2017-04-10 17:06:00

Afrika yahitaji kuongeza utafiti kisayansi,ubunifu na teknolojia


Afrika bado haijiwezi  kimaendeleo  katika sekta ya sayansi, Teknolojia ya maendeleo endelevu na ubunifu ili kuweza  kujitosheleza na kuingia katika mashindano ya sekta tatu msingi za maendeleo endelevu ya Bara. Hiyo ni Ripoti ya Chama cha kujenga uwezo Afrika kwa mwaka 2017.Chama hicho kinachojikita hasa katika utafiti wa maendeleo ambayo amefrika imefikia katika Sekta ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu. Chama hicho kwa ushirikiano na Uwezo wa Afrika ili kupima uwezo wa bara kwenye  suala la ushindani katika sekta tatu, lakini pia iko chini ya vipengele vingine vinne vidogo ambavyo vinatathimini sera za kisiasa,taratibu za utekelezaji, matokeo ya kuimarisha sekta binafsi katika ngazi ya kitaifa na matokeo ya shughuli zenye lengo la kuendeleza uwezo wa Afrika  kufikia  uwezo wa sayansi na teknolojia.

Uchunguzi wa muda mrefu  umetoa takwimu za kuonesha kuwa kuna mapungufu makubwa katika bara kwenye ujuzi wa msingi wa ufundi , katika maendeleo ya sayansi , teknolojia na mikakati ya ubunifu. Kwa njia hiyo , wanapendekeza kuwa  taasisi za kikanda  zijenga uhusiano kati ya vyuo Vikuu, serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali , masoko ya ajira ili kukuza sekta hizo tatu.
Aidha  ripoti imeonesha kuwa uwekezaji katika sayansi na teknoljia ya elimu, uhandisi na hisabati ni muhimu sana kwa Afrika ili kuongeza kwa kasi ubunifu ,kufanya ushindani wa haraka kufikia kundi kubwa la rasimali ya binadamu na vifaaa katika sekta hizi kimkakati. Ni jambo la kuvutia kutambua kuwa hali imekuwa  zaidi muhimu kwa ajili ya bara mara baada ya kupitishwa katika Agenda ya 2063 ya Umoja wa Mataifa ambayo imeweka  namba moja kati ya matarajio saba yenye kukuza mendeleo endelevu ya bara.

Ripoti hasa imetazama  nchi 44 ikiwemo nchi ya Morocco ambayo inachukua nafasi ya kwanza ikufuatiwa , Msumbiji na Rwanda. Mataifa matatu pamoja na mengine sita ( sambamba kwa asilimia 20,5%), kwenye ripoti uwezo wao unategemea na pointi kuanzia juu hadi ya chini zenye pointi 60 kwa 80.Nchi mbili tu ya Swaziland na Jamhuri ya Afrika ya Kati (zinaonesha asilimia 4.5%) ndiyo zinaoneka kuwa za mwisho katika orodha kwa  pointi kati ya 30 na 40. Nchi 33 zinazobaki ripoti inaonesha uhusiano (sambamba kwa asilimia 75%) na zinachukua nafasi ya kati kwa kuwiana na pointi kati ya 40 na 60.

Ni muhimu kutambua kwamba hakuna nchi yenye kuchukua nafasi ya juu zaidi  kama ilivyo onesha katika orodha kati ya 80 na 100na pia kati ya nchi 44 hakuna nchi katika orodha iliyoko chini ya ponti 30 kama zinavyoonesha katika  orodha. Kwa njia hiyo imesha kwamba Afrika inaanza pole pole katika maendeleo ya uwezo wake wa kisayanzi, kiteknoljia na ubunifui, pamoja na kwamba matokeo bado yana thibitisha uduni kwa kiasi fulani kwasabu nchi nyinu za Afrika bado hawaeki kipaumbele katika utafiti,na uwezo wa kimaendeleo ya kiteknolojiaunasabababishwa na ukosefu wa kubadilishana mawazo na kutimiza ahadi zao za sera kisiasa katika mipango na vitendo vya kukuza ukuaji wa sekta tatu.

Kwa ripoti hiyo inaonesha wazi kwamba bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto nyingi ili kuborehsa matokeo ya kuongeza utatifi, teknolojia , ubunifu na sayansi, ili waweze kuingia katika mashindano kwa ngazi ya kimataifa, na kuruhusu hupatikanaji bora wa Intanaet na katika uwekezaji zaidi wa utafiti na maendeleo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.