2017-04-11 15:06:00

Italia kutazama mchakato wa Mswada mpya wa wahamiaji!


Wakati harakati za mapambano ili kuzuia watu waalifu wanaotumia mitumbwi kuvusha watu kuja Ulaya, nchi ya  Italia inafanya mikutano ya kutafuta mbinu ya kuweka sheria na kuona ni jinsi gani ya kuwafukuza  waalifu, ili kuweza kutunza usalama wa taifa kabla wao hawajaanza mipango yao ya ugaidi.Tangu mwanzo wa mwaka huu watu 32 wanao sadikika kuwa na vitendo vya ugaidi au kuwa na mawasiliano ya watu waalifu na magaidi wamefukuzwa na kurudishwa makwao.

Taarifa inasema hii ni muhimu kwasababu inawezekana kuwa chombo madhubuti ambacho kinaweza kusaidia kuwa na msimamo mkali dhidi ya wahamiaji na wakimbizi  wanao ingia ndani ya nchi wakiwa ni waalifu au magaidi wakaweza kusababisha matatizo na ya usalama wa ndani ya nchi.Hayo yamedhibitishwa na Waziri wa Mambo ya ndani nchini Italia Bwana Marco Minniti , ambaye pia amesema hata hivyo tatizo halisi siyo uhamiaji lakini mojawapo ya tatizo ni ukosefu wa kushirikishwa ,kitu ambacho kingeweza kusaidia kizazi cha pili au watu wa mataifa ya ulaya. Pamoja na hayo Bunge nchini  Italia limeanza mchakato dhidi kupitisha mswada wa amri ya kufukuza wanaojihusisha na matendo ya kialifu.

Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji (UNHCR) ameomba kusitishwa kwa muda  uhamishwaji wa watu wanao omba hifadhi kwenda nchi ya Hungary kutoka katika nchi nyingine za Umoja wa Ulaya kwa mujibu wa  Mkataba uliotolewa Dublin. Mkataba wa Dublin ni chombo kinachotumiwa na Umoja wa nchi za  Ulaya katika uamuzi wa  nchi za Ulaya kutathimini maombi ya hifadhi kisiasa.

Hali ya watu wanao tafuta hifadhi katika nchi ya Hungary, ilikuwa tayari inaleta wasiwasi mkubwa kwa  Shirika la Umoja wa Mataifa la Waamiaji, (UNHCR) na kwasasa kuanza kutumika sheria mpya ambayo inatazama ulazima wa kutokuzuia watu wanao fatufa hifadhi hali imekuwa mbaya.NI maneno yaliyotamkwa na Filippo Grandi, mwakilishi wa Umoja wa mataifa wa kuhudumia Wakimbizi.Kutokana na hali mbaya ya watu wanao tafuta hifadhi katika nchi ya Hungary,anaomba nchi zisimamishe uhamishaji wa wakimbizi katika nchi hiyo, mpaka mamlaka ya nchi ya Hungary na mchakato wa kisiasa watakapo kubaliana wote sheria ya Ulaya na Kimataifa.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.