Matendo ya kigaidi ya Kikundi cha Boko Haram tangu mwaka 2014 kimeshambulia zaidi
watoto. Watoto wengi wanatumiwa kama mashumbulizi ya kujitoa muhanga.Utafiti uliofanywa
na Ofisi ya Sekretarieti Kuu ya Umoja wa Mataifa juu ya watoto na migogoro ya silaha
kwa mwaka 2013 -2016 , inaonesha watoto wanazidi kuteseka kiukatili katika mikono
ya magaidi wa Boko Haram katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria.
Taarifa inasema; kwa miaka mitatu wameua watoto zaidi ya 4,000 na 1,650 kufundishwa
kushika silaha au kuingizwa katika kundi lao. Aidha mashambulizi dhidi ya jamii na
mapigano dhidi ya vyombo vya usalama vimeacha ulemavu wa viuongo kwa watoto 7,300.
Katika ripoti ya Umoja wa Mataifa pia inaonekana wazi kwamba kulipuka kwa mabomu
ya kuua ndiyo sababu ya pili ya vifo miongoni mwa watoto.
Baadhi ya shuhuda mbalimbali zilizotolea na watoto wadogo waliokombolewa, wanasema,
wengi wao wanatekwa lakini wengine ni kwasababu ya uchumi au shinikizo la familia.
Hiyo imetokana na wakati mwingine wazazi wenyewe hutoa watoto wao ili wapate ulinzi
au faida kiuchumi.
Mashule ndiyo lengo kuu la mashambulizi ya kigaidi, kwani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,
inaonesha kwamba ni takribani ya mashule 1,500 yaliyo haribiwa kwa mwaka 2014 na rekodi
za waathrika ni 1280 katika ya wanafunzi na walimu wao. Tangu mwaka 2014 ni zaidi
ya 4000 ya watoto ambao wameteswa,au kulazimishwa kuolewa na pia kubadilisha dini
kuwa waislam.
Aidha,kundi la wataalam wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa wamekaribisha
tarehe 9 Aprili 2017 kuachiwa huru kwa wasichana 82 wa Chibok waliokuwa mikononi
mwa Boko Haram, na kutoa wito kwa serikali ya Nigeria na jamii ya kimataifa zichukue
hatua zote stahiki kuhakikisha kuwa wote waliokamatwa na Boko Haram wanaachiwa huru.
Wataalam hao ni Maud de Boer-Buquicchio,mhusika na uuzaji wa watoto, Urmila Bhoola
muhusika na utumwa, na Dainius Pûras muhusika na haki ya kuwa na afya bora. Halikadhali
wanatoa wito ili wasichana walioachiwa huru wapewe msaada utakaowawezesha kujiunga
tena na jamii zao na kuishi maisha ya kawaida, huku haki zao zikiheshimiwa kikamilifu.Hiyo
ni pia inajieleza wasiwasi mkubwa uliopo kuhusu hatma ya wasichana zaidi ya 100 ambao
bado wanashikiliwa na Boko Haram, pamoja na familia za wasichana hao. Ikumbkwe tarehe
14 Aprili 2014 kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kiliivamia shule ya Chibok Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria na kuwateka nyara wanafunzi 276.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |