2017-05-06 15:30:00

Mchakato wa wenyeheri na watakatifu wapya wakamilika!


Tarehe 4 Mei 2017 Baba, Mtakatifu Francisko alikutana na Kardinali Angelo Amato, Rais wa Baraza la Kipapa la kutangaza Watakatifu, na kukubali kuwatangazwa watumishi wa Mungu kuwa wenye heri ,Francesco Solano Casey Padre  wa Shirika la ndugu wadogo Wakapucini, aliye zaliwa tarehe 25 Novemba 1870 na kifo chake 31 Julai 1957. Mtumishi wa Mungu  Maria  Concetta, Mwanzilishi wa Shirika la Mabinti wa Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili, aliyezaliwa tarehe 10 Juni 1789 na kifo chake tarehe 10 Januari 1828.

Mtumishi wa Mungu Chiara Fey Mwanzilishi wa Shirika la Watawa wa kike Maskini mtoto Yesu , aliyezaliwa tarehe 11 Aprili 1815 na kifo chake tarehe 8 Mei 1894. Mtumishi wa Mungu Caterina Maria ,Mwanzilishi wa Shirika la Watumishi wa Moyo Mtakatifu wa  Yesu , aliyezaliwa tarehe 27 Novemba 1823 na kifo chake 5 Aprili 1896. Mtumishi wa Mungu na shahidi Luciano Botovasoa, mlei na baba wa familia wa Shirika la wasekulari wa  Mtakatifu Francisko aliyeuwawa huko Madagascar  tarehe 17 Aprili 1947.

Mtumishi wa Mungu Elia dalla Costa , Kardinali wa Jimbo Kuu la Firenze Italia, aliyezaliwa tarehe 14 Mei 1872 na kifo chake 1961. Mtumishi wa Mungu Francesco Saverio Nguyên Van Thuân Kardinali wa Kanisa la Roma aliyezaliwa tarehe 17 Aprili 1928 na kifo chake tarehe 16 Septemba 2002.
Mtumishi wa Mungu Giovanna Meneghini, mwanzilishi  wa Shirika watawa wa Moyo Mtakatifu wa Maria  (Ursura) , aliyezaliwa tarehe 23 Mei 1868 na kifo chake tarehe  2 Machi 1918. Mtumishi wa  Mungu Vincenza Gusmano aliyekuwa Mkuu wa kwanza wa Shirika la Watumishi  Maskini, aliyezaliwa tarehe 6 Januari 1826 na kifo chake  tarehe 2 Februari 1894.

Mtumishi wa Mungu Alessandro Nottegar Mlei na baba wa familia, mwanzilishi wa Jumuia ya Regina Pacis aliyezaliwa tarehe 30 Oktoba 1943 na kifo chake tarehe 19  Septemba 1986. Mtumishi wa Mungu  Edvige Carboni mlei aliyezaliwa tarehe 2 Mei 1880 na kifo chake tarehe 17 Februari 1952. Mtumishi wa Mungu Maria Guadalupe Ortiz de Landázuri y Fernández de Heredia, mlei na mwanachama wa Opus Dei, aliyezaliwa tarehe 12 Desemba 1916 na kifo chake  tarehe 16 Julia 1975.

Wakati huo huo, Kardinali Angelo Amato akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusiana na kutangazwa kwa mashahidi saba kuwa wenye heri wapya wa Kanisa tarehe 6 Mei 2017  wa Shirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Gironoa nchini Hispania amesema, ni tukio lilitendeka mwaka 1936 wakati wa nchini Huispania wanatesa wakristo. Watawa hawa kwa matashi ya Mkuu wao wa Chuo cha Kitume Canet wa Mar Catalonia huko Barcelona nchini Hispania aliwaruhusu kuondoka chuoni il wapate mahali pa kujikomboa. Wengine walifanikiwa lakini wengine hawakuweza kufanikiwa kutokana na kugunduliwa wakati wanavuka mpakani ufaransa. Mashahidi hao walipelekwa katika Wilaya wa Girona na kuwawa huko.Kikundi cha mashahidi hao kilikuwa na mapdre wanne na ndugu walei watatu. Aliyekuwa na umri mkubwa ni Padre Hortigüela  wa miaka 28 na mdogo alikuwa ni Frateli Jose wa Amo wa miaka 20.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.