2017-04-14 16:27:00

Yesu Msalabani amekabidhi Maria Mama yake kuwa Mama wa Kanisa!


Ndugu wasikilizaji wapendwa wa Radio Vatican leo hii ni siku ya Ijumaa Kuu ambapo Mama Kanisa Katoliki, anatualika kwa namna ya pekee kutafakari kwa kina  fumbo kuu  hasa kwa siku hizi za mateso ya Bwana wetu Yesu kristo, hatuna budi kwa siku ya leo, kuwa pamoja, kumsindikiza  katika mateso yake na ni katika mateso yetu wenyewe, ambapo siyo rahisi kutafakari fumbo hili kuu la mateso kwa mtazamo wa kijuju tu na kuelewa pasipo nguvu ya Roho Mtakatifu tunaye muomba usiku na mchana atujalie kupokea na kukubali ile njia ye mateso aliyo chagua yeye ili kuweza kutukomboa.Kwa njia hiyo tuone maneno  saba  ya Yesu aliyo yasema akiwa msalabani, lakini pamoja na hayo  ni zaidi ya maeno saba aliyo tamka akiwa msalabani, kwa sababu hayo ni zaidi ya maneno, ya matendo,ya  matukio , ya uzoefu wa kuishi, ya uchungu na mateso, ya furaha na matumaini. Kila aina ya Neno pekee kwa  pamoja yana jieleza kwa ufupi wa maisha ya Yesu,ni maisha ambayo yeye mwenyewe amejitoa kwa huru wake kwa ajili ya upendo wa binadamu.

Maneno ya kwanza matatu yanatoka katika Injili ya Mtakatifu Yohane;“Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.“Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake,” (Yoh 19,25-27).

Katika neno hili tutazame kwa karibu sana wanawake jasiri , pamoja  na yote yaliyotokea , hawakumwacha Yesu kamwe, hawa ni wanawake walio mfuata huko Galilaya, walisikiliza maneno yake  na waliona miujiza, ni wanawake walio  jisikia kukubaliwa na kutambuliwa, waliosamehewa na kupona na zaidi ya kupendwa.Hawa wanajumuishwa kuwa  mwamke wa kila aina, kwa hali yoyote, masikini, wayahudi, wageni, wenye afya , wagonjwa na walio baguliwa. Hata kama Mwinjili alitaja baadhi ya majina ya wanawake  lakini tunapata utambuzi ya kuwa  wote walikuwa pamoja kwa namna moja au nyingine karibu au mbali kwa sababu haijalishi umbali bali wote  walikuwapo mbele ya msalaba. Walikuwapo msalabani japokuwa wasingefanya lolote zaidi ya kutafakari , kupenda, kuteseka na kukaa kimya.

Wanawake hao tunawafananisha na wanawake wengi  kwa nyakati zetu , ambao wanateseka wakati huo wako kimya, wamezoea kupata kipigo, katika mateso yao na katika ukimya.Tuwaze katika nchi zetu barani Afrika, ni wanawake wangapi wanateseka, pasipokuwa na hatia? Tazama kwa upeo wako wa karibu na mbali, ona familia jirani, mara ngapi unasikia kelele za vipigo, wanao lia ni watoto lakini mwanamke hatoi sauti?... Pamoja na hayo ukweli ni kwamba aliyeteseka zaidi akiwa wa kwanza ni mama Maria , mama yake Yesu,na kufuatia  wanawake wengi wa nyakati zetu ambao wako radhi kutoa maisha yao, kuliko kuona watoto wao wanateseka na katika mahangaiko ya dunia hii.

Mtakatifu Roberto Bellarmino alitoa tafakari kuhusu mateso ya Maria akisema ;kama vile upendo ni kipimo cha uchungu, na hivyo uchungu mwingi wa Bikira Maria,unao lenga mwanae dhidi ya mateso makali ya  ukatili alio upata kutoka kwa binadamu, yote hiyo ni kwasababu alimpenda zaidi.Kwa njia hiyo Yesu akiwa ametundikwa msalabani,  anatambua mama yake mwenye uchungu akiwa karibu na mtume wake mpendelevu  na kumweleza maneno yenye fumbo , kubwa litokalo juu kwa urahisi inaweza kufiria ni msemo tu , lakini wenye kuwa na maana zaidi.

Jambo la kushangaza ni kwamba mwinjili kwa wakati huo hawataji majina, bali Yesu mwewe anataja mwamke, kama vile alivyokuwa ametaja mwanamke wakati wa Arusi ya Kana.Pamoja na hayo, Yesu mwenyewe asikika akiomba makazi ya mama yake kupitia mtume wake, maana kwa sasa anabaki mjane, peke yake, anahitaji msaada wa jambo fulani. Kwa njia hiyo tunaweza kuona kwa nini mwinjili anaeleza , maneno matatu katika msalaba, mwanamke, mama, na  mwana kwa maana ya kuonesha wazi kazi ambayo wanapaswa kuitekeleza.Ni mara ngapi wanawake wajane wanabaki hawana wa kuwalinda, Afrika ni wanawake wangapi ni wajane, wanakosa haki, hawana mtetezi…ni jambo la kutafakari namna ya wito wa Yesu , ni kama kutoa amri ya uangalizi wa wanawake wajane.

Katika injili Mtakatifu Yohane  mtazamo wake ni kwamba Mama wa Yesu na mtume mpendelevu , katika hatua hiyo anaonesha wawe ni wa kulinganishwa ,kuingwa mfano  kwa namna yake.Hiyo  ndiyo sababu Yesu anamfanya Mama Maria bila kuacha kuwa mama wa Yesu, ni mfano wa Kanisa,ambalo ndiyo mama yetu, na Yohane, bila kuacha kuwa mtume mpendwa wa Yesu anaendelea  kuwakilisha mitume wote wa Yesu , hata wote walio chagua kufuata nyayo zake.Hapo  tunaweza kutambua Manenoya Yesu akisema “tazama mwanao, na tazama mama yako”, siyo kueleza wasiwasi juu ya mama yake mwenyewe wakati anakufa, bali jambo msingi na  kina linalo unganishwa wote. Tangu Maria kukabidhiwa Yohane , ulitengenezwa uhusiano mpya wa kiroho , ambao Yesu ametaka mwenyewe kuukarabati na ambao utadumu milele.

Yesu tunakushukuru kwa sababu ya kuwaamini hata wanawake, katika imani yao, katika uamininfu wao , katika ushuhuda wao utume wao. Asante kwa yote uliyo fanya na unayo endelea kuyafanya. Asante kwasababu ya kukabidhi Kanisa mama yako katika mikono yake.
Kama tumeweza kuona maneno matatu ya kwanza ya Yesu ya kionesha huruma yake kwa wengine, sasa watesi wake, wanyang’anyi, mama yake na mtume mpendelevu ni maneno manne yanayo tafakarisha juu ya nguvu ya mateso ya ndani ya roho, mapambano ya maisha, kifo , kukataa na kukubali fumbo. Ni maneno manne yanayo toa ushuhuda wa ushahidi wa mwana wa Mungu aliykubali kujitoa kwa ajili ya ukombozi wa mwandamu.

Tunasoma; “Ilikuwa yapata saa sita mchana; jua likaacha kuangaza, giza likafunika nchi yote mpaka saa tisa, na pazia lililokuwa limetundikwa Hekaluni likapasuka vipande viwili. Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba, naiweka roho yangu mikononi mwako.” Alipokwisha sema hayo, akakata roho.  (Luka 23, 44-46).
Katika matanga yanayowakilisha dunia nzima ya kifo cha msalaba, kwayo muda umesimama na kuacha nafasi ya maisha mapya. Hii ni kutokana na giza nene limetanda na pazia la ekalu kupasuka vipande viwili ikiwa na maana ya  kutoa fursa ya kuonesha kile kisicho onekana  kuonekana wazi .Pamoja na mtatizo mengi yanao ikumba dunia hii msalaba unabaki daima umesimama kama wimbo mmoja usemavyo wakati wa kuabudu  msalaba.
Yesu anatoa pumzi akimwita Baba yake. Ni yule Baba aliye mpenda hata akamtuma duniani kutimiza utume wake, ambao kwa sasa katika macho ya binadamu haunekani ukombzoi huo.Yesu anatamkwa Baba Mikononi mwako naiweka roho yangu , ndiyo pia maombi ya mtakatifu Stefano wakati wa kifo chake, Bwana Yesu pokea roho yangu(Mdo 7, 59).Maneno yake ya mwisho wa shahidi huyo  ya maana ya kwamba tuna mwachia maisha yetu Mungu tu na siyo kuacha maisha yetu ardhini 

Kwa maana hiyo tunaweza kusali pamoja tukisema, "Bwana asante kwa maneno yako, sauti yako ya nguvu kabla ya kuangukia mikono nwa Baba ambaye amempokea akiwa amejaa damu , lakini na ushindi mkubwa. Ni kilio cha kutuliza binadamu anayeteseka, huko Afrika, asiye kuwa na chakula, asiye kuwa na maji ya kunywa, asiye kuwa na cha kujifunika au mkimbizi kwa ajili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, asiye kuwa na dawa, anayeshutumiwa na kulaumiwa, anaye baguliwa, anaye nyonywa kwa utajiri wake, anaye kuwa maskini kutokana na kunyonywa  mali zake asili , ndiyo ni kilio cha matumaini kwa wote wanao taka kukufuata".

Katika  maneno saba ya Yesu aliyotakwa msalabani na  tuliyo sikia ya kwanza kati ya hayo , neno au kilio cha nguvu  tucho sikia ni kama tabia ya Yesu mwenyewe kumuomba Baba yake lakini  ni kama vile  amekuwa kimya na kufanya liwe fumbo lisilo elezeka katika ukimya huo na kutokueleweka kwa wafuasi wake na watu wote. Na katika kilio cha nguvu kwenye maeno ya  mwisho yasemayo kutoa roho yake .Yesu anatoa ujumbe wa kuhamasisha  wote hasa mbele ya janga hili la mateso.Hiyo ni kufanya  kutafakari jinsi ya kuona uwazi kabisa wa mwisho wa Yesu katika hali ya kutisha na ngumu ambayo mitume wake waweze kukabiliana nayo. Ili mitume waweze kutambua mateso haya, ilibidi warudi kutazama kwa upya utamaduni wa kale. Kuchimbua historia ya kinabii na kama wasingerudi nyuma , ingekuwa vigumu kabisa kukubali janga hili la mateso ya Yesu. Na katika  kurudi kuchimbua utamaduni wa historia ya kale waliweza kupata ukweli ulio waangaza matumaini na kuwaruhusu waweze kujua zaidi mwisho wake Yesu kama tunavyoona hata sisi leo hii, hisotoria ya wokovu wetu.

Katika kurudi katika chimbuko la mapokeo ya utamadni wa kale wa  historia yote ya mateso ya Yesu ,mwenye haki anateseka na hadi kufikia mauti, tunaipokea kutoka historia ya maandiko Matakatifu ya Agano la Kale kuhusu Yosefu mtoto wa mwisho wa mzee Yakobo aliye uzwa kama mtumwa na ndugu zake. Tunamwona pia Yesu mteswa kutoka katika Zaburi,tunamkuta Yesu katika kitabu cha Ayubu na mateso yake, ananuka  kwa madonda yake, aidha katika kitabu cha  cha Nabii Yeremia, akiwa ametupwa kwenye matope na kuchwa peke yake. Kadhalika, Nabii Daniel aliyetupwa kwenye shimo la simba, Katika Kitabu cha hekima na zaidi kitabu cha Nabii Isaya , anaye mwelezea kama mtumishi wa Mungu aliye ondolewa kwa nguvu duniani  lakini “Mungu sema baada ya kutaabika sana mtumishi wangu satafurahi.Kwa kuwajibika kwake kikamilifu atatosheka na matokeo hayo. Kwa maalifa yake mtumishi wangu mwadilifu, atafanya wengi wawe waadilifu .Yeye atazibeba dhambi zao. Kwa hiyo nitamweka katika cheo cha wakuu atagawa nyara pamoja na wenye nguvu , kwakuwa alijotolea mwenyewe kufa, akajiachia kuwa kundi moja na wakosefu , alizibeba dhambi za watu wengi akawaombea msamaha hao wakosefu.

Leo hii ni ijumaa Kuu ya mwaka 2017 Yesu bado anakufa kwa kwa mara nyingine tena huko Nazereth, ni katika wayahudu wanao endelea kushtumiwa , ni yyey anayekufa kwa ajili ya wengine, ili kuweza kuwakomboa wengine katika wafu. 
Ujumbe huu uamshe hisia zetu, za kuamsha imani yetu zaidi ili dhifu, kwani Yesu anakufa na udhaifu wetu, kwa ajili ya kutupatia nguvu, haijalishi matatizo mengi yanayo ikabili familia yako,taifa lako, na mataifa yote ulimwenguni, haijalishi watu wano kusonga kwasababu wewe ni mwenye ni mwenye imani, unataka haki, untafuta amani, unatenda matendo ya huruma, unawatembelea wagonjwa, wafungwa, unazungyuka barabarani kuwatafuta watoto ombaomba Kariakoo , Mazenze, Nyamagana, Korokosho, Kampala, Bujumbula Malawi, Zambia Sudan ya Kusini, Msumbiji, Afrika ya Kusini, Maidaguri,Msumbiji.Yesu anakufa kwa ajili ya kuamsha dhamiri binafsi , na maneno yeke saba yajikite katika mshikamano kwa ajili ya binadamu woea katika mataifa wanao sumbuka kutokana na chuki, nguvu vita , ukosefu wa haki, rushwa ambayo imekuwa ni saratani ya mataifa mengi na kusabisha kudhoofisha na kuzidisha umasikini wa nchi, njaa na ukame.

Maneno saba ya Yesu msalabani, yaamshe dhamiri zetu ambazo zinapendelea mali kwa ajili ya mambo binafsi badala ya kuwafikiria wengine , Maneno ya Yesu ya kutoa roho yake yafungue midomo yetu kueleza ukweli, kuwa wakweli, kuwapenda wengine, kuwatumikia kwa upendo  mahali walipo, hasa wale wenye kuhitaji msaada wetu, tuondokane na ubinafsi, tuwe na nuru. Sauti ya kutoa roho yake iungane na yetu kumtambua kuwa kweli ni mwana wa Mungu.
Ninawatakia Ijumaa Kuu njema.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.