Nini maana ya nafasi ya Makanisa katika ujenzi wa amani, je ni changamoto gani na fursa zipi za kiekuene zinazojitokeza? Ni baadhi ya maswali ya kujiuliza katika meza ya mduara wa kikundi cha kazi wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni (World Council of Churches - WCC) na Kanisa Katoliki walio kutana kuanzia tarehe 24- 26 Aprili 2017 mjini Dublin Ireland. Mwaliko wa mkutano huo ulitolewa na Askofu Mkuu wa Dublin Diarmuid Martin ambaye pia alikuwa mmoja wa wasimamizi wa kikundi cha kazi pamoja na Askofu Mkuu Nifon wa Targoviste.
Katika mkutano huo pia uliudhuriwa na mwakilishi wa Baraza la Kipapa kwa Kuhamasisha Umoja wa Kikristo, Katibu Askofu Brian Farrell na Andrzej Choromanski muhusika wa mahusiano ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc).Katika hotuba yake,Monsinyo Martin amesisitiza umuhimu wa kushirikishana imani kwa vizazi endelevu na wajibu wa Kanisa kuhusu jumuya za wahamiaji.
Nafasi kubwa ya mazungumzo katika meza ya mduara ilikuwa ni kutazama kwa upya mafanikio yaliyo patikana katika Makanisa kuhusiana na suala la uhamiaji na ujenzi wa amani. Kwa mtazamo huo wamesema kuwa, kuna ulazima wa kutoa jibu kama wakristo dhidi ya majanga makubwa yanayo wakabili watu hasa kulazimika kuhama katika hali ngumu sana.
Na Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |