2017-04-10 15:31:00

Mheshimiwa Padre Edet Akpan ateuliwa kuwa Askofu wa Ogoja, Nigeria


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Edet Akpan alizaliwa kunako mwaka 1952 huko Ikot Ekpene kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Ogoja, nchini Nigeria. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Paroko wa Parokia ya “Holy Rozary Parish” Jimbo kuu la Abuja, Nigeria. Askofu mteule Edet Akpan baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi kunako tarehe 12 Oktoba 1985 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Ikto Ekpene. Tangu wakati huo ametekeleza dhamana na utume wake kama Mwalimu na mlezi; Paroko usu na kunako mwaka 1987 hadi mwaka 1989 alipelekwa na Jimbo kuongezea ujuzi na maarifa katika Chuo Kikuu cha Nsukka, kilichoko nchini Nigeria.

Kunako mwaka 1989 hadi mwaka 1991 alitumwa na Jimbo kutoa huduma za kichungaji Jimbo kuu la Abuja kama Mapadre wa “Fidei donum” yaani “Zawadi ya imani”. Kati ya Mwaka 1991 hadi mwaka 1994 alikuwa ni Gombera wa Seminari ndogo ya “Watakatifu Simon ina Yuda, eneo la Kule. Tangu mwaka 2001 hadi mwaka 2017 amekuwa ni Paroko katika Parokia mbali mbali Jimbo kuu la Abuja, Nigeria hadi kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu mpya wa Jimbo katoliki Ogoja, nchini Nigeria. Jimbo hili limekuwa wazi baada ya Baba Mtakatifu Francisko kumhamisha Askofu John Ebebe Ayah kwenda Jimbo Katoliki la Uyo, nchini Nigeria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.