2017-05-09 14:05:00

Maaskofu wa Msumbiji watoa wito wa kulinda ardhi nyumba ya wote!


Hivi Karibuni Baraza la Maaskofu wa Msubiji wameandika hati ya kitume kwa waaamini wakristo na wenye mapenzi kuhusu utetezi wa mazingira. Katika hati hiyo yenye kauli mbiu “katika wazawa wako  nitawapatia  nchi hii (Mw 17,7), maaskofu wa Msubiji wanachota tafakari kutoka katika Waraka wake wa kitume wa Baba Mtakatifu Francisko  kuhusu utunzaji bora wa mazingira, “Laudato si” yaani “Sifa iwe kwako. Maaskofu wanaandji wakisisitiza juu ya kutoa kipaumbele cha ardhi ambayo ni zana katika uzalishaji mali,  na kwamba matumizi yake ni haki msingi ya kutekelezwa na watu wote wa Msubiji.
Katika ujumbe huo kwa bahati mbaya Baraza la Maskofu wanaonesha kuwa, tangu mwaka 2000 hadi 2013 Hekta milioni 53 za ardhi  ya Afrika zimeuzwa au ziko chini ya usimamizi wa kigeni ,kwasababu Serikali za  nchi zenye viwanda wanatafuta katika bara la Afrika kupata  ufumbuzi wa migogoro yao ya nishati na chakula duniani , bila ulazima wa kujaribu kusaidia matatizo ya waafrika. Kwa njia hiyo wito wa Maaskofu unasema watafute mifano ya ndani ya maendeleo ambayo ni ya kweli, ya  dhati na haki.

Suala jingine muhimu katika ujumbe  wa Maaskofu wa Msumbiji ni kwa upande wa utetezi wa haki za ardhi: wanasema kunyimwa haki ki ukweli inalazimisha jamii mahalia kuacha ardhi yao na kusababisha uwekezaji wa watu binafsi ambapo wao huaribu mfumo wa kilimo kwa familia nyingi. Wanatoa mifano madhubuti kwa kubainisha kwamba, kuna baadhi ya mikoa ambayo tayari imeshaingia kwenye migogoro inayosababishwa   na ardhi kutokana na mipango mikubwa  ya makampuni makubwa.Unaendelea kwamba sheria ya serikali juu ya usimamizi wa ardhi inatazama maendeleo pamoja na usawa kati ya wawekezaji na jamii mahalia, katika mchakato inaogawanya majukumu na faida kati ya pande zote mbili. Lakini wanabainisha kuwa, tatizo  ni kutokutomia sheria hiyo ipaswavyo kwa wale wanaopaswa kufanya hivyo,kwa njia hiyo Maaskofu wanaiita  “kutojali”  na ndiyo maana inaleta   kubaguliwa na kuongezeka umaskini wa jamii.

Maaskofu wa msumbiji kwa njia hiyo wananyoshea  kidole dhidi ya uchumi wa kibepari unaozidi. Wanasema Hiyo ni aina ya uchumi inayoongoza kwenye matumizi mabaya, katika uzalishaji  mkubwa  na haraka wa rasilimali  za asili, wanarudia kusema kwamba, ni uchumi wa kifo, kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko. Kinyume na hali hiyo maaskofu wanabainisha umuhimu wa kuwa na ardhi ya pamoja , kwasababu ndiyo dhamana halisi na hakika kwa ajili ya maisha endelevu ya familia na jamii nzima. Hiyo pia ni kwasababu wanaandika, karibu asilimia 70% ya watu wanaisha katika mazingira ya vijijini wakiwasiliana na asili. Sehemu nyingine muhimu katika ujumbe huo maaskofu wanasisitiza  ukosefu wa ikolojia  muhimu na mfano wa maendeleo yenye kuheshimu kila mtu, watu hasa wadhaifu, ukosefu wa  maji ya kunywa, uharibifu wa misitu ambayo inahusisha mabadiliko ya hali ya hewa. Na hiyo pia inasababishwa na ukosefu wa  elimu  kwa maskini walio wengi , kwani hawana taarifa zaidi kuhusu haki zao, hawana uwezo kiuchumi ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao, aidha wanapuuzia uwezo wao wa kuhamasisha na hawana zana na usimamaizi wa ulinzi.

Pamoja na hayo Maaskofu wa Msumbiji wanasisitiza kuwa Kanisa daima limejikita kutetea haki ya mali binafsi  ili iweze kutekelezwa kwa faida ya watu wote na siyo kutambuliwa kuwa kitu kisichogusika. Ardhi imepewa  kila mtu na matunda yake ni kwa manufaa ya wote ikiwa pia ni kanuni ya wote.
Hati ya maaskofu  inahitimisha na mfululizo wa miito mbalimbali kwa wadau wote wa kijamii :Kwanza wanaomba watu wote wasikubali mtindo wa maendeleo ya kuabudu miungu ya kufedha ambayo ushirikisha uchumi wa kifo, wenye kuleta hasara , ukosefu wa adhi ya mtu na haki za kibinadamu. Badala yake wanahamasisha kufikiria kutumia bidhaa za ndani kutoka kwa wakulima mahalia,wasikubali mitindo ya matumizi makubwa ya maisha au uharibifu wa misitu , mimea na wanyama.Kwa njia hiyo wanaalika kuelimisha vizazi vipya thamani yake inayosaidia kuunda jamii ya haki.
Pili Maaskofu wa Msubiji wanatoa onyo kwa Wakristo wote ili wasiwe vipofu na viziwi  mbele changamoto ya hali halisi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi katika nchi, bali wajikite  katika mshikamano wa kibindamu. Kwa mantiki hii Maskofu wanatoa ushauri wa kupanga kila jimbo la Msumbiji kufanya kozi ya Mafundisho jamii ya  Kanisa Katoliki  ili kila mtu aweze kutambua vema wajibu wa utume wake na nafsi yake katika Kanisa na jamii kwa namna ya pekee.

Vilevile katika hati hiyo hata makuhani na watawa wote kike na kiume wanaalikwa kuwa wajasiri wa katika utambuzi wa  hali ya ukiukwaji  haki dhidi ya wakulima na kuwa upande wao kuwatetea, wakati huo huo wahusika wa vyombo vya habari wametoa wito kutoa habari kwa upendo na ukweli ili wawe sauti ya watu na vipaza sauti vya wasiwasi wao. Kwa upande wa walimu na wanafunzi, wanaalikwa kujikita kwa kina katika kutambua maarifa ya viumbe, na kwa kufanya hivyo wameomba kuadhimisha adharani siku  juu ya suala hili katika  kupambana dhidi ya aina zote za uchafuzi wa mazingira, na kwamba si katika kuonesha mafundisho bali hata kutoa  umakini wa thamani na mitazamo yenye haki. Halikadhalika, Maaskofu wanakumbusha wanasiasa wakristo uwajibu katika  kuongozwa kwa mujibu wa Mafundisho jamii ya Kanisa ili kufanya kazi kwa njia kuwajibika na kimaadili ili waweze kuepukana na aina zozote za rushwa.

Katika kutazamia mwaka 2025 ambampo nchi ya Msumbiji itafikisha miaka 50 ya uhuru, Maaskofu wanatoa wito kwa ajili ya ufanisi wa mageuzi ya kilimo ambayo yaweza kurekebisha athari  mbaya katika nchi  ziliozosababishwa na  na sera za kisiasa za sasa, ili kuruhusu upatanisho wa watu na uwepo wa usawa katika ugawaji wa utajiri wa nchi unaotoka kwa Mungu. Hati hiyo ya Maaskofu wa Msubiji unamalizika kwa maombi ya Mama Maria wa Huruma.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.