2017-04-21 13:24:00

Huruma ya Mungu kuunganisha Mt. Yohane Paulo II na Papa Francisko


Jumapili 23 Aprili 2017 Kanisa katoliki linasheherekea  Sikukuu ya Huruma ya Mungu.Ni tukio lililo anzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka 2000 wakati wa tukio la kumtangaza Mtakatifu Faustina Kowalska , mtume wa Huruma ya Mungu.Sikukuu inafungamana  na Ufufuko wa Bwana ,ambayo kwa hakika Mtakatifu Yohane Paulo II alipendelea ifanyike Jumapili ya kwanza baada ya Pasaka.Ili kupata habari zaidi mwandishi wa habari wa Radio Vatican alimuhoji kwa njia ya simu mtoa hoja ya mchakato wa kutangazwa Mtakatifu Yohane Paulo II Monsinyo Slawomir Oder  juu ulinganifu uliopo  kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Mtakatifu Yohane II kwa dhati juu ya huruma.

Monsinyo Oder amesema,huwezi kufikiria huruma ya Mungu bila uwepo wa ufufuko wa Bwana,kwasababu ufufuko wa Bwana yaani Pasaka ya Bwana ndiyo mwisho wa utambulisho wa huruma ya Mungu,ndiyo ufunguo wa maisha,na maisha ya milele.Ni zawadi ya Mungu anayo itoa kwa binadamu kwa njia ya Kristo.Yesu alikuja duniani kwasababu hiyo ya kuonesha uso wa huruma ya Mungu.Huruma ya Mungu ni mada muhimu inayo waunganisha Mtakatifu Yohane Paulo  II na Baba Mtakatifu Francisko, na wakati huo ni mwendelezo wa roho ya utawala wa  mapapa hawa  wawili .Wote wawili wanatoka katika hali iliyokuwa na mageuzi kijamii kutokana na matatizo ya kihistoria. Kwa dhati ni suala nyeti la kibinadamu kwani ukweli wa kihistoria ya mapapa hawa wawili , kwa kuweka umakini wa hadhi ya mtu na masuala ya umaskini,kwa wale wanao subiri utimilifu habari njema ya Injili na kwamba wanataka kufanya wawe karibu pamoja katika kukabiliana na tatizo la huruma ya Mungu.

Huruma haiondoi haki  bali ni kuikuza zaidi kama vile Mtakatifu Yohane Paulo II katika waraka (Dives in Misericordia) wake aliuliza je inatosha haki peke yake? .Yeye  akiwa na maana ya kujibu kwamba Kanisa linaitwa kutangaza huruma yake  ambayo muundo wake ni juu ya haki na upendo, kwa namna hiyo kuna uhusiano mkubwa  wa mapapa hawa amesisitiza .Hata hivyo wakati mwingine wengi hawelewi  vema kwa kufikiria huruma  ni wema tu kirahisi wa kutoa kwa njia hiyo Monsinyo anafafanua zaidi akisema ,katika mtazamo wa mihongo iliyopita tunaweza kusema wazi nini maana ya haki ya binadamu bila kuwa na Mungu, kwa maana bila kuwa na Mungu ilionekana hali ya kulazimika kukana ubinadamu,kuingi katika mfumo wa utumwa , na kunyimwa hadhi ya binadamu.Kwa njia hiyo hakuna utata kati ya haki na huruma, na wala siyo kukubali tu au suala la kuongea juu ya huruma tu.

Jambo muhimu ni lazima kukumbuka daima kuwa  hali yoyote ya ufunuo wa huruma ya Mungu ujikita katika ulazima kimaadili, mtu wa dini hupokea fumbo na pia hupata  kuongoka kwa njia ya fumbo hili. Kwa maana hiyo huruma  ni kukubali kuipokea mara kwa mara na kufanya mchakato wa kuelewa moyo wa mtu.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.