2017-04-24 14:43:00

Mtandao wa Kanisa Katoliki Amerika ya Kusini kusaidia watu asili!


Tangu Jumamosi 22 Hadi Tarehe Mosi Mei 2017 watu asili kutoka misitu ya  Amazoni Mosete nchini (Bolivia), Manduruku Yanomami (Brazil), na Kukama (Peru) wataudhuria  Jukwaa la Kudumu kuhusu masuala ya watu wa asili kwenye Umoja wa Mataifa katika mkutano unao endelea.Mpango wa Mtandao wa Kanisa kuhusu watu asilia, ni sehemu ya Kampeni ya muda mrefu kwa ajili ya uendelezaji wa utetezi  wa haki za binadamu. Chombo hiki cha Kanisa kama taarifa inavyotolewa kinashiriki kwa sasa katika kesi kumi kumi na tatu za nchi  Amerika ya Kusini ambazo ni Colombia, Ecuador, Perú, Bolivia, Brasile.Kwa mujibu wa REPAM, kile kinacho jitokeza kwa sasa katika  maeneo ya watu wa asili wa nchi mbalimbali duniani, ni matokeo ya unyonyaji wa kukithiri katika sera ya mali asilia na  zaidi hasa katika ukanda wa misitu ya Amazon kutoa faida kwa makundi binafsi,ambapo husababisha ukosefu wa haki, uharibifu wa binadamu na mazingira.

Aidha taarifa zinasema kuwa, mwezi ulio pita, Repam walitoa wazo kwa katika Kamati ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu kuzingatia uwezekano kwa njia ya mwandishi juu ya haki za watu asili ili kutayarisha na kuchapisha ripoti.Kwa sasa wawakilishi hao wa asili wakiongozwa na Askofu Mkuu Gustavo Rodríguez Vega  wa Jimbo Kuu la Yucatan ambaye ni Rais wa Baraza la haki na amani wa Baraza la Maaskofu wa Amerika ya Kusini (Celam) amesema kuwa, uwepo wa viongozi wa watu mbalimbali wa kiasili ni kuweza kupata fursa ya kueleza changamoto wanazo kabiliana nazo katika maeneo yao. Na pia wataendelea kufanya hivyo hata katika matukio mbalimbali yatakayo fanyika wakati wa vikao vidogvidogo vya Jukwaa hilo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.