2017-05-03 16:10:00

Mataifa fanyeni kazi kwa pamoja kwa ajili ya kukuza amani duniani


Hotuba ya Monsinyo Urbanczyk  Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa  kwenye ofisi zilizoko huko Viena katika Kamati ya kwanza ya Maandalizi ya Mkutano wa kupitia Mkataba kuhusu kusitisha silaha za kinyuklia 2020. Kikao cha Kamati ya kwanza  imenza tarehe 2 na inatarajiwa kumalizika tarehe 12 Mei 2017. Monsinyo Janus Urbanczyk anasema silaha za nyuklia zinaunda usalama wa uongo, kwasababu  anakumbusha wakati Vatican ilipojiunga mwaka 1971 katika mkataba huo walitaka kuchangia jitihada za kukuza usalama na ushirikiano wa amani katika mahusianao kati ya watu. Hivyo hata sasa kwa uwepo wa Vatican katika Kamati ya Maandalizi  imeongozwa na shahuku  ya kushirikiana kwa pamoja katika kazi kwa ajili ya kuiwezesha dunia iwe huru bila silaha za kinyuklia.

Pamoja na hayo yote lakini hadi sasa Jumuiya za Kimataifa katika kutumia mkataba huu ili dunia iweza kuwa na amani bado haijatosheleza , kwa njia hiyo Monsinyo Urbanczyk anasema, Vatican inatoa wito wa kufanya maendeleo halisi ya mkataba ulio wekwa ili kufikia lengo kuu la mwisho la kusitisha silaha za kinyuklia. Aidha Vatican ipo tayari kushiriki kwa namna ya pekee katika ujenzi wa mchakato huo . Amani lazima itambuliwe kama nguvu kazi ambayo inahitaji juhudi za kila mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
Maadili ya undugu na ushirikiano wa amani kati ya watu na kati ya mataifa ndiyo inatkiwa anaeleza Monsinyo , kama katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko  katika Siku ya Kimataifa ya Amani  mwaka huu kwamba, hatuwezi kuwa na mantiki ya hofu , vurugu na kufungwa, bali katika uwajibikaji, heshima na mazungumzo ya dhati.

Katika ujumbe huo anakumbusha  Monsinyo Urbanczyk kuwa  Baba Mtakatifu Francisko  alikuwa anatoa wito juu ya ukomeshaji wa silaha za kinyukilia na hata utengenezaji wake, kwani kutozuia makosa yasitendeke na tishio la uharibifu wa pamoja haviwezi kuwa na msingi wa aina ya maadili.
Vatican pamoja na kuuunga mkono juhudi na mazungumzo kuhusu hali hiyo na kuunda chombo cha kisheria cha kupiga marufuku silaha za kinyuklia bado inafuatilia kwa wasiwasi mkubwa wa hali ya kisiwa cha Korea. Monsinyo anakumbusha kuwamba Vatican inasaidia juhudi za Jumuiya ya kimataifa kwenye uzinduzi wa kampeni mpya ya wa mchakato wa kusitisha nyuklia na pia juu ya amani. Anahitimisha katika kutoa wito kwa viongozi wote Serikali na kisiasa kwamba siyo tu kutaka kuhakikisha usalama wa wananchi wake tu , bali inahitajika kufanya kazi kikamilifu  kwa ajili ya ukuaji wa  amani kimataifa ambapo binadamu wote wana haja kubwa.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.