Kila mmoja wetu ni historia ya upendo wa Mungu, na kila mmoja Mungu anamwita kwa jina lake binafsi kwasababu  anatutazama, anatusubiri, anatusamahe, na kuwa na uvumilivu nasi. Ni kweli au hapana? Baba Mtakatifu ameuliza, nakusema  kila mmoja anao uzoefu  huo…
Yesu alimwita Maria! Baba Mtakatifu anaeleza: Hapa ndipo kuna mapinduzi ya maisha yake, mapinduzi yaliyopelekea mabadiliko ya maisha ya kila binadamu ambayo yalianzia  kwa jina ambalo lilisikika katika bustani ya Kaburi wazi. Injili zote zinaelezea juu ya furaha ya Maria aliyoipata :Anatoa mfano; Ufufuko wa Yesu siyo furaha inayotolewa  kama kifaa kihesabucho  matone tone, bali ni kama  maporomoko ya maji kwa maisha yote.  Baba Mtakatifu anasema, maisha ya Mkristo hayakusukwa na furaha laini, bali ni kama mawimbi baharini yapigayo kila sehemu na kufagia kila kitu. Jaribuni kufikiria hata nyinyi wakati huo huo, iwapo kuna mzigo mzito, tunayobeba  kila mmoja ndani ya moyo na kukata tamaa , unasikia kwamba yupo Mungu karibu nasi, anatuita kwa jina akisema hamka na nyamaza  kulia, kwasababu nimekuja kukupatia uhuru! ni jambo zuri hilo!

Yesu siyo kwamba anafurahia kuja katika ulimwengu huu na kuvumilia kifo, huzuni , chuki , uharibifu wa maadili ya watu… Mungu wetu siyo mzembe, Mungu wetu, kama mnaniruhusu kutoa neno, Baba Mtakatifu Francisko ameongeza ; Mungu wetu ni mwotaji ndoto, yeye anaota mabadiliko ya ulimwengu huu, kwani ameukamilisha kwa njia ya fumbo la Pasaka. Maria alipendelea kumkumbatia Bwana wake, lakini  Yesu sasa yukotayari na mwelekeo wa Baba yake wa mbinguni, ambapo yeye alimtuma kwenda kutoa habari kwa ndugu zake. Kwa  maana hiyo mwanamke huyo ambaye kabla ya kukutana na Yesu alikuwa amezingirwa na maovu mengi , sasa amekuwa mtume wa matumanii mapya na makubwa zaidi. Kwa njia ya maombezi yake atusaidie kuishi uzoefu huu: katika saa ya kilio na kutelekezwa, kusikia Yesu Mfufuka anatuita kwa jina, na kwa mioyo uliyojaa furaha ya kweli kukimbia kutangaza kuwa nimeona Bwana. Nimebadili maisha kwasababu nimemwona Bwana leo , mimi ni tofauti kwasababu Bwana amebadili maisha yangu. Na hiyo ndiyo nguvu yetu na matumaini yetu.

Asante!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.