2017-05-01 07:56:00

Vijana wanayo nia ya kukabiliana na changamoto


Ni karibu muhongo mmoja inaadhimishwa Siku  ya Chuo Kikuu  Katoliki. Ni mojawapo ya tukio katika kalenda ya kila mwaka kwa wakatoliki nchini Italia, kufanya kumbukumbu hii. Siku ya chuo Kikuu Katoliki imeandaliwa na Chuo Kikuu Katoliki cha Toniolo Milano mbapo ni fursa ya kujikita kwa ndani katazama malengo ya Chuo Kikikuu katika msingi na thamani yake inayo waongoza katika kufanya  uchaguzi wa kila siku.
Katika kilele cha maadhimisho ya 93 ambayo yamefanyoka Jumapili tarehe 30 Aprili 2017, ikiwa na kauli mbiu “kujifunza ulimwengu ambao umekwisha badilika”, Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican, ametuma ujumbe wake kwa Rais wa  Chuo Kikuu Katoliki cha Milano ambaye ni Kardinali Angelo Scola, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Milano na kusema kuwa uwajibikaji wa mafunzo ya elimu ya  juu malengo yake ya mwisho yasiwe ya ubinasi, bali uwe ndiyo msukumo wa kwenda katika upeo wa nje.

Ni vema kwamba  manufaa ya kuhitimu yawe ndiyo hisia binafsi inayowaongoza vijana katika njia ya kuendelea na masomo ya juuu ambayo yanakuwa makamilifu kwa upeo  wa juukwa ajili yao binafsi, wengine na hata katika dunia.Kwa namna hiyo shuhuku  ya haki , ukweli , uzuri uweze kutawanywa katika kila moyo wa binadamu ili kumsukuma katika mabadiliko, ya ujenzi wa majibu kwa ajili ya ulimwengu wa haki na kweli kutokana na kukomaa katika njia hiyo ya akili ya binadamu kwa  miaka ya  mafunzo ya chuo kikuu. Matukio mengi sana yanatoa msukumo kutazama kwa upya na hasa kuzingatia vijana.Kwa upande wao ,kuna umuhimu wa kutafakari pamoja kutokana na thari na wasiwasi mkubwa wa kiuchumi  na kijamii kwa nyakati zetu,unaoleta kwa upande mwingine mahangaiko fulani ya kiroho. Wasiwasi wa kutokuwa na uhakika wa maisha endelevu na zaidi ukosefu wa ajira,suala la uhamiajai, matatizo yanayo kabiliana nayo katika kuingia maisha ya jamii  hasa uhalisia wa kupanga mikakati ya kuunda maisha ya familia,ni changamoto inayobaki tete zaidi katika vizazi endelevu.Lakini pamoja na vipengele hivi muhimu, vijana wanabaki na matumaini makubwa kwa nguvu ya uzoefu kwa ajili ya kujenga maisha bora ya baadaye.

Pamoja na hayo yote  mkono wa  Yesu unaendelea kuwalinda na pia  kuwatazama kwa matumaani, ukarimu ,kwa njia ya Kanisa kutokana na kuendelea na mipango ya kitume na mafunzo. Uwajibikaji huo unajikita zaidi  hasa katika maamuzi ya Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya kukabiliana na Sinodi ijayo ya Maaskofu yenye mada ya Vijana. Imani na Mang’amuzi ya miito. Mpango wa Sinodi ni kutoka kuonesha kwa dhati ukaribu na upendo wa binadamu wote kwa ujumla wa Kanisa kwa kizazi endelevu, wakati huo huo ni kutaka kugundua kwa pamoja na vijana ili  wao wawe mstari wa mbele katika maisha ya Kanisa na Jamii. Katika kuwajulisha vijana umuhimu wa matukio ya Kanisa, Baba Mtakatifu Francisko anawaalika kutafakari kwa kina imani ya Ibrahimu katika nyakati zetu,kwani yeye anatusukuma kwenda katika ardhi mpya ( Taz. Barua kwa Vijana 13 Januari2017). Baba Mtakatifu Francisko anawauliza vijana, je ardhi ni ipi kama siyo jamii ya haki na undugu ambao ninyi mnapenda kwa kina kuijenga hadi miisho ya dunia?

Pamoja na hayo yote vijana wanayo shahuku ya nguvu ya kwamba wasibaki watazamaji hivyo Baba Mtakatifu anawaalika wasizuie kilio chao cha dhamiri kitokacho ndani ya mioyo kwasababu kijana hakubalini  na manyanyaso,ukosefu wa haki,utamaduni wa kubagua, na hata kukobea katika utandawazi wa utofauti. Ni katika mang’amuzi makini yaweza kusaidia vijana kukabiliana na changamoto kubwa. Lakini mang’amuzi hayo yanahusu watu wote kwa nyanja zote za maisha, inahitaji kusindikizwa na viongozi kwa njia ya wahudumu wa kichungaji wa kawaida ndani ya jumuiya,vyama vya Kanisa hata katika taasisi zote zenye uwezo wa kuhakikisha uwepo wa sifa ya kisayansi katika mafunzo ya utamaduni na kiroho.

Katika eneo hili jukumu kubwa muhimu ni juu ya Chuo Kikuu Katoliki, ambacho kimekabidhiwa utume wa kuandaa vijana wenye kuwa na uwezo wa kukuza rasilimali zao kiakili, ukarimu wa moyo kwa nguvu ya Roho wa maisha yao kwenye njia ya maisha endelevu ya ubinadamu. Kwa njia hiyo Chuo Kikuu hicho bado kina majukumu ya kuchangia na kuendeleza kwa uamininfu na ubunifu wa mpango ulio anzishwa na Padre Agostino Gemelli na washiriki wake wa Chuo Kukuu Katoliki cha Italia ambacho kinazidi kuwa  kiungo kikuu kwa vijana wote wenye hamu ya kutoa mchango kwa ajili ya jamii ya haki na iliyo wazi na mshikamano.  Kwa namna hiyo ni kuwatia moyo katika shughuli za Jumuiya ya Kanisa ya Italia ili kuendelea kusaidia Taasisi kuu ya elimu ambayo mwaka 2017 imefikia maadhimisho ya 93 yenye kuwa na kauli mbiu “ kujifunza ulimwengu ambao umekwisha badilika, ili ipate kutoa fursa ya kutafakari juu ya kujifunza na mafunzo kwa ujumla ya binadamu ambayo yanatazama mabadiliko ili wote waweze kutoa mchango katika kujenzi wa dunia iliyo bora tunayoishi.

Hii ni hisia ya kina kwa maana ya masomo ya Chuo Kikuu pia kipindi cha masomo ni  muhimu kwa utambuzi binafsi na jamii. "Katika mazingira yoyote, hasa katika vyuo vikuu".Aliyasema Baba Mtakatifu Francisko  akizungumza hivi karibuni katika Chuo Kikuu mjini Roma Tre - kwamba ni muhimu kusoma na kukabiliana na mabadiliko haya ya enzi za sasa , kutafakari na pia kufanya  mang’amuzi, yaani, bila ya kiitikadi, chuki, bila hofu au kutoroka." Mang’amuzi  hayo yanasaidiwa na ukweli kwamba "chuo kikuu ni sehemu ya nafasi ya upendeleo ambayo inalea dhamiri katika kupambana dhidi ya mahitaji  mema, ya kweli na mazuri, vilevile ukweli wake katika utata,” (Hotuba katika chuo kikuu Roma Tre  17 februari 2017).

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.