2017-04-28 15:29:00

UBELGIJI:Matumaini ya wazazi wa Afrika kupata watoto wao nchini humo!


Ni hadithi  ambayo inatengeza kurasa ya giza katika ukoloni wa nchi ya  Ubelgiji katika Afrika. Hayo ni maneno kutoka katika Baraza la Maaskofu wa Ubelgiji wakikimbuka mateso ya watoto wengi waliozaliwa na mama kutoka nchi ya  Congo, Rwanda , Burundi na baba mweupe wakati wa Ukoloni. Ujumbe unasema kuwa watoto hawa waliozaliwa walifikiriwa na mamlaka ya kikoloni , na pia hata jamii yenyewe ikiwemo hata  Kanisa ya  kuwa watoto ni tatizo kutokana na mahusiano ya nje ya ndoa.Ujumbe unasema, watoto walio wengi waliondolewa kwa mama za ona kupelekwa Ubelgiji kwenye vituo vya watoto yatima au kwenye mashule ya bweni yaliyo endeshwa daima na watawa wa  kike na kiume huko Ubelgiji, mbali na familia, ndugu zao, hata katika mizizi yao ya kiafrika. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa machungu  kuanzia mwaka 1959, ambapo pia wengi wa watoto walipewa dhamana ya kutunzwa katika familia nyingine za Ubalgiji.

Maaskofu wa Ubelgiji katika ujumbe kupitia gazeti la Sir wanaomba msamaha na kuonesha nia yao kamili ya kutaka   kufungua nyaraka zake na kwamba ni matumaini yao watu wanaweza kupata taarifa ambazo ziawezeshe kupata watoto wao walio pelekwa Ubelgiji nyakati hizo.
Aidha Maaskofu pia wanawatoa wito kwa wote ambao wanaweza kuwa na nyaraka au hati za kihistoria ambazni ni nyenzi ynye thamani kwa ajili ya kuwasaidia upatikanaji wa watoto hao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.