2017-04-13 15:18:00

Ni mamilioni ya watoto wadogo wanaoishi barabarani ulimwenguni!


Kwa miaka saba mfululizo , kumekuwa na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya watoto wanaoishi barabarani, kwa lengo la kumasisha dhamiri ya umma na kila Taifa katika matukio ambayo mara nyingi yanabaki yamefichika. Ni milioni ya watoto duniani wanaishi barabarani ,ambapo kwa mwaka 2017 hata Umoja wa Mataifa wamejikita katika kuwahimiza mataifa ili kufanya kila iwezekanavyo kutambua haki na ulinzi wa watoto hawa.Shughuli nyingi za ulinzi wa watoto, mara nyingi utendwa na kwa matendo ya huruma na Mashirika yasiyo ya kiserikali kama anavyo eleza Alessia Andena , kutoka  katika kitengo cha mpango wa wamisionari duniani wa Shirika  Don Bosco alipo kutana na mwandishi wa habari wa Radio Vatican.

Alessia amesema , watoto wanaoishi barabarani  katika hali hasi ngumu na zaidi waakutana na hatari kutokana na ukosefu wa mtu mzima anayweza kuwasadia wakakakua kama binadamu , na pia kukosa mambo msingi ya maisha zaidi ule upendo.Katika kukumbuka haki msingi za watoto wanapo paswa kuwa nazo , na hasa kwa wale amabao hawana baahati ya kuwa nazi, ni jambo la kutufanya tutafakari zaidim kwa kuzingatia kizazi hiki na kile ambacho kitapoteza iwapo hakuna uangalizi kwa upande wa watu wazima , hiyo siyo tu kwa ajili ya kuwapatia vifaa vya kuwafurahisha tu, bali hasa katika ulinzi na uwepo wa mtu mzima wa kuwalinda na kuwatetea.

Kama utume wa Don Bosco unavyo jieleze au kujulikana tangu mwanzo kwa ajili ya kuwasaidia watoto na vijana , ni karama na ndiyo maana Mtakatifu JohnBosko alisema, siyo kwamaba watoto wanalazimika kupendwa, bali kazi muhimu ya kufanya ni kwamba wao wakatambua kwamba wanapendwa.Kwa namna hiyo kila anayejikita katika utume wa watoto na vijana hana budi kukariri sentensi hiyo. Vijana lazima watambue wenyewe kwamba wanapendwa.
Shirika la Don Bosco wanatenda kazi yao ya kitume kwa ajili ya vijana wote na pia wanaoishi barabarani katika ulimwengu mzima kwa mfano  Amerika ya Kusini ,kwenye nchi ya   Brazili ; Bolvia, Equador, Peru, barani Afrika, Asia katika Myanmar, Kamboja , Thailandia na laos .Kwa mfano Barani Afrika Alessia amependa kutoa mfano wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huko Lubumbashi , ambao ni mji mkubwa wa tatu muhimu katika nchi hiyo.

Amesema kwamba  takwimu zilizofanyika mwaka 2016 , watoto wadogo wanaoishi barabarani huko Lubumbashi ni kuanzia 1,200 na 2,500 .Maana yake familia nyingi zimejaribiwa na umaskini, kuwasababishia watoto wengi kuzurura barabarani na mitaani wakitafuta kazi ya kuweza kukidhi haja ya mahitaji ya familia.Mapadre wa Shirika la Don Bosco wanaoishi katika maeneo hayo wakitenda utume wa vijana barabarani, wanakwenda wakati wa usiku barabarani kuongea na kujenga mahusiano ya uaminifu na watoto hao, lengo likiwa kuwatoa barabarani, ni kujenga mahusiano kwa uaminifu ikiwa hatua ya kwanza. Alessia amesema, uaminifu ni ufunguo wa kwanza katika mchakato mzima wa watoto wanaoishi barabarani, kwasababu wamepoteza matumaini kutoka kwa watu wazima. Wamepoteza imani, maana ,watu wazima wamewatelekeza kiasi cha kujisahau kwamba watoto hao wana haki ya kuishi kiutu, kulindwa , kupata elimu chakula na malazi.Amemaliza akisema, ili kuweza kuwatoa watoto barabarni, wanahitaji uaminifu, kinyume, siyo rahisi kufanya safari ya kuwarudisha watoto wanaoishi barabarani na kujenga mahusiano ya matumaini.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.