2017-04-19 15:54:00

Paulo alikuwa mtesi wa Kanisa akageuka kuwa mtangazaji wa habari njema


“Sasa ndugu, napenda kuwakumbusha ile Habari Njema niliyowahubirieni nanyi mkaipokea na kusimama imara ndani yake. Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure. Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa; kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili.(1Kor 15,1-5). Tunakutanika kwa pamoja leo hii katika mwanga wa Pasaka ambao tumeadhimisha na tunaendelea kuadhimisha kwenye Liturujia. Kwa njia hiyo katika safari yetu ya Katekesi kuhusu matumaini ya Kikristo, napendelea kutafakari  kwenu juu ya Kristo mfufuka ambaye ni tumaini letu , kama alivyo mtambulisha Mtakatifu Paulo katika Barua ya kwanza ya wakorinto sura ya 15. Hiyo ni tukio, allikufa, akazikwa,akafufuka na kutokea. Maana yake Yesu anaishi na ndiyo kiini cha ujumbe wa kikristo.

Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo katika Katekesi yake ya kila Jumatano, ikiwa ni tarehe 19 Aprili 2017 wakati wakristo  bado wanaishi na kushherekea sikukuu ya Pasaka ya Bwana.Mtume anataka kutangua tatizo  ambalo kwa hakika Jumuia ya Wakorinto ndiyo ilikuwa kiini cha mabishano. Ufufuko ndiyo suala la mwisho kukabiliwa katika barua, labda ni katika mtiririko wa umuhimu, kwasababu hiyo ni ya  kwanza na mengine yote yanasimama juu yake. Akiongea na wakristo wake, Mtakatifu Paulo anaanzia  suala lisilopingika na siyo suala la kutafakariwa kwa  mtu mwenye hekima, bali ni hali halisi ,ni tukio ambalo limegusa maisha ya baadhi ya wangine. Ukristo unazaliwa hapo .Hizo siyo itikadi za mawazo tu na siyo mpango wa kifalsafa bali ni safari ya imani ambayo inatokana na tukio lililoshuhudiwa na mitume wa Kwanza wa Yesu.

Kwa maana hiyo Mtakatifu Paulo anaelezea kwamba “Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu; kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa; kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili.” (Taz,1 Kor 15,3-5). Akitangaza tukio hili ambalo ndilo kiini cha imani, Mtakatifu Paulo anasisitiza zaidi ya hayo kiini cha fumbo la Pasqua, yaani juu ya Yesu kufufuka. Iwapo hayo yote yangeishia katika kifo tu, kwake yeye tu ngekuwa na mfano wa wa kuelezea , lakini huo isingeweza kuwa imani yetu , kwani kwetu sisi angebaki  mtu maarufu tu , lakini yeye alikufa na kufufuka.Hiyo ni kwa sababu imani yetu inatokana na ufufuko. Kukubali kwamba Kristo alikufa Msalabani siyo tendo la imani. Badala yake ninaamini kwamba alifufuka. Imani yetu inazaliwa asubuhi ya Pasaka,Mtume Paulo anatoa orodha ya watu waliotokewa na Yesu mfufuka yaani “kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili”. (Taz 1Kor15, 5-7).

Kwa njia hiyo baba Mtakatifu Francisko amesema hapo tunayo maelezo yote kuhusiana na Pasaka na watu wote walio weza kuwasiliana na Mfufuka. Juu ya orodha yupo Kefa maana yake Petro na kikundi cha watu kumi na mbili, baadaye miatano na wengine ambao wangeweza kutoa ushuhuda na pia anatajwa Yakobo, na mwisho anajitaja mwenyewe  asemavyo “ baada ya wote akanitokea hata mimi , mimi niliye kuwa kama mtu aliyezaliwa kabla ya wakati. Paulo anatumia njia hii kwa kuelezea historia binafsi ya matatizo yake, yeye hakuwa mtumikiaji kanisani Baba Mtakatifu amesema, kwani yeye alikuwa ni mtesi na mchokozi wa Kanisa,alikuwa mwenye kiburi na uhakika kwamba anajisikia mwaume aliyefika, kuwa na mawazo wazi kana kwamba amejiweza katika shughuli zake na maisha yake.Lakini siku moja ikamtokea jambo la pekee bila kutegemea, tendo la kukutana na Yesu mfufuka katika njia ya Damasko. Pale hakuonekana tena mwaume mwenye nguvu bali alianguka chini, hapo ndipo matukio yaliyo jitokeza na kubadilisha maana ya maisha.Aliyekuwa mtesi wa Kanisa anakuwa mtume, Kwanini, kwasababu yeye amemuona Yesu mzima, alimwona Yesu Mfufuka. Hiyo ndiyo msingi wa imani ya Paulo, kama vile imani ya mitume wengine, kama ilivyo imani ya Kanisa ,na kama ilivyo imani yetu.

Ni vizuri kufikiria ukristo, kwamba jambo muhimu ndilo hili, siyo kwa namna yetu ya kutafuta Mungu katika ukweli wa ukisitasita, zaidi ni kumtafuta Mungu kwa ajili yetu. Yesu ametuchukua ametuamsha  ametukomboa, hatatuacha kamwe.Ukristo ni neema ni mshangao, kwasbabu  mioyo yetu ina uwezo wa mshangao. Moyo uliofungwa na unao bagua hauna uwezo wa kushangaam na huweze kutambua nini maana ya ukristo.Kwasababu Ukirsoto ni neema na no neema peke yake yenye uwezo wa kukutana na mshango wa makutano.Kwahiyo hata kama sisi ni wadhambi,maana wote tu wadhambi, mema mengi yamebaki katika karatasi au tukitazama maisha yetu, tunatambua kwamba tumejazwa na mambo mengi yasiyo kuwa mazuri,kumbuka kwamba asubuhi ya Pasaka tunaweza kufanya kama  watu ambao injili imewaeleza. Kwenda katika kabiri zetu kwasababu wote tunayo mizigo ndani yetu.Twenda pale kuona jinsi gani Mungu anauwezo wa kufufuka kuanzia pale.

Maana pale kunwa furaha ya maisha.Kwenda katika kaburi la Yusu kutazama jiwe kubwa lililoviringishwa na kufikiria kwamba mungu anatenda maajabu tusiyo tegemea katika maisha endelevu kwetu sisi na kwa wengine. Hapo kuna furaha kubwa na maisha mahali ambapo wengi wanafikiria kuna huzuni na giza;Mungu uotesha maua sehemu nzuri na hata katika sehemu zenye mawe na ukame.Baba Mtakatifu Francisko amemalizia akisema kuwa Mkristo siyo maana ya kuteseka na kifo, bali ni upendo wa Mungu kwetu sisi tulio shinda adui mkali. Mungu ni mkuu wa yote hata kitu kidogo maana yatosha kuasha mshumaa mmoja tu ukashinda giza nene la usiku. Mtakatifu Paulo anatoa sauti iliyokuwa tayari imetolewa na manabii kwamba “Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?”(1Kor,15,55).

Hivyo katika siku hizi za Pasaka tuichukue sauti hiyo kwa moyo na iwapo tunaulizwa kwa sababu gani tunatabasamu tuliyo ipokea kwa uvumilivu wetu na kushirikishana,tunaweza kujibu kwamba Yesu bado yuko hapa hai na anaendelea kuishi kati yetu,yupo hapa katika kiwanja na sisi anaishi, amefufuka!.
Na mara baada ya katekesi yake , kama kawaida Baba Mtaktifu Francisko, amewapa salam zake , mahujaji wote kutoka pande zote za dunia, bila kuwasahau vijana, wagonjwa na wanandoa wapya waliokuwapo katika viwanja vya Makatifu Petro kusikiliza katekesi hiyo na kuwapa baraka zake.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.