2017-05-03 17:03:00

Papa: Hija ya kitume nchini Misri, kielelezo cha matumaini mapya!


Injili ya Jumatano ya Katesi ya Baba Mtaktifu Francisko: “Walipokuwa wamekwisha kuondoka, tazama! malaika wa Bwana akamtokea Yosefu katika ndoto, akisema: “Simama, mchukue huyo mtoto mchanga na mama yake mkimbie kuingia Misri, mkae huko mpaka nikupe agizo; kwa maana Herode yuko karibu kumtafuta huyo mtoto amwangamize.  Kwa hiyo akasimama na kuchukua pamoja naye mtoto huyo mchanga na mama yake wakati wa usiku, akaondoka na kuingia Misri, naye akakaa huko mpaka kufa kwa Herode, ili litimizwe lile lililosemwa na Mungu kupitia nabii wake, akisema: “Kutoka Misri nilimwita mwanangu.”( Mt 2,13-15).
Leo ninapendelea  kuwasimulia juu ya safir yangu ya kitume ambayo kwa msaada wa Mungu ni meweza kuikamilisha siku zilizopita huko Misri. Nilikwenda katika nchi hiyo kwa ajili ya mialiko minne kwanza wa Rais wa Jamhuri ya nchi,  pili Patriaki wa Kikoptiki wa Kiorthodox, tatu Imamu Mkuu Al-Azhar na Mwisho Patriaki wa kikoptiki katoliki. Shukrani ziwandee  kila mmoja kwa makaribisho yao ya upendo mkuu niliyoyapata. Ninashukuru watu wote wa Misri kwa uwepo kwa wingi na upendo  walionesha  khalifa wa mtume Petro kwa siku hizo.

Ni utangulizi wa  tafakari  ya  Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kuanza katekesi yake ya kila Jumatano tarehe 3 Aprili 2017 katika viwanja vya Mtakatifu Petro Vatican, akiwashirikisha waamini na mahujajaji wote juu ya ziara yake ya kitume nchini Misiri.
Rais na viongozi wa serikali walijitahaidi katika shughuli  ya ajabu sana ili  kila kitu kufanyika vizuri, na ili iweze kuwa ishara ya amani kwa ajili ya Misri na na kwa ajili ya kanda hiyo, amabayo kwa bahati mabaya inateseka na ghasia na pia magaidi, na ndiyo maana kauli mbiu ya Ziara ilikuwa “Papa wa amani nchini Misri.

Ziara katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar , chuo cha kiislam cha kizama , ni taasisi ya eleimu ya Juu ya waislam suni , ambapo chuo hicho kina upeo wa aina mbili ikiwa ni  mazunguzo  kati ya wakristo na waislam, wakati huo huo na  kuhamasisha amani katika dunia. Katika chuo kikuu hicho imefanyika mkutano wa Imamu Mkuu, na baadaye kupanuka kwa kufanya mkutano wa kiamatiafa kwa ajili ya amani.
Katika mantiki hiyo, Baba Mtakatifu alifanya tafakari inayotoa thamani ya  historia ya Misiri kama nchi ya ustaarabu wa mambo ya  kale na ardhi ya magano. Kwa binadamu wote  wanatambua kuwa Misri ni sawa na ustraarbau wa mambo ya kale , katika thamani yake nyenye  tunu ya kisanii na ufahamu. Hiyo inafundisha kwamba amani inajengwa kwa njia ya elimu, mafunzo ya hekima, na ubinadamu unao tambua kwamba sanaa ni sehemu ya muhimu ya kidini, uhusiano na Mungu, kama alivyo wakumbusha Imamu Mkuu katika hotuba yake. Amani inajengwa kuanzia na agano kati ya Mungu na binadamu. Msingi wa agano  kati ya binadamu wote , unasimama juu ya amri za Mungu zilizoandika katika meza ya jiwe  mlimani Sinai, lakini zaidi ya kina katika moyo wa binadamu wa nyakati zote, kila mahali, ni sheria inayo kusanyika  katika amri ya upendo wa Mungu na jirani.

Msingi huo pia ndiyo msingi wa mfumo wa ujenzi wa kawaida wa umma na jamii ambao unawataka wananchi wote kushirikiana  , kutoka vyanzo vyote, utamaduni na dini. Maono haya mema yaliibuka katika kubadilishana hotuba na Rais wa nchi ya Misri, mbele ya  viongozi wa nchi na wa kidplomasia. Sehemu kubwa ya kihistoria na kidini katika nchi ya Misri, na nafasi yake katika kanda ya Mashariki ya kati zinawawaajibisha katika kazi muhimu  ya kuelekea njia ya amani ya kudumu  ambayo inasisimamia sheria ya nguvu, lakini katika  nguvu ya sheria. Wakristo wa Misri kama wakristo wa nchi yoyote ile duniani wanaalikuwa kuwa chachu ya undugu. Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kusema, hiyo inawezekana kama  wataweza kuishi wao wenyewe katika muungano na Kristo. Ishara ya nguvu ya umoja kwa neema ya Mungu imewezekana wakat wa kubadilishana hotuba pamoja na kiongozi Mkuu mwenzake  Tawadros II ambaye ni Patriaki wa Kikoptiki wa Kiorthodox. Wao pamoja walirudia kwa upya ahadi zao za ubatizo,hata katika kusaini Azimio la pamoja kwa ajili ya kutembe pamoja ili wasirudie kufanya ubatizo kwa upya katika makanisa husika. Kwa pamoja walisali kwa ajili ya mashahidi wa hivi karibuni katika mashambulizi ya kusikitisha ya kigaidi katika Kanisa lenye heshima. Anaongeza kusema; Damu yao inarutubisha sasa mkutano wa kiekumene ambapo aliudhuria pia Patriaki wa Costantinopoli Bartholomew. 

Siku ya Pili ya ziara yake, Baba Mtakatifu Francisko anasimulia kuwa, ilikuwa ni kwa ajili ya waamini, kwani waliadhimisha misa takatifu katika uwanja wa mpira uliowekwa kwa  kwa ajili hiyo na viongozi wa Serikali ya Misiri ambapo ilikuwa ni sikukuu ya imani na undugu ,kwasababu walijisikia uwepo hai wa Bwana Mfufuka. Baba Mtakatifu akitafakari Injili amesema , aliwataka jumuiya ndugu  wakatoliki wa Misri, waweze kuishi kwa upya ule uzoefu wa mitume wa Emau: yaani kwa kumtafuta daima Kristo , katika Neno , kushiriki katika kuumega mkate wa maisha ya kila siku, furaha ya imani, matumaini ya kweli na katika nguvu ya kushuhudia upendo ya kwamba wamekutana na Bwana.

Daki za mwisho kabla ya kurudi nchini Italia Baba Mtakatifu Francisk amesema alikutana na mapadri, watawa kike na kiume , waseminari kutoka Seminari kuu,kuna waseminari wengi na hiyo ni kitulizo ameongeza. Hiyo ilikuwa ni ibada ya Neno ambapo walirudia ahadi zao za maisha ya wito.Anaendelea kusema kuwa, katika jumuiya hii ya wanaume na wanawake walio chagua kujitoa maisha yake kwake Kristo na kwa ajili ya ufalme wa Mungu, ameona uzuri wa Kanisa la Misiri na amesali kwa ajili ya wakristo wote wa Makanisa ya Mashariki ya Kati, ili kwa maongozi ya wachungaji wao, na kongozwa na watauwa waweze kuwa chumvi na mwanga katika nchi hizo kati ya watu wote.

 Ameongeza Baba Mtakatifu Francisko akisema kwa upande wetu nchi ya Misri imekuwa ishara ya matumaini ya wahamiaji na msaada. Ametoa mfano juu ya historia ya maandiko matakatifu kuhusu wakati ule dunia ilipokuwa na njaa Yakobo na wanae walikwenda huko. Hata Yesu alipotaka kuwawa alikwenda huko; aidha amesema juu ya  kuwasimulia ziara hiyo inajikita katika katika njia ya kuonesha  matumaini ya kwamba nchi ya Misri kwetu sisi ni ishara ya matumaini hata katika nykati za sasa.Amemaliza kuelezea juu ya ziara yake Baba Mtakatifu akisema  anawashukuru wote walio wezesha ziara hiyo  hata wote kwa namna moja au nyingine wametoa mchango, hasa zaidi watu wengi waliotoa sadaka zao na sala kwa ajili ya wale wanaoteseka. na kwamba Familia Takatifu iliyo hamia  kando ya mto wa Nile wakati wanakimbia mashambulizi ya Erode iwabariki na kuwalinda watu wa Misri na kuwaongoza  katika njia njema ya undugu na amani.

Baada ya katekesi
Mara baada ya katekesi yake Baba Mtakatifu Francisko amesalimia mahujaji wote kutoka pande za dunia, na zaidi wanaongea lugha ya kiarabu, kwa namna ya pekee wanaotoka Misri na nchi za  mashariki ya kati. Anawashukuru watu wote walio wezesha kufanikisha ziara yake huko Misri, kwa mwaliko wa ukarimu na mapokezi mema; Bwana awabariki na kuwalinda na maovu yote. 

Akiwasalimia watu kutoka Poland;amekumbuka kuwa tarehe 3 Mei, Kanisa la Poland linafanya  sikukuu ya Bikira Maria wa Poland pia ni sikukuu ya Kitaifa. Amewataka wasikilize kwa upendo na makini maelekezo ya Malkia wao, wanaye mwita kuwa;  “yeye ni mkuuu wa sifa ya kitaifa”. Katika uchaguzi wa maisha yao ya kila siku wafuate njia mapatano na usikivu. Wafanye uchaguzi muhimu wakitafuta ukweli kwa ajili ya wema na amani. Wawe wazi na upendo kwa mahitaji ya ndugu. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amebariki nchi yao na watu wote wa Poland mahali popote walipo duniani.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.