2017-04-08 16:07:00

Tume ya Kipapa ya Biblia kukutana tarehe 24-28 Aprili 2017


Tume ya Kipapa ya Biblia kuanzia tarehe 24- 28 Aprili 2017 itakuwa na mkutano wake wa mwaka, utakaofanyika mjini Vatican chini ya Uenyekiti wa Kardinali Gerhard Ludwig Muller, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kwa kushirikiana na Padre Pietro Bovati, Katibu mkuu wa Tume ya Kipapa ya Biblia wataendelesha mkutano huo. Hii itakuwa ni nafasi kwa wajumbe kuweza kushirikishana mada mbali mbali ambazo zimefanyiwa kazi na wajumbe binafsi mintarafu elimu binadamu inayojikita katika Maandiko Matakatifu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.