2017-04-08 10:10:00

Takwimu za idadi ya Wakatoliki duniani kwa mwaka 2015!


Takwimu za maisha na utume wa Kanisa kwa mwaka 2015 zimewasilishwa kwa kutoa picha kamili ya hali halisi ya takwimu za Kanisa Katoliki kwa mwaka 2015.Takwimu hizo kwa sasa zinapatika katika duka la vitabu Katoliki, lakini pamoja na Takwimu hizo, kuna habari nyinginezo zinzaohusu maisha ya kitume ya Kanisa Katoliki duniani tangu kuanzia mwaka 2015. Takwimu zilizotolewa za mwaka 2015 zinaonesha hali halisi kwa ufupi kuhusu maendeleo na utume wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, ambapo Idadi ya wabatizwa katoliki imeongezeka kutoka milioni 1.271 mwaka 2014 kufikia milioni 1,285 kwa mwaka 2015 ni ongezeko la asilimia 1%.Na hiyo ni asilimia 17,7% ya jumla ya watu wote. Ongezeko hilo linaendena na wabatiwa kutoka kila bara , kwa mfano Bara la Afrika , linaonesha  ongezeko la asilimia 19,4% wakatoliki kwa kipindi hicho kutoka  milioni 186 hadi 222.

Wakati Bara la Ulaya linaonesha hali halisi ya mwaka 2015 wakatoliki kuongezeka karibia milioni 286  ambao ni kidogo zaidi ya 800,000 ukilinganisha na mwaka 2010 na milioni 1,3 ikiwa ni pungufu ukilinganisha na mwaka 2014. Kwa upande wa mabara ya Marekani na Asia mahali ambapo taarifa zinasema kuwa kuna ongezeko zaidi la wakatoliki  kwa asilimika +6,7% na +9,1%, lakini ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu  katika mabara hayo Vilevile kwa upande wa Bara la Australia imeonesha upungufu kidogo wa wakatoliki.

Takwimu za Afrika: Takwimu zinaonesha ongezeko  ya  wabatizwa kutoka asilimia 15,5% kufikia  asilimia 17,3% ya dunia. Na kwa upande wa Ulaya imepungua kutoka Asilimia 23,8% kwa takwimu za mwaka 2010 kufikia 22,2% kwa mwaka 2015. Marekani  inakaribia asilimia 49 ya wakatoliki waliobatizwa.Katika bara ya Asia ni karibia asilimia 11% katika ulimwengu kwa mwaka 2015 .Na kwa upande wa Bara la Australia takwimu zinaonesha asilimia 0,8 % ya wakatoliki duniani.Nchi ya Brazil ina  idadi kubwa ya wakatoliki kwa ukilinganisha takwimu za mwaka 2015 ambayo ndiyo ya kwanza kati ya nchi 10 zenye idadi kubwa ya wakatoliki, ikiwa na idadi ya milioni 172,2 ambayo ni asilimia 26,4% ya jumla ya wakatoliki wote wa Bara zima la Marekani. Mexico (110,9 milioni),UFilippini (83,6 milioni),USA (72,3), Italia (58,0),Ufaransa (48,3), Colombia (45,3),Hispania (43,3), Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo (43,2) na  Argentina(40,8). Upungufu wa Mapadre  duniani: Takwimu za mwaka 2015 zinaonesha makuhani duniani  466.215, wakiwa maaskofu 5.304, mapadre 415.656 na Mashemasi wa kudumu 45.255. Mwaka 2015 unaonesha kupungua kwa idadi ya mapadre ukilinganisha na miaka iliyopita kuanzia 2000 hadi 2014. Pungufu kati ya 2014 na 2015 ni 133 ambayo inatazama hasa katika Bara la Ulaya (-2,502) na kwa upande wa Afrika ni +1,133, Marekani +47, +1.104 na Austraria +82.

Ongezeko la mapadre Afrika na Ulaya: Kama Afrika na Asia zinaonesha ongezeko la asilimia +17,4% na 13,3% , bara la Marekani ni asilimia (+0.35), Ulaya na Australia  takwimu zinaonesha kwa kipindi hicho uwiano wa hasi ambao ni kati ya asililia  -5,8 % na -2,0% .Kwa kupembua  kati ya majimbo  na Watawa , takwimu zinaonesha nafasi ya kwanza  kuongezeka kutoka asilimia 1,6% ambayo ni 277.009 kwa mwaka 2010  kufikia 281.514 mwaka 2015. Nafasi ya pili ni kutoka asilimia 0,8% ambapo ni zaidi ya 134,000 kwa mwaka 2015.Ongezeko la mashemasi wa kudumu: Kuna ongezeko la mashemasi wa kudumu kwa mwaka 2015 kwa asilimia 14,4% kulinganisha na miaka mitano ya kwanza kutoka 39.564 hadi 45.255 kwa namna hiyo tunaweza kusema idadi ya mashemasi wa kudumu ni nzuri katika mabara yote.

Kundi la watawa na siyo mapadre: Kundi la watawa ,wasiyo madre wanaunda timu kwa ngazi ya ulimwengu kuonesha upungufu wa miito. Kama ilikuwa inaonesha 54,665 kwa mwaka 2010 , mwaka 2015 wakumekuwa  54,229. Pungufu  hiyo inaelenga kwa upande hasa  wa kundi la Ulaya, Marekani na Astralia, wakati Afrika wahudumu wameongezeka kama na pia kwa upande wa bara la  Asia japokuwa kwa kiasi kidogo.
Upungufu ya watawa wa kike:Takwimu zinaonesha watawa waliofunga nadhiri kwa mwaka 2015 wanazidi kwa asililimia 61% ya idadi ya mapadre wote duniani ambao  kwa sasa wanazidi kupungua.Katika ngazi ya ulimwengu idadi yao ni kutoka idadi ya 721.935 kwa mwaka 2010,kufikia   670.320  mwaka 2015, ambayo ni asilimia 7,1%. Afrika ndiyo inayoonesha ongezeko la watawa wa kike kutoka 66.375 kwa  2010 kufikia 71.567 kwa  2015.
Inafuata Bara la Marekani lenye upungufu kuanzia mwanzo hadi mwisho kutoka watawa  122.213 kwa mwaka 2010, kufikia 112.051 kwa mwaka 2015. Kwa kutazama maeneo ya bara zina ya Marekani ya Kaskazini ni asilimia  (-17,9% ya kundi lote ambayo ni   -3,6% , Ulaya  (-13,4% na -2,7%) Australia (-13,8% na -2,7%). 

Upungufu wa mapadre: Kwa miaka hii miito ya upadre  imezidi kuwa na pungufu kwa mwaka 2015 katika Seminari kuu zimeonesha idadi ya 116.843 kulinganisha na idadi ya 116.939 kwa mwaka 2014, idadi ya  118.251 kwa mwaka  2013, idadi ya 120.051 kwa mwaka  2012, idadi ya  120.616 kwa mwaka 2011 na idadi ya 118.990 kwa mwaka  2010.Kwa upande wa Afrika idadi ya vijana  katika seminari kuu kwa mfululizo wa mika mitano umezidi kuongezeka kwa kipindi hicho kwa asilimia 7,7%. Kwa upande wa Marekani , umeonesha upungufu  wa miito  kufika asilimia 8,1%.Kwa upande wa Kanisa na Mashirika nayo yaonesha upungufu wa miito kufikia mwaka 2013 lakini kwa miaka iliyofuatia , inaonesha ongezeko.

Tofauti na Bara la Asia mashariki ambao imeonesha idadi ya vijana katika Seminari Kuu kwa mwaka 2015 pungufu ya asilimia 1,6 ukilinganisha na ongezeko kubwa la mwaka 2012. Ulaya idadi ya Vijana seminarini  tangu mwaka 2010 hadi 2015 imepungua kwa asilimia 9,7%. Katika bara la Australia ongezeko lilikuwa  kwa mwaka 2012 ; na kwa miaka iliyofuatia, inaonesha pungufu ya idadi ya vijana seminarini kwa mwaka 2015 kwa asilimia ya 6,9% kulinganisha na ile ya mwaka 2012. Bara la Asia kwa ujumla idadi ya vijana semnarini ni wengi:Ni idadi ya 116.843 kulinganisha  duniani kote, kwa mwaka 2015 , idadi ya wasemniari wa Asia  ni  34.741. Wanafuatia Marekani kwa idadi ya 33.512, Afrika idadi ya 29.007, Ulaya idadi   18.579 na mwisho Australia idadi ya 1.004  waseminari.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.