2017-05-16 16:43:00

Maaskofu nchini Peru: Kanisa kuwakaribia watu wanaoteseka


Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu 15 Mei 2017 alikutana na kuzungumza na Maaskofu kutoka nchi ya Peru ambao wamekuja Vatican kwenye Ziara ya kichungaji. Askofu Mkuu wa Ayacucho na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Peru ; Salvador Piñeiro García-Calderón amehojiana na mwandishi wa Radio Vatican kuhusu Kanisa la Peru linavyojikita katika utume kutokana na mantiki za kiuchumi na matatizo ya kijamii. Askofu Mkuu anaelezea kwamba wanapitia kipindi kigumu na wasiwasi kutokana na madaraka ya viongozi wa umma, majanga ya kiasiali ya mvua ya El Nino  iliyowakumba Kaskazini ya nchi. Watu wamekata tamaa  kwasababu wanateseka, lakini wakiwa na imani kwa Yesu na wanapenda sana Kanisa, ambapo wanazidi kumwomba  Baba Mtakatifu awatie moyo  ili waimarike  katika imani.

Ili kuweza kukabiliana na matatizo ya kijamii , kama Kanisa kwa  mantiki hii, Askofu Mkuu anasema, Kanisa linaaminika sana japokuwa na  matatizo, udhaifu na makosa ya kanisa. Na kwa hali halisi kuna kipeo cha uchumi kikubwa pia kipeo cha kimaadili na kama Kanisa wasiwasi mkubwa  ni  juu ya familia. Katika umbu  lake, kipeo daima kinazidi kuwa kikubwa kwani wanawake wengi wameachwa peke yao . Pia wasiwasi  wa Kanisa ni juu ya sekta za kisiasa ambazo wanapendelea kupitisha badhi ya sheria fulani ambazo kwa kiasi fulani ni aina ya ubaguzi wa Kanisa ambalo daima limekuwa likijieleza lenyewe katika misingi ya familia na elimu. Anaongeza ki ukweli Kanisa lina makubaliaao muhimu na Serikali,kwasababu Katiba inatambua kuwa taifa limekua na kuongezeka kutokana na imani ya Kanisa na ndiyo sababu mada ya familia na elimu ni lazima viwepo katika mazungumzo na mawasiliano.

Kutokana na mapambano ya nguvu ya Kanisa kwa njia ya vyama katoliki katika utetezi na ulinzi wa maisha na familia Askofu mkuu anaelezea kwamba, kwa ngazi ya kisiasa kwa bahati nzuri sheria zimepitishwa lakini wapo wanaopenda kufanya mchezo wa upìnzani, hawakosekana vikundi vinne, vitano vinavyo tetea itikadi za mawazo ya ndoa ya jinsia moja. Lakini ni sehemu ndogo inayo piga kelele,  kwa bahati nzuri kuna sauti ya Kanisa kukumbusha nini maana ya familia na thamani ya elimu. Kuna kipindi kigumu lakini kuna mawasiliano kati ya Baraza la Maaskofu na Serikali. Siyo tu kuendelea kufanya majadiliano, bali lazima kuwafanya watumbue kwamba Kanisa ina historia yake na sauti hiyo lazima kutambuliwa.

Kuhusiana na uchumi kijamii nchini Peru, Askofu mkuu anasema zipo mada mbili zenye kuleta wasiwasi sana ambazo zimeongezeka kutokana na majanga ya asili huko Kaskazini mwa nchi. Pamoja na kuwa na mshikamano kutoka kwa wadahu mbalimbali na misaada ya kitaifa na kimataifa, bado umaskini unakithiri. Majanga ya asili yanayozidi kutokea , ni kama vile Baba Mtakatifu Francisko alikuwa ametabiri katika waraka wake wa sifa kwa Bwana, ya kwamba tunapaswa kulinda dunia hii, pia kuwa na mshikamano na maskini.Na mada ya pili ni ile ya msitu wa Amazon; ni zaidi ya asilimia 60 ya wilaya na mikoa  iko katika msitu huu na hiyo husababisha umbali mkubwa  na rasilimali chache kwasababu ya idadi ya watu kuishi mbali sana kati yao na kutengwa. Kusema ukweli kuna ndugu maaskofu nane wenye maeneo makubwa sana lakini wenye idadi ya watu wachache, wakiwa na changamoto kubwa,hivyo wanahitaji msaada ili kukuza ukarimu wa uwepo wao katika maeneo hayo.

Pamoja na uwepo wa wakatoliki wengi katika nchi yao, kwa asilimia 88% ya watu bado kuna ongezeko ya haraka ya makundi mengine yatokanayo na ukristo, je hayo yanasabaishwa na nini? Askofu  Mkuu anasema hiyo ni kutokana na kwamba mahali ambapo hakuna Kanisa Katoliki , makundi mengine huzuka , maana hao wanakuja na ulaghai kwamba, wanao upendo mkubwa na baadaye kidogo, yanaanza malumbano kati ya madaraka ya Kanisa na makabila dhidi ya picha takatifu. Kwa njia hiyo Kanisa linatafuta namna ya kufanya mazungumzo ya kiekumene , ili kuwakaribia kwa urafiki. Pamoja na hayo siku chache zilizo pita kumekuwa na tabia mbaya zilitokana na mitandao ya kijamii dhidi ya makanisa na wachungaji wake, Askofu mkuu anasema lazima kufanya kazi ili kuweza kuwa wachungaji wema wenye roho kama ya Kristo Yesu mbele ya matukio ya kijamii.

Kuhusiana na miito ya Kanisa Katoliki nchini Peru, amesema Jumapili ya siku ya mchungaji mwema yeye alisema kwamba walikuwa wachache, maana hata kama Kanisa linafanya kazi kubwa mashuleni na katika familia , mada ya miito ina ututa wake. Ni lazima kuomba Bwana aoneshe eneo na sehemu gani ya kufanya kwa ajili ya miito. Maana inawezekana leo hii vijana walivyo wadhaif wanaitwa sehemu nyingine hata kama siyo njia zao, na pia ukosefu wa familia inayo wasukuma katika mang’amuzi halisi, kwa namna moja au nyingine ni kipindi kugumu japokuwa yeye binafsi anayo matumaini ya kwamba wataebdelea kutenda wajibu wao kwa ajili ya miito ya Kanisa.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.