2017-05-12 16:17:00

Wito wa Maaskofu Marekani katika Seneti juu ya haki ya maisha na afya


Maaskofu wa Marekani wametoa wito  katika Seneti ya  Marekani tarehe 11 Aprili 2017 ya kwamba wasisahau walio wathaifu. Seneti inapaswa kuchukua maamuzi wa mwisho kuhusu Bima ya afya  (American Health Care Act) ambayo inapatikana katika  kifungu cha 1628. Huo ni mswada wa sheria unaopaswa kutafsiriwa kwa upya juu ya mfumo wa afya. Hivi karibuni  baada ya kupitishwa mswada huo  wawakilishi wa Bunge 217  wametoa ndiyo dhidi ya 213 wa hapana. Asofu Frank. Dewane wa Jimbo la Venice na Rais wa Tume ya Haki na Amani na maendeleo ya Binadamu katika Baraza la Maaskofu wa Marekani ametuma ujumbe katika Senate  ili yafanyike wamadiliko kadhaa katika mkutano wao. Anasema Licha ya jitihada za kubuni bado masuala makubwa hasi yapo hasa kwa upande wa marekebisho ya Matibabu katika mpango wa afya wa serikali ambayo inatoa misaada ya watu na familia zenye kipato kidogo, na hiyo  inatishia bima ya afya kwa mamilioni ya watu.

Kwa mujibu wa Askofu Dewane, ni kukatisha tamaa kwa kina kwani haikusikika kilio cha watu wengi wathirika. Bima ya Afya inatoa ulinzi muhimu wa maisha na mfumo wao wa afya unahitaji ulinzi huo. Hata hivyo anaongeza; watu wanaoishi katika  mazingira magumu ni lazima wasiachwe katika umaskini na  hali mbaya zaidi. Mageuzi ya Bima ya Afya ambayo Rais Trump anataka kufanya badala ya "Obamacare", yanatazamia kuwanzishwa bima binafsi ya afya yenye kuwa na asilimia 30 ya ziada kwa wale wenye kipato cha chini, wakati huo kuna mikopo mingine ya kodi ya kuongeza na michango ya usalama wa bima ya afya.

Kwa njia hiyo katika miezi ya hivi karibuni Askofu Dewane alionya wanasiasa dhidi ya hatari itakayojitokeza, pamoja na mageuzi mapya ya  Pro- life, wagonjwa na wazee wanaweza kulipa zaidi kwa ajili ya afya zao. Tangu  kuanza mjadala wa Affordable Care Act”,ulio anzishwa na Rais Obama, Maaskofu wamerudia kuomba Seneti  kuheshimu misingi ya kanuni ya Sheria katika mageuzi ya afya.  Miongoni mwa maombi ya maaskofu ni kwamba watu wote waweze kupata huduma ya kufaa ya afya na pia kuheshimu maisha na uhuru wa ulinzi wa dhamiri.
Kwa njia hiyo Askofu Dewane ametoa wito katika wajumbe wa Seneti na kusisitiza juu ya mabadiliko hayo kwamba iwapo Seneti itazingatia bima ya afya itabidi kuchuka hatua za kuondoa mapendekezo yenye kuleta madhara. "Afya yetu" amesema, "lazima kuheshimu  awamu zote za Maisha na adhi ya binadamu".

Sr Angela rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.