Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Tarehe 22 Aprili 2017 Padre Luis Ormieres kutangazwa mwenyeheri!

Luis Antoine Ormieres atatangazwa mwenyeheri huko Oviedo Hispania tarehe 22 Aprile 2017.Padre mwenye huruma na upendo, mnyenyekevu na mpole - RV

21/04/2017 16:22

Kardinali Angelo Amato , Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuwatangaza watakatifu, amefanya mahojiano ya Mwandishi wa  Radio Vatican, kuelezea maisha ya  Louis Antoine Ormières  ambaye atatangazwa  mwenyeheri huko Oviedo Hispania  tarehe 22 Aprile 2017.
Louis Antoine Ormières alizaliwa tarehe 14 Julai 1809 huko Quillan mji mmoja kusini mwa Ufaransa, unaopakana na nchi ya  Hispania. Alipata daraja la upadre mwaka 1833 , na kujikita katika shughuli za kitume kwa ngazi ya  elimu na kufundisha vijana. Mwaka 1839 akaanzisha Shirika la kike kwa jina la Malaika Walinzi, ambapo jina linejieleza karama ya shirika hilo. Alikufa katika hali ya utakatifu tarehe 16 Januari 1890 baada ya kuwa ameanzisha mashule 87 huko Ufaransa na Hispania.

Kuhusiana na utakatifu wake, Mwenye heri alikuwa mwelewa na mwalimu wa kuzaliwa , alikuwa amejaa karama za kikristo, imani , matumaini na upendo. Alikuwa amejaa ubinadamu wa huruma na shukrani, vilevile mtulivu na rafiki. Kutokana na kuwa na huruma ya Mungu ilimfanya kuwapenda walio wadogo, wadhaifu , masikini, na wasio kuwa na hatia. Yeye alikuwa anaishi maisha na kufuata mafundisho ya Mtakatifu Paulo akisema “ Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu. (Wakol 3,11-12)
Aidha Kardinali Amato ameelezea baadhi ya mifano halisi ya matendo ya upendo aliyofanya kuonesha kuwa ni mtakatifu kweli kwani amesema, zipo shuhuda nyingi zinaonesha upendo wake kwa mfano wa kutetea mwanaume mmoja aliyekuwa ameonewa bia hatia, Alikuwa akitoa makaribisho kwa wakimbizi kutoka Hispania, alimwombea kijana aliyekuwa anapaswa kutunza familia yake mara  baada ya baba yake kufa msaada kutoka kwa watu watajiri wamsaidie. Alijikita kumtafutia msaada masikini mama mmoja na watoto wake wawili .Alimtia moyo wa kibaba mtawa mmoja aliyekuwa mgonjwa sana.

Kwa mambo haya kadhaa na mengine  yanaonesha kuwa alikuwa mtu wa Mungu na mtakatifu kweli. Hata katika kitabu cha maisha yake , kinaeleza hali halisi zaidi . Alikuwa ni mkarimu, kuwasaidia wagonjwa ambapo Askofu wake alimwita kuwa ni shahidi wa upendo. Alikuwa akiwaalika watoto wake kiroho waige mfano wake na kuwasaidia wengine kufanya hiyo safari ya kuiga. Alikuwa akiwambia kwamba watoto mnapaswa kuweka mabawa na kuwa jasiri.
Amemalizia kwa kusema ni kwanini atangazwe kuwa mwenye heri,na kusema,    karama ni pete ya mkofu wa dhahabu ya utakatifu. Anaye bahatika kuwa nayo anapata hata nyingine zaidi. Kwa njia hiyo ni dhahiri kutokana na imani kubwa aliyokuwa kuwa nayo , mifano yake, tabia yake ya uvumilivu, upole , na unyenyekevu. Tunatambua ya kwamba unyenyekevu ndiyo msingi wa kila karama, kwa njia hiyo Padre  Ormières alikuwa na unyenyekevu wa aina yake.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

21/04/2017 16:22