2017-05-15 13:26:00

Semina ya wahudumu wa haki na amani kijimbo nchini Ethiopia


Kumweka  Kristo katikati katika utume na daima kuendelea kuomba hekima kwa Mungu.Ndiyo matashi mema ya kutiaa moyo kwenye semina ya wahudumu kichungaji wa Kijimbo katika  kitengo cha Baraza la  Haki na Amani nchini Ethiopia kwenye semina ya hivi karibuni. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Ethiopia ambapo ilifanyika huko Adds Abeba.
Katika semina naye Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Padre Hagos Haysh aliwaalika waratibu  wa kijimbo kuwa watendaji katika huduma ya amani na mapatano ya Kanisa Katoliki, katika kujikita kwenye huduma hiyo kama wawakili wa amani na mapatano, daima wanapaswa kuwa wajasiri na kutafuta hekima kwa njia ya mwanga wa Kristo,pia lazima kusali na kuimarisha imani ya kila mmoja wao.

Hii ni kwa sababu amesema,kwa njia ya hekima ya Mungu wanawezesha kuwa na utambuzi wa hali halisi ya jamii kwa nyakati za sasa,kwa kutoa huduma kila siku na hata baadaye kwa waamini wote. Huduma kama hiyo ndiyo inayo tofautisha kati ya wafanyakazi wa sekta nyingine za kijamii. Kwa namna hiyo amesisitiza umuhimu wa kutetea walio wanyonge na wasio kuwa na mtetezi. Padre Hagos amesema, anayetoa huduma kwa ajili ya amani, mapatano na haki ni lazima kila siku awe na utambuzi wa matukio yanayojitokeza katika nchi yake na mahali anapoishi ili kuweza kujitoa kwa ajili ya huduma ya dhati kuanzia mambo halisi na sahih yanayozunguka nchi.

Ni zaidi ya miaka 20 Kitengo cha Haki na Amani kimejitika zaidi katika hali halisi ya nchi na matokeo muhimu yameonekana ykutokana na kuendelea mbele ndani ya Baraza najadiliano ya kidini  la kitaifa katika ujenzi wa amani. Katika ya mada zilizoguswa wakati wa Semina hiyo ni pamoja na changamoto za sasa wanazokabiliana  vijana na pia kuanguka na kudhoofika kwa maadili katika jamii.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.