2017-04-12 14:35:00

Kuna ongezeko la watu wenye magonjwa ya kudumu nchini Italia"


Ripoti ya takwimu ya Afya  kwa mwaka 2016 nchini Italia imewakilishwa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Afya "Agostino Gemelli" Roma. Ripoti hiyo ni kuonesha juu ya afya kwa upande wa wazalendo nchini Italia, vituo vyote vya afya , mgawanyiko wa kutoa huduma ulio fanywa na watafiti 180 kutoka katika Vyuo  Vikuu na sekta mbalimbali lakini zaidi  takwimu za Kitaifa. Mkurugenzi wa Taifa kuhusu  afya ya mikoa nchini Italia aliye wakilisha Ripoti hiyo akihojiwa na mwandishi wa habari wa  Radio Vatican amesema, pamoja na mengi yaliyomo katika ripoti hiyo kuna ongezeko la magonjwa ya kudumu kwenye  vituo vyote vya afya kitaifa. Hiyo ni matokeo ya sekta hii nyeti kuonesha kuwa na kiasi kikubwa cha kuwekezaji  kiuchumi imekuwa kubwa zaidi kwa miaka 15 ya hivi karibuni.

Asilimia 40 ya watu walio ongezeka nchi Italia ambao ni kusema milioni 23 ya waitaliani,kati yao asilimia 20 inaonesha kwamba watu wana magonjwa mawili ya kudumu, ambayo yanagharimu asilimia 55 ya rasimali ya huduma ya afya kitaifa. Anaongeza kusema,hiyo ni changamoto ya muhongo huu kwasababu bila kuwa na mipango madhubiti, maana yake walio wengi hawataweza kupata huduma zaidi ya matibabu.
Namna ya kuwasadia kimatibabu, kwa upande mwingine kuna tatizo la uwekezaji kwa ajili ya kuzuia kwani amesema mara nyingi magojwa yanafikia kuwa ya kudumu kutokana kwamba wengi wanafika vituo vya afya  wakiwa tayari na uzito mkubwa, hawawezi kufanya kazi yoyote kimwili, wengine wanakunywa pombe zaidi, au wengine wanavuta zaidi, lakini pamoja na sababu hizi nne za hatari bado kuna uwezekano wa kubadilishwa.

Kubadilishwa kwake ni wazi lakini lazima kujaribu kujipanga ili kuweza kuwasaidia wazelendo wa Italia wasiachwe peke yao kwasababu inawezakana kukaribisha mapendekezo na kuwaongoza kuelekea katika tabia yenye busara. Zaidi ya hayo inapotokea magonjwa, inabidi kuchukua hatua japokuwa lazima hatua hiyo kuichukua kwa njia zinazo faa na matumizi ya dawa sahihi bila kupoteza rasilimali.
Kwa mtazamo wa upungufu wa watu ambao kwasasa hawafikii umri wa miaka 100 tofauti na miaka ya nyuma.Mwaka jana takwimu zilionesha tayari tatizo hilo na kwasasa ripoti pia zinaonesha kushuka kwa watu kuishi miaka mia  moja lakini wakati huo huo  takwimu pia zinaonesha kuongezeka kwa hali ya maisha kwa ngazi ya kimataifa, kwa njia hiyo ni ishara ya dharura na hivyo ni taadhali ya kuwa makini kwa nyakati zijazo.

Katika takwimu za upungufu wa watu kufikia umri mkubwa zaidi unazidi kujionesha katika mikoa ya Kusini mwa Italia.Suala hilo linatokana na kwamba watu wa kusini mwa Italia hawafanyi uchunguzi wa afya na pia chanjo za kuzuia magojwa kwa wastani, ndiyo maana  karibu mikoa ya kusini watu wake ni wenye uzito mkubwa kimwili, wana magonjwa ya kusukari, wanapata shinikizo la damu kwa wingi na wakati huo huo hawezi kutibiwa vizuri;Ameongeza jambo hili ni gumu na halikubaliki.Sababu pia kubwa ya tatizo hilo anathibitisha ni ukosefu wa mgawanyiko sawa kwa vituo vya afya ambavyo havitoshelezi idadi ya watu  kwa  kukizingatia kwamba mikoa ya kusini kumekuwa pia na ongezeko la wahamiaji .Wahamiaji ambao wanahitaji  matibabu, katika  huduma ya afya, kiasi cha kuziidisha hali kuwa ngumu kwa ajili ya  kukosekana wahudumu wa kutosha. Hiyo inachangia sababu ya kuwa na wagongwa wa kudumu.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.