2017-05-08 09:09:00

Wanafunzi 82 kuwa huru kutoka mikononi mwa Boko Haram tangu 2014


Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram nchini Nigeria kimeaachia huru wanafunzi wa kike 82 miongoni mwa 276 waliokuwa wametekwa nyara katika Shule ya Chibok mwaka 2014 , Kaskazini mwa nchi hiyo.Wameachiwa huru mapema mwisho wa wiki iliyopita baadaya ya mchakato wa mazungumzo marefu kati ya Serikali ya Abuja na kikundi cha itikadi kali cha Kiislam.
Wanafunzi hawa wamekuwa mateka tangu tarehe 14 Aprili 2014,  na kuachiwa huru kumetokana na makubaliano kati ya kikundi cha kigaidi na serikali ya kuwaachiwa huru wafungwa wa kundi hilo. Taarifa kutoka nchini Nigeria  zinaripoti kuwa wasichana hao baada ya huru wao walikuwa  mikononi mwa maafisa wa Ulinzi karibu na mpaka kati ya Nigeria na Cameroon kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya kabla ya kusafirishwa kuelekea Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno na hatimaye mjini Abuja, mahali ambapo wakutana na Rais wa nchi Muhammadu Buhari.

Japokuwa tukio la kutekwa nyara wasichana wa shule ya mji wa Chibok limepewa uzito mkubwa kieneo na kimataifa lakini kundi la kigaidi la Boko Haram limeshateka nyara maelfu ya watu wakiwemo watoto wadogo, ambao wengi wao kesi zao hazijapewa uzito wala kushughulikiwa.
Halikadhalika tangu kutokea tukio hili kampeni nyingi zimefanyika za kimataifa,ikumbukwe hata ile kampeni ya Michelle Obama, lakini pamoja na hayo taarifa  kutoka Nigeria zimebainisha kuwa Uswisi na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu zimesaidia kufanikisha kuachiwa huru wasichana hao baada ya kufanyika kile kilichoelezwa kama mazungumzo marefu

Zaidi ya wasichana 20 waliachiwa huru mwezi Oktoba mwaka jana katika mapatano yaliyosimamiwa na shirika la Msalaba Mwekundu. Wasichana wengine kadhaa walitoroka kutoka mikononi mwa kundi hilo la kigaidi la Boko Haramu,lakini inaaminika kuwa  pamoja  kuachia uhuru wasicha hao bado wanakosekana zaidi ya wasicha na 100 wanaoshikiliwa na Boko Haram.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.