Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican: tuhuma za fedha chafu zimepungua

Imetolewa taarifa kwasababu ya kukamilika mpango wa kutoa ripoti iliyoanzishwa mwaka 2013 ya Bank ya Vatican IOR - EPA

17/05/2017 17:04

Mamlaka ya Habari za Kifedha Vatican inaridhishwa na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha fedha cha Mwaka 2016, matunda ya ushirikiano wa kimataifa katika mchakato wa kupatamba na utakatishaji wa fedha haramu duniani! chombo  ambacho husimamia sekta  ya Fedha ambayo  katika taarifa ya mwaka 2016 mchakato wa tuhuma za kifedha umeonesha kupungua ikilinganishwa na mwaka 2015 japokuwa kiwango kilikuwa cha juu zaidi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Mwaka jana kulikuwa na  tuhuma 207 za shughuli za fedha kati ya 544 katika mwaka 2015.Ni ripoti ya AIF ambayo ni Mamlaka ya habari kuhusu fedha za Vatican,  katika taarifa yake iliyotolewa mapema wiki hii. Mwaka 2016, taarifa  22 zinazohusu shughuli za uendeshaji wa mchakato wa uchunguzi kwa upande wa mamlaka ya mahakama ya Vatican. Mkurugenzi wa AIF Tommas di Ruzza anasema; mfumo wa kutoa taarifa unaendelea kuleta mafanikio na ufanisi mkubwa.

Kwa upande wa Rais wa AIF, René Brülhart, anasema, katika mchakato ulio mbele yao wanaukabili kwa  utaratibu na hatua kwa hatua unazidi kukomaa. Aidha anasema, kwa kuchambua utaratibu mzima kwa namna ya pekee kuanzia  miaka ya mwisho mitatu - minne kuhusisha mchakato wa kifedha wa Benk ya Vatican , kumekuwa na upungufu kulinganisha na jinsi walivyo ukuta, anaongeza akisema,  kiukweli haikuwa jambo la kushtukiza. Kwa njia hiyo anadhani siyo matokeo ya kimantiki katika hatua waliyopitia kwa miaka ya karibuni, bali anapenda kusema kwamba ni jambo ambalo linapaswa kuwa la kawaida yaani wa kuwa mfumo wa kutoa taarifa kama hiyo.

Hii Taarifa imetolewa kwasababu umekamilika mpango wa kutoa ripoti iliyoanzishwa tangu mwaka 2013 ya Bank ya Vatican IOR. Na taarifa inaonesha kwamba kuna ongezeko sasa  la ushirikiano wa kimataifa kati ya AIF  na umoja wa vitengo  vya kifedha kutoka matukio 81 mwaka 2013 hadi kufikia  837 mwaka 2016. Mwaka  jana Desemba 31 yalikuwa mashirika 32 ya nchi nje yanayoshirikiana  na AIF. Aidha michakato minne imesitishwa kwa shughuli za uendeshaji , wakati huo  kuzuia akaunti au rasilimali za uchumi. Lakini katika hali zote mbili thamani ya jumla ni pungufu  ukilinganishwa na mwaka 2015. Kuna ongezeko kidogo kutokana na  taarifa za usafirishaji wa wa fedha za ndani na nje zinazo ingia na kutoka.

Katika uhusiano na MONEYVAL, Kamati ya Wataalamu wa Baraza la Ulaya kwa ajili ya tathmini hatua dhidi ya fedha chafu, René Brülhart amekuwa wazi kwamba ukisoma kwa makini MONEYVAL, Vatican imeweza kutambua mikopo kwa maendeleo makubwa katika sekta hiyo. Mwaka 2016, Mkuu wa utawala  ameondoa orodha ya watu 29 ambao walikuwa wanatishia amani na usalama wa kimataifa.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

17/05/2017 17:04