2017-04-06 16:06:00

Ibrahim ni uzao wa Kanisa la sasa, aliamini na kutii Mungu daima


Mungu ni mwaminifu daima katika agano lake: amekuwa mwaminifu kwa Ibrahimu na katika ahadi ya ukombozi wa mwanae Yesu Kristo. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa misa ya Asubuhi Alhamisi 6 Aprili 2017 katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko anahimiza kutafakari kwa dakika 5 au kumi hivi kufikiria kila mmoja historia yake ili kuweza kugundua uzuri wa upendo wa Mungu , hata katika mambo mabaya , ambayo binadamu anakabiliwa nayo.Baba Mtakatifu Francisko akichambua somo la siku kwa kutazama sura ya Ibrahimu amesema, katika historia ya agano la Mungu na Ibrahim ambaye ameitwa Baba na hata  enzi za Yesu  na wafarisayo katika Injili ya siku, ni baba kwasababu Ibrahimu ndiyo uzao wa Kanisa la sasa .Ibrahimu aliamini na kutii alipoitwa kwenda katika nchi nyingine ambayo angepokea urithi.

Ibrahim ni baba wa Imani na matumaini, kwani anaamini alipo ambiwa atakuwa na mtoto, alikuwa na miaka mia moja na mke tasa. Kama mtu anaweza kuelezea maisha ya Ibrahim anaweza kufikiria na kusema huyo alikuwa anaota ndoto anabainisha  Baba Mtakatifu. Lakini pamoja na hayo suala  la ndoto linawezekana japokuwa ndoto ilikuwa ya matumaini, hivyo Ibrahim hakuwa kichaa. Ibrahimu  aliwekwa katika majaribu mara baada ya kumpata mtoto, kwani  akiwa kijana aliomba amtoe dhabihu: yeye alitii na kwenda kinyume na matumaini yake. Huyo ndiye Baba yetu Ibrahim , ambaye anakwenda mbele,na kuonekana katika maneno ya  Yesu akimwelezea   kwamba Ibrahimu aliona siku yake, yaani aliona  na akawa na furaha. Baba Mtakatifu amesema ndiyo aliona ahadi na furaha ya kuona ukamilisho wa ahadi ya agano ,furaha ya kuona kwamba Mungu hakuwa mdanganyifu , Mungu ambaye tumeomba katika wimbo ulio bora, daima ni mwaminifu katika agano lake.

Hata katika zaburi, inatualikwa kukumbuka maajabu na matendo yake. Hayo ni kwa ajili yetu sisi tulio uzao wa Ibrahimu. Ametoa mfano Baba Mtakatifu kwamba huyo ni kama tumfikiriavyo baba yetu mzazi anapo ondoka , tunakumbuka mambo yake  na kusema , alikuwa na mambo makuu baba!
Mkataba kwa upande wa Ibrahimu ni pale alipotii daima , anaendelea Baba Mtakatifu. Kwa upande wa Mungu ahadi yake ni kumfanya awe baba wa mataifa. Kwani alisema,sitakuita tena Abram bali Ibrahimu, alimwambia Bwana. Na Ibrahimu aliamini. Hata katika mazungumzo mengine kutoka kitabu cha Mwanzo , Mungu alimwambia, uzao wako utakuwa kama idadi ya nyota mbinguni na kama mchanga wa baharini. Kwa kuthibitisha hiyo Baba Mtakatifu amesema, leo hii tunaweza kusema kila mmoja wetu ya kwamba  mimi ni mmojawapo wa nyota na pia mimi ni mmoja wa chembechembe ya mchanga.

Katika kutazama historia, Baba Mtakatifu amesema kati ya Ibrahim na sisi kuna Histroria ya Baba wa  Mbingu , ambayo kwa njia ya Yesu anawaeleza mafarisayo kwamba Ibrahim alifurahi kwa matumaini kuona siku hiyo. Aliiona na kujazwa na furaha , na huo ndiyo ujumbe mkubwa wa Kanisa ambalo leo hii wanaalikwa kutoa kwa msisitizo  na kutazama mizizi yetu , kutazama baba yetu kwa yote aliyofanya kwa watu wake, kutazama mbingu iliyo jaa nyota na fukwe zilizojazwa na chembechembe za mchanga. Kutazama historia ni kuona kwamba mimi siyo peke yangu bali mimi ni watu na tunakwenda pamoja kwasababu Kanisa ni watu. Baba Mtakatifu Francisko amesema lakini watu hao wali otwa na Mungu ni watu walio pewa Baba katika dunia, na ambaye alitii, vilevile tunaye kaka aliyetoa maisha yake kwa ajili yetu sisi ili tuwe wamoja. Kwa njia hiyo tunaweza kumtazama Baba  tukashukuru, tukatazama Yesu tukashuru , tukatazama Ibrahim na sisi wenyewe tunaoshiriki katika safari .

Mungu ni mwaminifu, Baba Mtakatifu Francisko amealika  leo hii kufanya kumbukumbu kwa kujaribu kuchanganua historia kubwa iliyoko katika picha kubwa ya Mungu na Yesu lakini kwa utambuzi ya kuwa ndani yake kuna hata historia ndogo ya kila mmojawetu. Na mwisho anatoa mwaliko wa kukaa kwa muda mfupi, dakika tano , kumi bila radio, bila TV kwa kufikiria kila mmoja historia yake kwa kutazama baraka, na vituko, na kila kitu au kutazama neema na dhambi na kila kitu.Aidha ni kutazama pale imani ambayo Mungu amebaki mwaminifu katika agano lake. Yeye alibaki mwaminfu katika ahadi alizokuwa ametoa kwa Ibrahimu , alibaki mwaminifu katika ahadi ya ukombozi wa mwanae Yesu kristo. Na kwa kufanya hivyo Baba Mtakatifu Francisko ana uhakika kwamba kati ya mambo mabaya ambayo kila mmoja anayo ya maisha , tunaweza kugundua uzuri wa upendo wa Mungu , uzoefu wa huruma yake , uzuri wa matumaini, na uhakika kwamba wote tutajazwa na furaha.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.