2017-05-08 11:38:00

Maaskofu wa Kenya wanashutumu uchoyo na ubaguzi wa wanasiasa!


Ukosefu wa uwezo uliooneshwa na wingi vya vyama vya kisiasa katika uchaguzi wa hawali ,umeonesha jinsi gani mfumo wa Kisiasa nchini Kenya ulivyo mdhaifu kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu. Ni ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa Kenya uliotolewa na Fides hivi karibuni  ambapo Maaskofu wa Kenya wanaelezea wasiwasi wao kuhusu mvutano wa kisiasa unao athiri nchi yao. Maaskofu hao wanaeleza kuwa uchaguzi wa hawali uliofanywa na chama kimoja kimoja kuchagua wagombea wa kuwasilisha katika uchaguzi Mkuu mwezi Agosti,umekuwa na sifa ya udanganyifu, mvutano na vurugu.

Katika ujumbe huo Maaskofu wa Kenya wanasema, tunavyo vyama vya kisiasa ambavyo havina uwezo wa  kuendesha mchakato wazi na ipasavyo katika kuonesha amani ya kidemokrasia ya ndani. Hali kama hiyo tayari  imeonesha wasiwasi mkubwa  unaoweza kujitokeza hasa machafuko na vurugu wakati wa uendeshaji wa uchaguzi Mkuu mwezi Agosti. Na hofu hiyo imejionesha hata katika baadhi ya wawekezaji wa kimataifa na watalii ambao wameanza kuacha nchi ya Kenya. 
Bara la Afrika linakabiliana na mgogoro mbaya zaidi wa chakula kwa mihongo pia dharura kutokana na ukame. Maaskofu wanashutumu vingozi wakisema, hilo ni janga lakini ni pamoja na viongozi wenyewe kwasababu wanapoteza rasilimali chache zilizopo kununua kura. Kwa njia hyo katika ujumbe wanasema, utamaduni wa uchoyo na ubaguzi unazidisha hali ya sasa kuwa ngumu na ndiyo maana wakenya sasa wana msukumo wa nguvu wa mawazo ya kukata tamaa.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.