2017-04-20 16:07:00

Watoto wa Fatima: Francis na Yacinta kutangazwa watakatifu 13 Mei!


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Makardinali katika Mkutano mdogo Vatican na kuruhusu kutangazwa watakatifu watoto wawili wa Fatima kuwa watakatifu tarehe 13 Mei 2017  ambao ni Mwenye heri  Francisko Marto, aliyezaliwa 11 Juni 1908 na kifo chake kikatokea hapo 4 Aprili 1919 na Mwenyeheri Yacinta Marto, aliyezaliwa 11 Machi 1910 na kifo chake  20 Februari  1920, hawa watoto ni ndugu wawili wa Fatima.
Wengine watatangazwa watakatifu tarehe 15 Oktoba 2017  ambao ni Angelo da Acri Padri wa Shirika la ndugu wadogo Wakapuchini aliyezaliwa Oktoba 1669 na kifo chake 30 Oktoba 1739. Faustino Míguez, padre wa Shirika la Scolopi na mwanzilishi wa Shirika la Calasanziano wa watawa wa kike Mchungaji mwema;
Mwenye heri Andrea de Soveral na Ambrogio Francesco Ferro,mapadre wa Jimbo na Matteo Moreira, mlei na wanzake 27 mashahidi waliouwawa kwa ajili ya kutetea imani yao nchini Brazil tarehe 16 Julai 1645 na tarehe 3 Oktoba 1645. Na mwisho Cristoforo, Antonio na  Giovanni, vijana mashahidi walio uwawa kwa ajili ya kutetea imani yao nchini Mexco mwaka 1529.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.