2017-04-25 16:13:00

Askofu Mkuu Auza: Watu asilia wanahitaji kutambuliwa na kuheshimiwa


Katika Jukwa la Kimataifa kuhusu watu wa asili linaloendelea  huko Makao Makuu ya Umoja wa mataifa New York,tarehe 24 Aprili 2017 Askofu Mkuu Bernardito Auza mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa, ametoa hotuba yake katika kikao cha kumi nasita kwenye mjadala wa maadhimisho ya miaka kumi ya tangu kuweka azimio la Umoja wa mataifawenye kauli mbiu “Haki za watu  asili;hatua zichukuliwe kutekeleza azimio.
Askofu Mkuu Auza  amesema mwaka huu una uzito mkubwa kutokana na tukio la kuadhimisha miaka kumi ya kupitishwa azimio katika Umoja wa Mataifa kuhusu  Haki za watu wa kiasili.Ni fursa kukaribisha  wadau wote ili kuchukua hatua  ya mafanikio ya Azimio na kutathmini changamoto iliyobaki.

Miezi miwili iliyopita, Baba Mtakatifu Francisko  Francisko amekutana mjini Vatican na makundi ya wawakilishi wa watu asilia kutoka sehemu mbali mbali za dunia ambao walijadili masuala mawili ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu asilia,na kuhusu haki ya maendeleo na haki ya kutambuliwa asilia. Katika matukio mbalimbali, hasa wakati wa ziara yake ya Amerika ya Kusini,Baba Mtakatifu  ameelezea nia yake ya kwamba yeye ni msemaji kwa kina  kwa ajili ya watu asilia,na kutetea heshima ya watu kiasili ili kuongeza uelewa mkubwa wa umma kuhusu ukweli kwamba watu asilia wanaendelea kuteseka kwa ajili ya utambulisho wao na hata katika uwepo wake.Askofu Mkuu  Auza amesema;Vatican inaamini kwamba,kukuza maendeleo ya kweli ya watu asilia, lazima  kuoanisha haki yao ya maendeleo ,ya kijamii na kiutamaduni pamoja maendeleo ya kiuchumi.

Hii ni wazi hasa wakati wa kupanga shughuli za kiuchumi ambazo zinaweza kuathiri tamaduni za watu wa kiasili kutokana na uhusiano wa mababu zao, kwa dunia na hata  asili.Jambo hilo ni muhimu kwasababu kama siyo  kusimamiwa, kuheshimiana na kujali kutokana na haki zao inaweza kusababisha mgongano na mzozo wa kimaslahi. Matatizo haya yanaweza kushughulikiwa kwa njia tatu muhim wa  kuweka kipaumbelea katika kuazisha taarifa zinazo waathiri, kuanzishwa mipango ya serikali na hata  miradi ya sekta binafsi. Katika suala hili haki ya idhini na taarifa ziakikishe zinachukua hatua  mbele zaidi kama inavyojieleza katika ibara ya 32 ya Azimo la Haki za binadamu wa kiasili. Ibara hiyo inasema; Watu wa kiasili wana haki ya kuamua na kuendeleza vipaumbele na mikakati kwa ajili ya maendeleo au matumizi ya ardhi yao au maeneo na rasilimali nyingine. Mataifa  yashauriane  kushirikiana kwa nia njema na watu wa kiasili wanaohusika kupiti wawakilishi wao ili wao wenyewe wato ridhaa kabla ya idhini ya mradi wowote unao athiri ardhi yao au maeneo na rasilimali nyingine, hasa katika uhusiano na maendeleo,au matumizi ya madini, maji au rasilimali nyingine.Nchi zitoe  mfumo bora wa haki na usawa  wa kurekebisha na kuelekeza shughuli kama hizi na hatua mwafaka zichukuliwe kupunguza migogoro ya  mazingira, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni au athari za roho mbaya ..

Jamii za kiasili siyo tu mojawapo ya watu wachache  miongoni mwa wengine, lakini  inapaswa kuwa mojawapo ya msingi wa washiriki wa mazungumzo wakati wa miradi mikubwa ya ardhi ya mababu zao iliyo athiriwa.Kama Baba Mtaktifu Francisko alivyo bainisha kuhusu jumuiya hizi za asili kwamba ardhi sio bidhaa bali ni zawadi kutoka kwa Mungu na kutoka mababu zao ambao waliishi huku, wao ni nafasi ya utakatifu na ambao wanahitaji kushirikiana katika kudumisha utambulisho wao na maadili. Askofu Mkuu Auza amesema  kwa hiyo, wao wanatoa uduma bora yao wenyewe wakiwa katika ardhi yao. Hata hivyo,katika maeneo mbalimbali ya dunia,shinikizo ni kubwa kutokana na watu wanchi zao bila ridhaa kutoka kwa watu wa asili ambapo hujenga nyumba kwa ajili ya miradi ya kilimo au madini ambayo  hufanywa bila kujali haja ya kulinda asili na kuhifadhi mila na tamaduni za watu wa kiasili ambao wameishi nchi hizo tangu nyakati za kale.

Halikadhalika Askofu mkuu Auza amesema Vatican inakaribisha sera hizo za kitaifa ambazo zinahitaji mashaurino na ridhaa ya watu wa asili  kabla ya miradi ya maendeleo katika ardhi ya mababu zao ambazo zimepitishwa na kutekelezwa. Zaidi ya hayo, kuna lazima wa kuwa na  maendeleo ya miongozo na miradi ambayo uheshimu utambulisho wa kiasili. Hii ina maana kutambua kwamba jamuiya  hizi ni sehemu ya idadi ya watu, ambao ushiriki wao kikamilifu, hivyo ni lazima kukuzwa katika mioyo ya ngazi ya kimataifa katika kuzuia kubaguliwa na zaidi kukuza ushirikiano wao kikamilifu juu ya jamii hiyo. Ukosefu wa heshima na utambulisho wa asili ni ukiukwaji wa roho na makubaliano ya agenda ya  2030 ya Maendeleo Endelevu, ambayo haitaki mtu yoyote kuanchwa nyuma. Kuheshimu utambulisho wa asili pia neema ya huduma kwa ajili ya nyumba yetu ya pamoja. Ki ukweli mila na tamaduni za kiasili zinaonesha mwingiliano muhimu na pia binadamu kutegemena ambapo hasa huduma ya nchi katika kutunza ardhi yetu ambayo ni mama.

Mbinu zao ni hali ya kujenga ndani yao hisia kubwa ya uwajibikaji , na nguvu yao husababisha hali ya umojo, utayari kusadia wengine, roho ya ubunifu na ya kupenda nchi yao sana. Pia wanahisia ya mshikamano kati ya vizazi,kwasababu wao kwa dhati wanatunza mazingira kwa ajili ya vizazi endelevu.
Thamani hizi zinazo onekana katika mila na tamaduni za kiasili zinastahili kuwa kama mifano kwa ajili ya watu wote kwa kuhifadhi mazingira katika kuzuia uharibifu zaidi. Kwa hali hiyo,watu asilia wanastahili siyo tu heshima yetu bali pia shukrani zetu na msaada.

Na Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.