2017-04-27 16:43:00

Argentina:Karama ya Kanisa Katoliki ni kupokea wote waliotengwa!


Inabidi kupinga vizuizi vinavyozuia kukaribisha, ndiyo nia kubwa ya ujumbe wa Baraza la maaskofu wa Argentina wakipinga wazo la kubadilisha sheria iliyotolewa katika nchi yao kuhusu wahamiaji. Maaskofu wa Argentina wamesema kwamba hakuna ruhusa katika hali yoyote kwenye ibara ya 8 ya katiba ya nchi hiyo inayokataa au kuzuia haki ya afya, huduma za kijamii au hutoaji  wa huduma ya afya kwa wageni wote wanaohitaji msaada na  bila kujali hali zao za wanaohama. Ujumbe huo wa Maaskofu uliotolewa hivi karibuni katika vyombo vya habari  unasema; nchi ya Argentina daima imekaribisha ndugu na watoto wa wahamiaji kutoka pande zote za dunia na zaidi katika miaka ya hivi karibuni, wahamiaji  kutoka nchi zinazopaka na Amerika ya kusini.

Maaskofu hao wamesema ni lazima kuendelea  kukuza maendeleo ya utamaduni wa heshima, mshikamano, na utambulisho kwa Kanisa Katoliki  ambao ndiyo unatoa utaofauti kwani. Hiyo ni kwasababu utambulisho na kupokea ndiyo karama za Kanisa kwa ajili kuwatambua maskini, waliotengwa katika jamii na wakati mwingine wageni ndiyo wanatuhumiwa kuhusika na majukumu ya maovu katika jamii ya Agentina.
Kwa mtazamo huo  Maaskofu wa Argentina  wamesema hakuna haja ya kufanya mabadiliko ya sheria ya 25871, wakikumbuka ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya Wahamiaji duniani kwa mwaka 2016 usemao Kanisa linaambatana na wale wote wanaojikita katika jitihada zao kulinda na kutetea haki ya kila mtu ili aweze kuishi kwa adhi ya kiutu.

Na Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.