2017-04-29 16:52:00

Afrika imefadhiliwa tangu zamani na wamisionari kutoka Ulaya!


Wajumbe kutoka katika Chama cha  Msaada wa Kanisa linalohitaji nchini Italia, wakiongozwa na Mkurugenzi wao Alessandro Monteduro mwishoni mwa wiki hii wamekutana na Kardinali na Kard Peter K.A.Turkson Rais wa Baraza la Kipapa kwa Huduma ya Maendeleo endelevu ya Binadamu katika mazungumzo kuhusu masuala mengi ya na zaidi juu ya ziara ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Misri. Baada ya mashambulizi ya hivi karibuni katika maadhimisho ya Jumapili ya Matawi mjini Cairo, Chama cha Msaada wa Kanisa linalohitaji limesaidia vijana 3.000 wa Misri kuweza kufanya  maandalizi yao na kufanikisha kukutana na Baba Mtakatifu katika Ziara yake ya kitume nchini Misiri kama muhujaji wa amani.

Kardinali Turkson katika mazungumzo yake na wajumbe hao pia  amelezea juu ya Rais wa Misri kutangaza maombolezo ya Kitaifa mara baada ya mashambulizi ya Kanisa la Kikoptiki, ya kwamba  ni jambo la ujasiri na  chanya, lakini pia ingekuwa vizuri zaidi, Rais kujihusisha katika mamlaka kuhusiana na suala la ujenzi na ukarabati wa makanisa ya Kikristo kwa kutoa ruhusa ya uwezekano wa kujenga sehemu za kufanya ibada takatifu. 
Kardinali amesema, ili kufikia mizizi ya matatizo hayo ni lazima kuhamasisha mazungumzo kati ya makundi yenye  mvutano mkali kati ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia. Kwasababu iwapo familia hizi mbili hazipatani na kuendelea na uadui kati yao itakuwa vigumu kweli kutatua matatizo hayo kwa maana hiyo kuna ulazima wa kutafuta njia ya kukuza majadiliano.

Mara nyingi Kiongozi wa Kiorthodox Tawadros II  amesema kuhusu uekumene wa damu,kwa maana ya kwamba, wakati magaidi wanatesa wakristo walio wachache,hawafanya utofauti,badala yake ni kinyume kwani utambuzi ni mmoja tu ambao ni Mkristo. Kwa maana hiyo kardinali Turkson amesema,nchini Misri kuna aina mbali mbali za madhehebu ya Kikristo,pamoja na tofauti hizo ni  lazima kuongelea Ukristo kama jumuiya moja bila utofauti.Katika nchi hiyo kumekuwa na mashahidi wa damu,na kwali ipo  damu ya  kiekumene kwa maana hiyo, anayo hofu kuwa siyo mwisho wa matukio hayo.

Chama cha Msaada wa Kanisa linalohitaji kimetumia zaidi rasilimali zake kwa msaada wa unjilishaji hata barani Afrika. Kwa namna ya pekee chama hicho kwa sasa kinaanda baadhi ya miradi kwa ajili ya bara,ni kwasababu gani kuendelea kusaidia Ukristo katika Afrika,Kardinali amesema kuwa, sehemu kubwa ya Afrika imeundwa kwa ufadhili wa wamisionari kutoka Ulaya.Ukifikiria ukosefu wa imani katika Ulaya,itakuwa huzuni makanisa ya Afrika kubaki yatima, kwa njia hiyo msaada lazima uwepo na msaada wa kifedha ni muhimu, unahitajika, lakini kwanza Ulaya yote lazima irudie kushuhudia imani ya Kikristo.

Amemalizia akisema pamoja na Chama cha Msaada wa Kanisa linalohitaji kusaidia miradi mingi katika bara la Afrika,lakini hata Baraza la Kipapa kwa Huduma ya Maendeleo endelevu ya Binadamu katika mpango wa Impact Investiment linajihusisha ili kuhakikisha upatikanaji wa fedha zinazo hitajika kwa ajili ya miundo mbinu ya mifumo ya uinjilishaji.

Na Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.