2017-05-11 09:33:00

Wafungwa wa Kipalestina huko Israeli kufanya mgomo wa kula chakula!


Tangu tarehe 17 Aprili 2017 Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye magereza ya utawala wa Israeli walianzisha mgomo usio na muda maalum wa kususia kula chakula wakilalamikia vitendo vya ukatili na vya kinyama pamoja na hali mbaya ya huduma na mazingira inayowakabili katika jela hizo. Hatua za Mgomo huo unaongozwa na Marwan Al-Barghuthi kwa kaulimbiu ya "Uhuru na Heshima". huyo ni kiongozi wa Kipalestina  ambaye kwa miaka 15 yuko jela kwa ajili ya kudai uhuru na haki. Kwa mujibu wa Idara ya Magereza ya Israeli  ni wafungwa 1800 kati ya 6,500 ambao kwa wiki hizi wamesusia chakula.

Gazeti la Sir limesambaza habari hivi karibuni kutoka Tume Katoliki ya maeneo Matakatifu inayowataka viongozi wa Israeli wasikilize kilio cha wafungwa na kuheshimu adhi ya ubinadamu wao, kwa kufungua njia mpya  kuelekea ujenzi wa amani. Ujumbe huo unasema wafungwa wanalalamikia  ukosefu wa kuheshimiwa haki za na adhi  za kibinadamu kama inavyotambuliwa katika haki za Kimataifa na mkataba wa Gineva. Ujumbe huo unawataka pia wakristo wote kushiriki kikamilifu katika  utume huo  kwa ajili ya uhuru wa kila binadamu na kuunda jamii ya kibinadamu yenye usawa kwa wote, wawe  Wasraeli au Wapalestina.

Halikadhalika ujumbe huo unasema; juhudi za wakatoliki mahalia zinaongezeka kwa ajili ya wafungwa huko Israeli. Juhudi hizo ni kutoka na utume wa kichugaji wa Kanisa wenyewe  kwa ajiili ya wafungwa wote wa Kipatriaki mjiniYerusalem na zaidi ya miaka  20 ni utume ulioanzishwa kwa matashi ya Patriaki mstaafu Michel Sabba. Padre David Neuhaus muhusika  mkuu, mwandaji wa timu ya watu 10 wa Tume Katoliki ya Huduma kwa wafungwa Magerezani, miongoni mwao wakiwemo mapadre , watawa na walei kwa sasa wanasaidia mamia ya wafungwa wakristo, miongoni mwao wakiwemo wanawake wa kiorthodox. Padre David anabainisha kwamba hao siyo tu  wafungwa wa kisiasa bali kuna hata wafungwa wengine zaidi walio hukumiwa kwa ualifu wa makosa ya kawaida.

Ikumbukwe kwa siku hizi kumekuwa na ongezeko kubwa la kungwa mkono mgomo huo karibu kila kona ya nchi , hata  Mamlaka ya Palestina, mashirika yasiyo ya serikali ya Palestina pamoja na vilabu vya muungano wa jela Palestina zimefahamisha ya kuwa mgomo huo ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea ndani ya mwaka. Maandamano ya kuunga mkono yameonekana katika nchi za  Arabia, London, Marekani, na hata Afrika ya Kusini  wote wakiwa wanataka mamlaka kuwapa huduma ya afya na njia ya mawasiliano na familia zao.

Licha kuungwa mkono watu mbalimbali hata Askofu Mkuu  wa Kipatriaki wa Yerusalem  wa Kanisa Katoliki la Kigiriki na Melkit ,Gregory Lahan wa III, hivi karibuni naye  aliamua kususia kula chakula ili kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wake kwa Wapalestina hao waliosusia kula katika magereza ya utawala wa wa Israeli. Askofu Mkuu Gregory Laham wa III,ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki  la kigiriki katika maeneo ya Mashariki yote, Alexandria na Quds mwenye umri wa miaka 83 pia amechukua hatua hiyo kukosoa ukandamizaji wanaofanyiwa wafungwa wa Palestina katika magereza ya kutisha ya utawala wa Israeli.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.