2017-04-13 14:43:00

Baa la njaa na ukame nchi za Pembe ya Afrika,Yemen na Nigeria!


Tatizio lingeweza kutatuliwa lakini ni fedha zinahitajika; ni tamko kutoka katika Kamati ya Umoja wa Mtaifa ya  Shirika la kuhudumia wakimbizi (Unhcr) ambao wametoa  mapema wiki hii huko Gineva kutokana na kuongezeka kwa hatari ya vifo vya jumla kwa sababu ya baa la njaa katika maeneo ya Pembe ya Afrika,Yemen na Nigeria. Taarifa zinaonesha kwamba ni karibia milioni 20 ya watu wamekumbwa na ukame,na milioni nne ni wakimbizi. Kwa namna ya pekee watu milioni 22 ni watoto wanao sumbuliwa na utapia mlo,hawana maji na madawa ya kutosha. Milioni moja na nusu ya watoto hao wanaweza kufa kwasababu ya njaa. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wanathibitisha kwamba watu wanaweza kufa kwa ukosefu wa chakula nchini Sudan ya kusini, mahali ambapo hivi karibuni walitangaza janga la kitaifa.

Nchini Somalia janga la kitaifa ni kwasababu ya ukame ambapo watu milioni 2,9 wanakabiliwa na hali hiyo. Kaskazini ya Nigeria utapiamlo unazidi kuongezeka, pamoja na kuendelea na mashamabulizi ya kigaidi ya Boko Haramu.Huko nchini Yemen, mahali ambapo vita vimedumu kwa muda mrefu, watu milioni saba hawana chakula cha kutosha.Kwa upande wa watoto Shirika la kusaidia watoto Unicef limethibitisha juhudi zake katika eneo hilo, lakini wanatoa habari kwamba kuna upungufu wa misaada kutoka katika mataifa, kuanzia  Washington, ambapo katika mktaba wa mwisho wa Donald Trump , umekata nusu ya uwekezaji wa mipango ya kibinadamu.

Umoja wa Mataifa unahitaji milioni 712 za dola  kwa mwaka 2017, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema ni bilioni 4,4 za dola zinahitajika  kwa ajili ya kukidhi majanga angalau kufikia mwezi  Julai mwaka huu, lakini ni asilimia 10 tu fedha kati ya zile zinazo hitajika. 
Ukame katika Pembe ya Afrika kwa mwaka 2011,watu 260,000 walipoteza maisha yao, zaidi ya nusu yao walikuwa ni watoto chini ya miaka mitano. Shirika la kuhudumia wakimbizi (Unhcr) wanasisitiza kwamba hali ya  tukio la namna hii kamwe lisitokee.Mipango ya Shirika la kuhudumia wakimbizi Sudan ya Kusin , Somalia na Yemen hadi sasa wamepokea fedha asilimia kati ya 3 hadi 11 tu. Msemaji wa Shirika hilo amesema, kipeo cha binadamu kinachotatuliwa,kimekuwa kisicho wezekana!.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.