2017-05-07 09:32:00

Vijana wasiwe na hofu ya kukabiliana na utamaduni wa uharibifu!


Kushinda utamaduni wa uharibifu wanachokiita mama ni bomu na kuonesha katika televisheni mambo mabaya kwa ajili ya kutafuta sifa kwa watazamaji. Ni maneno yaliyotamkwa na Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 6 Aprili 2017, wakati wa mazungumzo kati ya wanafunzi walioudhuria Mkutano ulioandaliwa na Mpango wa Kitaifa kwa Mashirika mahalia kwa ajili ya amani  na haki ya binadamu katika Ukumbi wa Nwenye Heri Paulo VI mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena anashutumu janga la unyonyaji wa kazi na kutoa  wito kwa kila mtu kujikita zaidi katika  kulinda mazingira. Aidha  amechangamotisha  vijana wanafunzi wa Italia wanaojikita katika mashirika mahalia kwenye masuala la amani  kukabiliana na kushinda bila woga utamaduni wa uharibifu kwa nguvu ya unyenyekevu. Anawashukuru  wanafunzi hao kwa maswali halisi ambayo yanatia uchungu kutokana na majanga mengi yanayotesa ulimwengu  kama vile vita, umaskini na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Hawali ya yote  Baba Mtakatifu anabainisha kwamba leo hii hakuna jibu hata kwa ajili ya watoto maana  anasema  hata  televisheni kwasababu wanaonesha habari za uharibifu na kwamba utafikiri majanga haya ndiyo yenye mafanikio.  Kwa mara nyingine tena amekumbuka kipeo cha wahamiaji, ambacho amesema ni janga kubwa Ulaya baada ya Vita ya pili ya Dunia; kwa namna hiyo mawazo yake yametazama juu ya vurugu na vita vinavyoharibu uso binadamu. Anasema, “tunaishi katika kipindi kugumu baada ya vita ya Pili  ya dunia,pamoja na kwamba ndiyo kuna watu wema katika dunia wanaoonekana, lakini dunia iko katika vita”. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasema,  wambie neno  ninyi mlio katika shule ya amani ya kwamba dunia iko vitani; ametoa mfano juu ya mabomu yanayorushwa hovyo katika mahospitali  na mashuleni wakati kuna wagonjwa na watoto na kwamba hawa hawajali.  Ni aibu ya damu ya watu wasiokuwa na hatia inayoendelea kumwagika kila kukicha kutokana na vita, dhuluma na nyanyaso za kila aina, Ni aibu kusikia jina la bomu, mama wa mabomu yote. Tazameni mama anatoa maisha, wakati hawa wanatoa vifo.

Katika mifano hiyo Baba Mtakatifu pia anatambua  udhaifu  wa viongoza wengi wa kimataifa. Na ameonya akisema,  kwa upande mwingine wanaomba amani, lakini  ndiyo wazalishaji silaha na ndiyo biashara. Kuna wafanya biashara ya kuwauzia wale wenye kinzani za kivita na hivyo hawa wanapata  faida juu ya vifo vya watu wengine. Vilevile ,bado Baba Mtakatatifu anashutumu biashara ya madawa ya kulevya ambayo yanaharibu maisha ya vijana wengi. Anashutumu akisema katika kitovu cha uchumi, ipo dhamana ya kutafuta fedha na utawala wa binadamu, hapa akimaanisha hasa hatma ya kazi nyeusi na  unyonyaji wa watu  pamoja na watoto. Baba Mtakatifu anasema; hali hiyo haijitokezi katika bara au nchi ya mbali ni hapa Ulaya,hapa Italia, mahali ambapo unyonyaji wa watu unazidi katika kuwalipa watu kidogo baada ya kufanya mkataba wa kazi tangu Septemba hadi Mei, miezi mingine miwili bila kazi kwa kusubiri Septemba tena. Hiyo inaitwa uharibifu, na wakatoliki wanaita unyonyaji wa namna hii ni dhambi ya kufa.

Baba Mtakafu Francisko anabainisha mada ambayo mara nyingi amekuwa akisistiza kwa wote inayohusu masengenyo na kurudia kusema ni ugaidi wa kweli, kwani ni kuharibifu wa watu, kwa maana hiyo anawashauri  vijana wajiume midomo yao kabla ya kutoa maneno ya kusema wengine vibaya.Wakati huo huo wameonya kuwa na tahadhari ya vurugu ya matusi dhidi ya wengine, ambapo amebainisha kwamba tabua hizo zinaonekana  hata katika mijadala ya kisiasa. Ili kukabiliana na hayo yote anasema inahitaji mtazamo wa unyenyekevu. Anafafanua kwamba; kuwa mpole  au mtazamo wa unyenyekevu haina maana ya kuwa mjinga: maana yake ni kisema mambo kwa amani, utulivu bila kuathiri au kutafuta namna ya kusema bila kudhuru. Hata hivyo Baba Mtakatifu anasema upole ni mojawapo ya karama ambayo tunalazimika tena kujifunza na kkuigundua kwa upya katika maisha yetu. Na hii husaidia sana katika mazungumzo yetu na siyo kuwa kivumishi cha watu. Ni lazima kuacha kwa upole ambao ndiyo tabia ya unyenyekevu dhidi ya vurugu.

Ametoa wito kwa vijana wasitoe  maneno kamwe ya kudhuru wengine, kwa maana  hiyo amesisitiza juu ya ujenzi wa mtakaba wa elimu kati ya shule na familia ili kukuza na kuhamasisha jamii kwa manufaa ya wote . Amewataka vijana kushiriki kikamilifu hasa katika kusikiliza, na walimu wao kujitoa muda wao katika kujikita  kwenye  elimu ya amani. Mwisho amesema Baba Mtakatifu kwa uchungu akishutumu uharibifu wa zawadi ya thamani ya Viumbe tuliyopewa na Mungu.Anasema uharibifu huo umetokana zaidi na matumizi mabaya yaliyoongozwa na majaribio ya mimea na wanyama kwa kuibua magonjwa nadra. Haya ni matukio ya kutisha kama vile “ ardhi ya moto au uchafuzi wa Bahari ya meditranean. Na mwisho amegusia hatari ya maneino mengi yaliyotolewa lakini juhudi kidogo baada ya Mutano wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.