2017-05-09 14:25:00

Shetani yupo ulimwenguni anazunguka japokuwa amefungwa mnyororo!


Jumatatu 8 Aprili 2017 katika Chuo Kikuu cha cha Kipapa Regina Apostolorum, Roma Italia imefunguliwa kozi ya XII ya kitume, ikiwa na washiriki zaidi ya 240 kutoka zaidi ya nchi 40 duniani, yenye kauli mbiu "Kupunga mapepo na Maombi ya Uponyaji".
Ni muhimu kujiandaa kwa kina ili kuweza kuepuka mambo yanayotokana na akili na mazoezi ambayo hayaendani na sheria za Kanisa. Ameyasema Bwana Giuseppe Ferrari, Katibu wa Taifa wa Kikundi cha Utafiti na mafundisho ya dini Jamii huko Bologna nchini Italia, katika utangulizi ya kufungua Kozi ya kupunga pepo wabaya na maombi ya uponyaji. Kozi hiyo imeandaliwa na Chuo kikuu cha Kipapa cha Rigina Apostolorum kwa ushirikiano wa Kikundi cha utafiti  na pia chama cha Kimataifa cha kupunga Pepo (Aie). Katika kozi hiyo wanashiriki zaidi ya watu 240 wakiwemo mapadre na walei kutoka zaidi ya nchi 40 duniani.

Naye Padre José Enrique Oyarzún Msaidizi wa  Gombera wa Chuo hicho cha kipapa katika hotuba yake amesema  Ibada na mazoea ya  kuabudu mashetani imezidi kuenea hasa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambapo uwashirikisha idadi kubwa ya watu wenye umri mdogo hasa vijana na hivyo shetani yupo hata kama wengi hawakubaliani .Akitoa hotuba yake Kardinali Angelo Amato Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu katika Kozi hiyo ya XII kuhusu kupunga mapepo  na maombi ya uponyaji amesema,  hata watu wengi kwa upande wa Fatima wamekuwa na vishawishi  katika akili na moyo kwa karne zilizopita. Anayasema hayo kutokana na ni siku chache kabla ya Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko huko Fatima kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 100 tangu Mama Maria awatokee watoto watatu.

Kardinali Amato anathibitisha kuwa hakuna siri yoyote ya nne ya Fatima inayosadikika na watu wengi kwamba imefichika, kwamba kuna maafa ya kutisha kwa ajili ya Kanisa. Anasisitiza  hakuna siri zaidi kwani kila kitu kuhusiana na mambo ya Fatima kimekuwa wazi kwa umma; iwe kwa upande wa sista Lucia  au binamu zake wawili Francisko na Jasinta Mart watakao tangazwa watakatifu na Baba Mtakatifu.
Kwa upande wa Sista Lucia, bado wako kwenye mchakato wa kutangazwa mwenye heri.  Kwa kurudi kwenye kumbukumbu ya mashambulizi dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 13 Mei 1981 ambapo alipigwa risasi katika viwanja vya Mtakatifu Petro, Kardinali amebainisha kuwa Papa Wojtyla alishtushwa na tukio la Fatima wakati muuaji huyo kitaalam hakutubu kuhusiana na tukio hilo la kutisha.Kardinali Amato anabainisha kuwa  kwa Upande wa Mtakatifu Yohane Paulo II,  lakini ilikuwa ni  kuzaliwa upya kwa mara ya pili.

Mtakatifu Yohane Paulo II alianzisha kipindi cha Maria ambacho kikwa  ndiyo mwongozo wa utume wa khalifa wa Petro, kwa maana ya kuweka utume wake chini ya mwanga wa Totus Tuus (majitoleo ya Bikira Maria ) Kardinali Amato anasema hiyo inaelezea mageuzi ya uhakika kuhusu utume wake aliofanya. Lakini pamoja na majaribu hayo kwa upande wa Yohane Paulo alishinda mwovu  na kuonesha kuwa shetani ni wa kushindwa tu.Aidha amesema Mateso ya Kanisa ambayo yameonekana kwa karne na kuendelea kuoneshwa bayana kwamba bado  upo mwovu. Lakini pia anabainisha kuwa, siyo rahisi kuelezea juu ya shetani bali  inahitaji ujasiri. Anaongeza, ni rahisi kujadili juu ya mambo mazuri tu lakini wakati huo huo sote tunaishi katika kipindi cha majaribu ya ubaya  zaidi ya awali. Hiyo inatokana na kuendelea kushuhuhudia utamaduni unaopinga uwepo wa shetani,japokuwa tunaendelea kushuhudia kuenea kwa makampuni yanayofanya mazoezi ya kishetani. Sababu kubwa anasema, inatokana na mtu anapoikataa Injili  ni kukaribisha maovu.

Aidha Askofu Erio Castellucci wa Jimbo la Modena na Nonantola Italia katika hotuba yake amesema, siyo lazima kujadili uwepo wa kazi ya shetani kwa maana yupo. Hiyo ni kutokana na uhusiano kati ya aina za kiakili na umilki, magonjwa yanayokuja,wakati mwingine mipaka yake siyo nadhifu. Kwa hivyo ni Yeye anashauri muhimu kuwapo mtoa mapepo. Askofu Castelluci anasisitiza, ni muhimu katika makanisa mahalia uwezekano wa maalumu wa mtu mmoja au zaidi wa huduma ya kutoa pepo na uponyaji.  
Iwapo katika Jimbo hakuna uwezekano wa kutoa huduma hiyo,lakini  ikumbukwe kwamba utume ni lazima na haupaswi kukoma, kwasabau ni utume wa Yesu alio wakabidhi mitume wake katika Kanisa.

Kwa upande wa Askofu Castellucci anabainisha pia kuwa,kazi ya mapepo ni kubwa lakini haina nguvu,kwasabau shetani kweli ni simba lakini aliyefungwa mnyororo. Mafundisho ya TaaliMungu kwa upande mwingine yanashindwa kujenga mantiki ya moja kwa moja kutokana na matendo ya kiajabu ya shetani kujificha kichini chini. Hivyo Askofu Castellucci anabainisha akisema siyo mara kwa mara mawindo ya shetani utenda maovu, inawezakana wakati mwingine kutokea hata kwa watu watakatifu hata kwa watoto wachanga.  Amemalizia na maneno ya Baba Mtakatifu Francisko yasemayo kwamba; Kanisa ni kambi ya hospitali daima; na hivyo ni lazima uwepo wa  makuhani wa kutoa mapepo na maombi ya uponyaji.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili

 








All the contents on this site are copyrighted ©.