2017-04-21 12:55:00

Baba Mtakatifu katika Mkesha wa sala kwa Mashahidi wa Karne XX


Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inajiandaa kwa furaha kubwa kumpokea Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Bartolomro,kwenye mkesha wa Sala kwa ajili ya Mashahidi wapya wa Karne ya ishirini. Kanisa hilo liliwekwa  kuwa  msimizi wa kumbukumbu ya mashahidi wapya mwaka 1999 kwa utashi wa  Mtakatifu Yohane Paulo II. Liturujia ya Neno itaanza saa 11 Jioni masaa ya Ulaya  Jumamosi 23 Aprili 2017.Katika maadhimisho hayo,kutakuwepo na hotuba kutoka kwa ndugu na marafiki watatu kati ya mashahuda wa imani,ambao  masalia yao yako ndani ya  Kanisa kuu la Mtakatifu Bartolomeo.

Baada ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko, atatoa heshima yake kwenye vikanisa 6 vidogo pembeni ya Kanisa Kuu vinayo tunza masalia ya mashahidi wa Ulaya, Afrika, Marekani na Asia, wa ukomunisti na wa kibaguzi.Aidha itafuata tendo la kuasha mishumaa kadhaa ambayo itasindikizwa kwa naombi ya sala, kwa ajili ya kukumbuka mashahidi wa imani walio kufa kwenye  karne ya XX hadi leo hii, hawa ni  wakristo na waathirika wa makanisa mengine wakati wa vita vya kwanza vya dunia wakiwa ni mashahidi wa imani na mazungumzo.Watawaombea mapadre,watawa na wamisionari wote walio uwawa  wakitoa maisha yao kwa ajili ya Injili duniani.Baada ya maombi hayo Baba Mtakatifu atakutana na kikundi cha wakimbizi waliofika kwa njia ya msaada wa kibinadamu, wakiwemo wanawake waathirika wa biashara ya binadamu na watoto wasio kuwa na msindikizaji, katika mojawapo ya ukumbi wa Kanisa Kuu .

Historia ya mashahidi  wa Karne ya XX na XXI ilipatika kutokana na kwamba,iIlikuwa mwaka 1999 Mtakatifu Yohane Paulo II alipo amua wakati wa maandalizi kwa ajili ya Jubilei ya mwaka 2000 kuanzisha tume ya Mashahidi wapya, ambayo ilikuwa na wajibu wa kuchunguza juu ya mashahidi wa kikristo wa karne ya XX. Tume hiyo ilikuwa na mratibu Andrea Ricardi Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio; ilifanya kazi kwa miaka miwili katika majengo ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Bartolomeo,kwa kukusanya karibu ripoti 12,000 za makala za mashahidi wa imani kutoka katika majimbo yote duniani kote.

Miongoni mwa matunda ya kazi hii, kulikuwa na maombi ya kiekumeni yaliyofanyika katika Colosseo Roma akiwepo Mtakatifu Yohane Paulo II pia wawakilishi wa kila Kanisa kuu ya Kikristo. Wakati wa tukio hilo walisistiza ni kwa jinsi gani bado kuna idadi kubwa ya wakristo walio uwawa na kuteswa katika karne ya Ishirini ambao bado kuna haja ya kuchunguzwa urithi wao na  kushirikishana jumuiya zote za kikristo  Baada ya Jubilei ya miaka 2000 ya Ukristo, Mtakatifu Yohane Paulo II akapendelea kufanya kumbukumbu ya mashahidi wa imani wa karne hizo iweze kuwa jambo la kuonekana katika Kanisa Kuu ka Mtakatifu Bartolomeo.

Oktoba 2002 katika maadhimisho ya kiekumene kwa uwepo wa Kardinali Ruini, George Kasper, Patriaki wa Kiorthodox Teoctist,waliweka Picha kubwa katika Altare Kuu  inayowakilisha Mashahidi wa Karne ya ishirini. Picha hiyo imechorwa kutokana na tafsiri ya somo la ufunuo, kwa njia ya matukio ya mashahidi  iliyotambuliwa na kazi ya tume hiyo .Baadhi ya kumbukumbu za mashahidi wengine zinapatika katika vikanisa vidogovidogo vilivyomo pembeni ya kanisa vikionesha hali ya kihisoria ya mashahidi hao. Mahujaji wengi wanafika katika Kanisa hili kuu kwa ajili ya kutoa heshima ya mashahidi wa karne ya ishirini.

Hata Baba Mtakatifu Benedikto XVI alitembelea tarehe 7 Aprili 2008, na kutoa ujumbe kuwa; hija katika kumbukumbu ya mashahidi wa karne ya XX; kwa watu wengi walio mwaga damu yao kwa ajili ya Bwana, ni kuonesha kuwa, kufufuka kwa Bwana ni kuangaza ushuhuda wao na kufanya tutambue maana ya kuwa shahidi. Ni nguvu ya upendo bila kuwa na silaha ya kujilinda ,lakini yenye ushindi ambao tunauona wazi.

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.