2017-05-09 13:48:00

A.Kusini: Inahitajika mabadiliko ya uchumi kwa ajili ya vijana


Ni kitu kidogo cha kusheherekea wakati milioni ya vijana wa Afrika ya Kusini hawana ajira, ni maneno ya Askofu Abel Gabuzi wa Jimbo la Kimberly na Rais wa Tume ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya Haki na Amani nchini Afrika ya Kusini, katika ujumbe uliosambazwa kwa umma kwa njia ya vyombo vya habari  wakati wa tukio la siku ya Mei Mosi kimataifa 2017. Rais wa tume ya Haki na Amani anasema, ukosefu wa ajira kwa vijana katika nchi ya Afrika ya kusini umefikia ngazi ya hatari, vijana wengi wasio kuwa na ajira wako hatarini: waathirika wa madawa ya kulevya,  biashara ya binadamu, kujiingiza katika vitendo vya kialifu, vilevile kudanganywa na baadhi ya wanasiasa wasio kuwa na huruma ili wafanye  maandamano ya vurugu na ghasia  wakati wao  wanatulia katika maisha yao ya kisiasa.

Askofu Gabuza anaomba Serikali kupitia na kuchunguza kwa upya sera za  kisiasa hasa  ruzuku ya mishahara kwa vijana, kwasababu huo  ndiyo mpango hatari wenye gharama kubwa na siyo endelevu unaotumika katika makampuni mengine binafsi ambayo uongeza bila kutoa faida na wala kuunda mafunzo ya lazima kwa ajili ya vijana ili waweze kupata ajira ya kudumu.
Aidha ujumbe wa Askofu Gabuza unasema; ni mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayoweza kutatua janga la ukosefu wa ajira kwa vijana, lakini  kwa bahati mbaya anabainisha, utamaduni wa sasa katika uongozi wa kisiasa ambao umetanda mizizi  katika ufisadi na upendeleo wa kisiasa  hauna uwezo kimaadili katika ukufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na ukuaji wa umoja.
Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.