2017-04-27 15:44:00

Waaamini wapya miatatu kupata ubatizo katika Jumuiya ya Cambodia


Katika Sikukuu ya Pasaka, karibu waamini  miatatu wakiwa karibu wote ni vijana kutoka katoka dhehebu la Kibudhisti wamepokea Sakaramenti ya Ubatizo kuwafanya wawe moja kwa moja sehemu ya  jumuiya ya kikristo kwenye Jumuiya ndogo Katoliki nchni Cambodia; ni kipindi cha mchipuo mpya wa kiroho katika eneo hilo. Hilo ni  tukio la pili kuzingatia kwamba Kanisa mahalia la Cambodia  idadi ya waamini ni 23,000 tu ambao ni asilimio 0,2 ya watu wote wa nchi, kutokana kwamba idadi kubwa ya wakazi ni dhehebu la kibudhisiti, ambao hadi sasa ni milioni 16,000,000.

Pamoja hayo historia ya nchi ya mambo ya kale ni kubwa  kwa  muhongo wa XVI ma pia imepata kuteseka na vita na  mauaji  kwa miaka ya 70  kuanzia 1979-1989 chini ya utawala wa kivietnam.Inatosha kuona kwamba kati ya waamini 65,000 walio kuwapo kwenye miaka ya 1970 na baada ya miaka 20 wamebaki kiasi kidogo tu.Kwa njia hiyo  ubatizo wa watu mia tatu  ni ishara ya maisha mapya na matumaini ya Kanisa Katoliki katika nchi ya Cambodia.

Pamoja na hayo yote, kwa kawaida Sikukuu ya Pasaka imekuwa muhimu katika historia ya jumuiya wa wakristo wa Cambodia.Hayo yalisemwa na Padre Vincent Senechal  mmisionari wa chama cha utume wa nje kutoka Paris Ufaransa ambaye yuko Cambodia kwa miaka 15 kama mmisionari. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.