2017-04-24 08:39:00

Waamini Katoliki kuadhimisha miaka 600 ya Ukuu wa Kanisa Poland


Baba Makatifu ametuma barua yake kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Gniezno nchini Poland kwa ajili ya kuwatakia matashi mema wakati Jimbo Kuu hilo linafanya kumbukumbu ya miaka 600 tangu ipewa ukuu wa Kanisa hilo. Katika barua hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesema, ni mihongo sita imepita tangu Mtaguso wa Costance ufanyike.Ikumbukwe kuwa  ni mtaguso wa XVI ulio julikana kuwa ni wa Kiekumeni wa Kanisa katoliki ,huko Costance ulioitishwa kwa matashi ya Mfalme wa Warumi Sigsmund wa wakati ule ili kukomesha mafarakano ya nchi za Mashariki. 

Askofu Mkuu wa Jimbo la Gniezno Mikołaj Trąba aliteuliwa  kuwa mkuu wa Kanisa la Uholanzi. Uchaguzi huo siyo kwamba haukuwa na sababu, kwani ilitokana na kupata heshima ya uwajibikaji wa upendo wa Jumuiya ya Kanisa ya Uholanzi hasa katika mji wa Gniezno. Hata hivyo pia kuna msingi wa kihistoria wa Kanisa  katika ardhi hiyo kutokana na  shughuli za kimisionari kwa njia ya  ushuhuda  wa mfiadini Mtakatifu Aldabert. Halikadhalika hapo kuna masalia ya Baba Mtakatifu Silvester. Hivyo Baba Matakatifu anesena,hiyo pia ni kwasababu miaka ya 1000 alikutana na mfalme Otto III wa Ujerumani pia mfalme jasiri  wa Poland  Boleslaw .Baadaye Gniezno ukawa mji mkuu wa kwanza wa kituo cha mji mkuu wa Kanisa mahalia.

Mwaka 1417 Kanisa kuu la Poland likawekwa wakfu na kutambuliwa kwa kupewa nafasi ya pekee iliyofanywa na historia ya mji wa  Gniezano katika akili na mioyo ya watu wa Poland. Hata katika mihongo iliyofuata, kwenye kipindi kigumu cha changamoto, watu wa uholanzi na kwa namna ya pekee wa mji wa Gnizno walibaki kidete wakitafuta uhuru,wakiongozwa na nguvu na motisha wa  kujenga  pamoja makuzi ya kiroho. Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili amekuwa akiwakumbuka wazalendo wake mara kwa mara  hasa urithi mkubwa wa Mtakatifu Adalbert,na kwa miaka ya karibuni aliweza kusisitiza juu ya kurithi mantiki ya umoja wa Ulaya.

Baba Mtakatifu Francisko aidha ameandika kuwa,alikumbusha kuwa msingi wa mji wa Gniezno ni kama roho ya umoja wa Ulaya na Ukatoliki katika Injili inayo fumbatwa na binadamu katika kuchangia maendeleo ya kihistoria ya watu na Taifa. (Yohane Paulo II(/03/06/1997). Leo hii Gnezno na Kanisa zima la Poland linapo adhimisha miaka 600 ya ukuu wa Poland ni lazima kuangalia maisha endelevu na kuomba Mungu ili kuweza kuwa mashahidi wa kweli wa Mtakatifu Adalbert,pia iwe chanzo  hai kwenu cha  uongozi katika utume wa uinjilishaji kwa vizazi endelevu vya kumfuata Kristo. Zaidi ya hayo , maadhimisho hayo yawe ndiyo mwanzo wa mwaka, kuwapa fursa ya  mang’amuzi ; na changamoto iwafanye mfike mkiwa na wajibu wa kutangaza ujumbe wa Injili katika dunia ya kisasa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.