2017-04-08 08:58:00

Serikali ziwajibike pamoja kulinda watoto waathirika wa biashara!


Hatari kwa watoto katika kanda za vita, mifumo ya kuwalinda wadogo na mipango ya maendeleo ya kisiasa yanayofaaa, ni mambo matatu makuu yaliyo jiokeza katika hotuba ya mwakilishi wa Baraza la kudumu la OSCE Monsinyo Janusz Urbancyk wakati wa Mkutano wao wa 17  huko Vienna tarehe 3 -4 Aprili 2017 mada kuu ikiwa ni mkataba wa kukomesha biashara ya mtu.Monsinyo Janusz Urbancyk amekumbusha kwa namna ya pekee aina nyingi za utumwa ambazo watoto wadogo  wengi ni waathirika ambapo imekuwa biashara kuu ya wafanya biashara haramu hao katika kanda nyingi za dunia.

Halikadhalika amesisitiza juu ya kutoa kipaumbele cha kuheshimu haki za kila mtoto ili aweze kuishi katika familia.Ameongeza juu ya kutazama hali halisi ya sasa na hasa kwa upande wa vijana wasichana wengi ambao wameathirika katika biashara ya binadamu, au kufanyishwa kazi ngumu za kunyonywa na pia watoto wengine ni maaskari katika maeneo ya migogoro ya kivita, aidha wengine kuhusishwa kwenye madawa ya kulevya.
Inabidi kukabiliana na kipeo kikubwa hicho hasa cha  wakimbizi na hasa wale watoto wahamiaji, kwa kuwapa mafunzo ya mwanzo katika ngazi ya kimataifa.Hiyo  kwasabau wote wanaweza kuwajibika katika kulinda utu wa binadamu japokuwa suala hili linabaki bado kuwa nyeti la unyonyaji na kuwatumikisha watoto wadogo. 

Kati ya watoto wahamiaji, Monsinyo anakumbusha wale wasio sindikizwa, na kwa njia hiyonameota aisna tati za kufanya , kwanaza kutoa huduma ya kuhakiksha watoto wote wanaorodheshwa katika nchi zao asili ,kuweka molatana ya kimataifa inayotetea haki za watoto, na kuunda nyavu zinzaofaa  ili kukbalibilana na biashara ya binadamo au unyinyaji.Kwa njia hiyo amekumbuka kwa namna ya pekee chama cha Talitha kum , ni chombo cha kimataifa cha maisha ya kitawa kinachopinga biashara ya watu,ambacho kimeweza kufanya utume wake katika nchi zaidi ya 70 duniani, kwa ajili ya kuhamasisha dhidi ya  aibu na janga kubwa la biashara ya binadamu. Kwa kutazama mwongozo ili kukabiliana na makundi haramu ya  biashara ya watu, Monsinyo Januszyk amesisitiza juu ya ushirikiano wa kutosha kati ya sera za kisiasa, nguvu za polisi, taasisi za upelelezi kitaifa na mashirika yasiyo ya kiserikali Aidha umuhimu wa kushirikiana unahitajika hata katika kuhakikisha ulinzi na usalama  wakati wa safari ndefu ya watoto kutoka nchi asili kuelekea zile wanakokwenda.
Na mwisho amesema juu ya msingi wa kutambuzi mahitaji kuhusu mabadiliko ya utamaduni,ambao ndiyo msingi na thamani ya kila mtu inayjieleza katika katika mkataba wa haki za mwanadamu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.