2017-04-27 16:56:00

Pokea moto wa Roho Mtakatifu uwafungulie mikono watu wengine!


Tarehe 25 Aprili 2017 umehitimisha muunganiko wa pamoja wa Jumuiya wa wakarisimatiki ulio anza tarehe 22 Aprili katika Mji wa Rimini nchni Italia. Watu zaidi ya 15,000 wameweza kuudhuria tukio hili la kitaifa na kimataifa lifanyikalo kila mwaka. Kauli mbiu iliyo ongoza makutano yao ya kiroho kwa mwaka huu ni kutoka katika Kitabu cha Isaya isemayo; “ imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwasababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia imbeni kwa furaha…(Is 44,23). Makutano hayo yamekuwa pia na fursa ya kusheherekea kwa pamoja miaka 50 tangu kuanza kwa chama hiki cha Kikarismatiki ulimwenguni.

Ushuhuda kutoka kwa watu mbalimbali ulitolewa wakati sala nyimbo zikiwasindikiza katika makutano ya yao; aidha kuudhuriwa na  wageni  kutoka pande nyingi za dunia katika tukio makusanyiko ya 40.Misa ya kufunga makutano hayo iliadhimishwa na Kardinal Angelo Bagnasco, ambaye ni Rais wa Baraza la maaskofu nchini Italia, pia Rais wa Baraza la maaskofu wa Ulaya. Katika mahubiri yake amesema ni maadhimish0 ya mwaka wa neema ambayo ni kuwakumbusha uwajibikaji kwa Kanisa katika Ulimwengu. Aidha Kardinali Bagnasco amesema, anayo furaha ya kuendelea kushangilia nao kwasababu Bwana anaendelea kutenda maajabu katika historia, anajionesha kwa namna ya pekee ya kumtolea sifa na utukufu wake. Kwa njia ya kumbukumbu ya kuzaliwa chama cha kitume cha  kikarismatiki, wanaondoke kwenye makutano hayo wakiwa wapya ili kumtumikia Mungu na watu. Hiyo ni kwasababu kadiri mikono  inavyo jifungulia moto wa Roho Mtakatifu, ndivyo mikono inapanuka zaidi kuhudumia wengi wenye matatizo ya kiroho na kimwili. Miujiza ya roho wa Bwana  ambayo inafanya kazi kwa njia ya unyenyekevu, upole wa kibinadamu ni muungano katika imani ambayo uzaa umoja wa mioyo na kuendelea kuzaliwa mwili ya Yesu katika historia ya Kanisa. 

Naye Mh. Antonio Tajani Rais wa Bunge la Ulaya , wakati wa hotuba yake amesema wakati Ulaya inapitia kipindi kigumu lakini suluhisho siyo kujifunga ndani yake binafsi, dawa ya kuponya Ulaya ni kufungua mioyo inayo ungana na ambayo  msingi wake ni uhuru. Ameongeza kusema kuwa mizizi ya Kikristo haitazami waamini wake  peke yake kwa sababu inawaunganisha watu wote wanao ishi Ulaya nzima. Hiyo ni kwasababu kwa kutazama  bendera ya Ulaya ina nyota 12, inafana na taji la mama maria mwenye taji la nyota 12, Kitambaa cha bendera ya Ulaya kina rangi ya blu, amabayo ni vazi la mama Maria.Kwa misingi hiyo watu wengi waliofika katika makutano ya kiroho wamewakilisha uzalendo wa Ulaya kwa kina, kwasababu hiyo ndiyo historia ya Ulaya. Aidha amesema kuunganika wote  kitaifa na kimataifa ni kuonesha kama roho mtakatifu anavyoendelea kuwa hai ndani ya nchi za Ulaya kwasababau waamini wake wanao msingi mkuu wa  thamani na maadili katika mawazo ya uzalendo wa Ulaya. 

Naye Rais wa Chama cha Kikarismatiki  Salvatore Martines amesema nguvu za kiroho  zinaanza kupungua japokuwa roho hizo zinaweza kurudia tena upya  kutoka ndani ya noyo wa kila mt una wala siyo mahali pengine. Ameyasema hayo akitafakari juu ya barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Timoteo isemayo “tunza salama yale uliyo kabidhiwa” 1Tm 6,20a).Na kwamba  Jubilei ya Wakarismatiki inawaalika  kufanya hivyo kurudi katika mambo yaliyo muhimu. Aidha kusema kuwa huo ni wito pia alio utoa Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka 2002 wakati wa kukabidhiwa katiba ya Kikaristimatiki ya kwamba “endeleeni kupenda  na kufanya Roho Mtakatifu apendwe. Iwapo kuna kipeo che maisha ya kiroho, lakini hakuna kupeo charoho Mtakatifu maana Roho Mtakatifu ni yule yule anaendelea kutenda kazi yake  wakati wote hadi miisho ya dunia.Aidha hakuna kipeo cha Roho Mtakatitu kwasababu imejionesha wazi  katika makutano haya ya mwaka huu, jinsi gani roho wa Bwana anaendelea kutenda maajabu yake katika jamii, vilevile matunda yake yanaonekana katika maisha ya watu.

Anaye sali anayo lugha mpya; anao uwezo wa kusema ukweli;mwenye uwezo wa  kusema maneno ya dhati ya kibinadamu, hawezi kamwe kunyamaza mbele ya mambo maovu na yasiyo stahili. Kwa njia hiyo inabidi kuanza upya kujitafakari kiroho na kujifunza upya kwa ajili ya kuelemish dunia hii, hasa katika kizazi kipya na familia ili wapate kutembea kadiri ya Roho Mtakatifu,pia kuwa tayari kusaidia au kufungua mlango kwa kila anayebisha hodi. Nchi yetu na bara la Ulaya kwa ujumla wanahitaji mioyo safi hasa moyo mpya wa kiinjili.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.