2017-05-08 09:20:00

Wazalendo wa Togo wamekata tamaa hawajuhi njia ipi ya kufuata!


Kuchanganyikiwa kwa jamii ya nchi ya Togo ni bomu ambalo liko tayari kulipuka  wakati wowote. Ni maneno yanayosomeka katika ujumbe wa Baraza maaskofu wa Togo wakati wa kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru iliyofikia kilele chake  tarehe 27 Aprili 2017.  “Ebu sote tutambue nyuma ya kivuli cha amani na utulivu kwasababu nchi ya Togo imeugua.Watoto wake daima wanazidi kukata tamaa na hawajuhi njia ipi ya kuchukua ili kuondokana na hali ya sasa ya kufikia amani. Maendeleo endelevu yanaonekana kukwama”.

Maaskofu wanasema,“kanuni ya kubadilishana kisiasa hata kabla ya kuwa na thamani ya kidemokrasia zaidi ni msingi wa mahitaji ya utaratibu wa kawaida”. Mwaka 2005 baada ya kifo cha Gnassingbé Eyadema aliyeongoza nchi kwa muda wa mika 38, alifuata madarakani mtoto wake Faure Gnassingbé, ambaye kwa miaka 12 anaongoza nchi. Maaskofu hao wanaonesha kupinga hatua ya kuongeza muda wa kuendelea na urais kama vile kinachotokea katika nchi nyingine za Afrika kwa mfano wa nchi ya Burundi.

Maaskofu wanasema,ukosefu wa kutokuwa wazi unajenga watu kuchanganyikiwa kwa watu  hasa tangu serikali kuonesha udhaifu wa kutoweza kutoa haki ya kweli kwa  jamii katika ugawaji sawa wa utajiri wa nchi. Chanzo cha uovu huo nchini Togo, Maaskofu wanaandika, ni mabadiliko ya utumishi wa umma. Wanasema; badala ya kuwalinda maskini,Serikali hupendelea matajiri ambao hawafanyi lolote badala yake ni kujinufaisha  kwa mali zao. Hii ni aibu si kwamba kuna matajri na maskini!. Aibu ipo ukweli taasisi ambazo zinapaswa kuanzisha mchakato wa kuunda uwiano wa chini katika jamii ndiyo kwanza wanajipendelea wao wenye bila kujali wengine  au huchagua nafasi ya matajiri ili wapate kujificha huko.

Kutokana na mchakato wa mjadala wa nchi juu ya mabadiliko ya katiba unao endelea, Baraza la Maaskofu,linatoa wito kwa wanasiasa wasipoteze fursa hii katika kufanya mageuzi yanayotarajiwa na idadi kubwa ya  watu, kwa namna ya pekee juu kutazama mustakabali wa nchi katika mamlaka ya kugombea urais na namna ya utaratibu wa uchaguzi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.